Uchaguzi 2020 Nimemsikiliza Mnyika, kama ni kweli kuna tatizo mahali

Kigongoi kwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
447
440
Kwa muda mrefu,sikuwa ninafuatilia masuala ya siasa na hasa za upinzani kutokana na nature ya shughuli zangu nizifanyazo za kila siku,kiukweli nafasi yangu ni ndogo na hata ikitokea nina nafasi uwezo wangu mkubwa kwa eneo nililopo ni kuangalia au kusikiliza vyombo vya habari vya umma.

Nimepata nafasi ya kumsikiliza Katibu mkuu wa CCM na wakati mwingine katibu wa uenezi wa CCM Bwana Polepole wakielezea mambo mbali mbali yahusuyo Chama, serikali na hasa kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Mazungumzo ya Bwana Mnyika niliyoyasikiliza jana yamejikita kwenye mwenendo wa uchaguzi mkuu na katika 'press realize' amelilaumu jeshi la polisi na hasa IGP kwa matukio yanayojitokeza yanayokihusu Chama chao na jinsi wanavyofanyiwa timu zao za uchaguzi na jeshi la polisi. Mbali na hayo ametaka wapiga kura walinde kura baada ya zoezi la upigaji kura. Wakati kimsingi kwa kufanya hivyo inaweza kuleta shida.

Vile vile ameilaumu tume kwa kushindwa kuweka wazi suala la uchapishaji wa karatasi za kupigia kura na pia kaelezea mapingamizi waliyoyawakilisha kwa tume.

Kwa kuwa hayo yote yamezungumzwa na kiongozi wa Chama cha upinzani,kuna haja ya mamlaka zilizohusishwa na malalamiko hayo kuchunguza tuhuma hizo na kuzifanyia kazi haraka ili umma usijenge taswira hasi juu yao kwamba wanaegemea upande fulani.

Na kama ni kweli vyombo hivyo vinaegemea eneo fulani basi pia ni tatizo kubwa sana kwetu watanzania na sio ishara njema kwetu.

Ni rai yangu,haki na amani vikaenziwa.

Asanteni
 
Mnyika anajua baada ya Uchaguzi hana tena mshahara maana kupata hata wabunge wawili ni miujiza

Usione Chadema wanatukana hovyo wanajua hali mbaya
 
Kumbe wanatukana? Ila matusi kwa kikao cha jana sikuyasikia.
Hata hivyo inawezekana wakakosa kweli wabunge kama ulivyosema,basi taratibu na uwanja ukae sawa hata wakikosa wabunge wasilalamike kwamba wameonewa
 
Kupiga kura bila kuzilinda ni kazi bure,ni bora kuacha kupiga kura yenyewe kwa utawala huu wa Afrika. Kukitoa chama tawala madarakani ni lazima itumike nguvu ya ziada .vinginevyo
Anayedhani safari tutakwenda nyumbani baada ya kura heri aanze kuzowea. Vinginevyo bora uchaguzi usiwepo.

Uchaguzi wa nini kama kura anakuja baki nazo Dkt. Mahera afanye nazo lolote apendalo?

Kwa hili tutaelewana tu. Kama vipi hili ndilo litakuwa mwanzo wa goma.
 
Kwa muda mrefu,sikuwa ninafuatilia masuala ya siasa na hasa za upinzani kutokana na nature ya shughuli zangu nizifanyazo za kila siku,kiukweli nafasi yangu ni ndogo na hata ikitokea nina nafasi uwezo wangu mkubwa kwa eneo nililopo ni kuangalia au kusikiliza vyombo vya habari vya umma.

Nimepata nafasi ya kumsikiliza Katibu mkuu wa CCM na wakati mwingine katibu wa uenezi wa CCM Bwana Polepole wakielezea mambo mbali mbali yahusuyo Chama, serikali na hasa kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Mazungumzo ya Bwana Mnyika niliyoyasikiliza jana yamejikita kwenye mwenendo wa uchaguzi mkuu na katika 'press realize' amelilaumu jeshi la polisi na hasa IGP kwa matukio yanayojitokeza yanayokihusu Chama chao na jinsi wanavyofanyiwa timu zao za uchaguzi na jeshi la polisi. Mbali na hayo ametaka wapiga kura walinde kura baada ya zoezi la upigaji kura. Wakati kimsingi kwa kufanya hivyo inaweza kuleta shida.

Vile vile ameilaumu tume kwa kushindwa kuweka wazi suala la uchapishaji wa karatasi za kupigia kura na pia kaelezea mapingamizi waliyoyawakilisha kwa tume.

Kwa kuwa hayo yote yamezungumzwa na kiongozi wa Chama cha upinzani,kuna haja ya mamlaka zilizohusishwa na malalamiko hayo kuchunguza tuhuma hizo na kuzifanyia kazi haraka ili umma usijenge taswira hasi juu yao kwamba wanaegemea upande fulani.

Na kama ni kweli vyombo hivyo vinaegemea eneo fulani basi pia ni tatizo kubwa sana kwetu watanzania na sio ishara njema kwetu.

Ni rai yangu,haki na amani vikaenziwa.

Asanteni
"press realize"

Press release.
 
It’s very sad kwamba watu wanaokuja kutetea chama tawala hawana hata point za msingi. Very sad!! Chama kikongwe kweli!? Inaumiza sana.
 
Hawawezi kuwa Na imani Na jeshi LA polisi, ulisikia Yale ya hai. Mbowe anaambiwa huwezi kushinda
 
Back
Top Bottom