" Nimemteua Dr Mpango kwa sababu ni mtaalamu wa Uchumi atanisaidia kwenye mambo ya Uchumi na Fedha" kauli hii ina maana pana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Rais Samia Suluhu Hassan amesema amemteua Dr Mpango kama makamu wa Rais kwa sababu ni mtaalamu wa uchumi na kwamba atamsaidia katika maswala ya uchumi na fedha.

Rais Samia amesema inaeleweka kuwa ofisi ya makamu wa Rais inashughulika na mambo ya Muungano, Umaskini na Mazingira lakini Dr Mpango atamsaidia katika mambo ya Uchumi na fedha pia.

Yawezekana Dr Mpango akawa bado ni boss wa Hazina " kivingine"

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Waziri wa fedha Mwigulu.
Katibu wa wizara D.James.
Hapa naona miradi aliyoacha JPM inakamilika.
 
Zama za ghiriba kuwa maendeleo hayana chama, Mara wapinzani wametuchelewesha, mara msipochagua CCM sileti maendeleo, zimetwa na wakati.
Kauli hizi zilitumika kukandamiza baadhi ya watu, kuwaumiza, kuwatesa kiakili na kusababisha mpasuko mkubwa sana.
Sasa ni zama mpya, naomba tuzizike kauli hizi za mwendazake ambazo zimeacha majeruhi makubwa kwa walio wengi.
Tumuunge mkono rais wetu SSH, tuijenge nchi pamoja.
 
Tumuunge mkono mama kwa kumueleza ukweli, tukiendelea na utaratibu uleule wa kulamba miguu ili tupewe mkate wetu Kama walivyofanya kina mwigulu, polepole na hata bashiru tutaliangamiza taifa letu.Jambo la msingi uadilifu, haki, uchapakazi na kufuata katiba na sheria za nchi yetu
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema amemteua Dr Mpango kama makamu wa Rais kwa sababu ni mtaalamu wa uchumi na kwamba atamsaidia katika maswala ya uchumi na fedha.

Rais Samia amesema inaeleweka kuwa ofisi ya makamu wa Rais inashughulika na mambo ya Muungano, Umaskini na Mazingira lakini Dr Mpango atamsaidia katika mambo ya Uchumi na fedha pia.

Yawezekana Dr Mpango akawa bado ni boss wa Hazina " kivingine"

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
Okay
 
Back
Top Bottom