Liverpool_Jr
JF-Expert Member
- Sep 7, 2019
- 1,220
- 1,411
Kweli SINGLE MAZA sio wa kuoa..
#YNWA
#YNWA
Miaka 9 iliyopita nilimtia mimba Mwanachuo wa mwaka wa 2 akajifungua mtoto wa kiume. Hatukuweza kuoana maana na mimi ndiyo kwanza nilikuwa nina mwaka mmoja mtaani sina mbele wala nyuma.
Hivyo kila mtu alishika 50 zake na kutafuta mwenza wake mpya wa maisha. Lakini malezi ya mtoto niliyabeba kama baba.
Yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumpata mwenza wake wa maisha. Alimpata miaka 7 iliyopita na sasa wana watoto 2 ndani ya ndoa yao
Mimi nilichelewa kidogo kwasababu ya kujipanga kimaisha, ndoa yangu ndiyo kwanza ina miaka 2 na nina mtoto wa miezi 7.
Miezi 2 iliyopita nilienda semina mahali fulani. Nikakutana na mzazi mwenzangu naye akiwa ni mshiriki wa semina ile. Kwa kuwa mke wangu ana katoto kachanga ka miezi 7, na kwakuwa huyu mzazi mwenzangu tumekutana mazingira mapya ya semina, na kwakuwa jicho lilimtamani kwa jinsi alivyo nawiri na kustawi basi semina ilienda vizuri.
Juzi nimepigiwa simu na mzazi mwenzangu akidai ana mimba yangu na mumewe amegoma kuikubali.
Sasa mabibi na mabwana, nawauliza suala hili nilishughulikie vipi?
Naombeni suluhisho la suala hili pasipo kuvuruga ndoa yangu changa.
- Nikubali ama niikatae mimba hii?
- Nikiikataa itakuwaje endapo mtoto atafanana na mm na mumewe anaijua chapa yangu kupitia mtoto wangu wa kwanza?
- Je, nikikubali mke wangu patakalika?