Nimempita GF wangu tofauti ya zaidi ya miaka 17 JE HAPO HAKUNA TATIZO

Mi sioni tatizo lakini tatizo linapokuja ni hapo wewe kuto kuwa muwazi kwa mwanza wako!

Kama unampenda kweli hakuna haja ya wewe kumficha umri wako halisi.
 
Lol! Unatafuta balaa wewe! Mwenzio kwenye diskasheni wanamsimulia stori za sun ciro wewe unaongelea sijui matofali na mashamba! Jamani wadada wa 30 wakaolewe na nani mnaoa watoto?!
Hakikisha una-maintain membership humu, utahitaji stress relieve za kutosha. 19 yrs!!! She could be ur daughter for pity's sake!!
 
Kaka shkamoo...

Hapo kwa age diference ya 17yrs naona tatizo lipo....huyo mboni ni kama mwanao wa kike?..au hilo hata wewe hulioni?...tafuta mwenzio bana atleast age difference isifike double digits...yani iwe kwenye 9 kwenda chini .

Duuh mie mpaka naogopa...hivi huoni hata aibu kuvua nguo kisha unakatiza chumbani bo@#$ro linaninginia na ke@#$nde zako kisha kabinti kanakuangalia??

Hako ukikaoa then miaka mitano ijayo unaanza kuzinguliwa na sugar kenyewe ndio dam full kuchemka..utagongewaje na vijana wa bonge-fleva...aibuu. Mtafute mkubwa mwenzio kama huweza sema tukusaidie kutafuta waliojichokea na midume wanataka kutulia waolewe walee familia.

Ulisema una deg 2??..yani masters?...hukuchukulia hata russia ingekusaidia ungerudi na bibi wako wa kizungu uwe umetupiga bao sie tulio-owa waswahili...

Bora umwambie labda atajifikiria mara mbili mbili!
 
mwaya oa tu
wangapi wameolewa na watu wanawazidi umri na familia zinaenda tena kwa raha zao.

Si kila mwanamke kapitia disko, au anatamani kujirusha. Wengine wamezaliwa wakiwa wabibi tu.
 
Dah... Jamani hakuna kitu kibaya kwenye mahusiano kama udanganyifu... Sasa huo uongo wako unaweza kukugharimu ndugu yangu... Yaani muda wote alikua anajua anampenzi aliyemzidi miaka 7 leo hii aambiwe ni miaka 17.. Ingekuwa mie nakutosa kwa kweli..! Inaelekea sio umri tuu ambao umemdanganya, wewe yaelekea sio Mkweli kwa mambo mengi..!
 
Kwa hiyo unataka kuoa kwa ajili umri unakutupa mkono na wenzako wa umri wako wote wana fam au vipi?
 
Mpigie demu wako story za Waziri mkuu wa Zimbabwe kaoa juzi, tofauti ya umri wao haikuwa ajenda kwenye uhusiano wao! Kwa hapa bongo , cheki kidogo udaku utajua kuna kigogo mmoja (media mogul wa TZ)kaweka ndani kigoli mdogooooooo ukilinganisha na yeye, nadhani jibu unalo sasa, furahia maisha yako.
 
Dah... Jamani hakuna kitu kibaya kwenye mahusiano kama udanganyifu... Sasa huo uongo wako unaweza kukugharimu ndugu yangu... Yaani muda wote alikua anajua anampenzi aliyemzidi miaka 7 leo hii aambiwe ni miaka 17.. Ingekuwa mie nakutosa kwa kweli..! Inaelekea sio umri tuu ambao umemdanganya, wewe yaelekea sio Mkweli kwa mambo mengi..!

dah.....ila wajameni huyu nae alienda far kwakweli! Yaani 7 na 17, kudanganya miaka 10 yote hiyo? Mmmmh!!
 
kwa elimu ya masters unauliza swali kam hilo basi elimu yako ni makorokocho

Na wewe kwani siku hizi kuna masterz tena, pole sana maana huyo ndugu anavoonekana ni kama vile hajitambui kwa hiyo hata hiyo mastaz ni ya kimagumashi
 
huwezi tamani maziwa at 35 wakati hujawahi yaonja.

Mie sasa hivi nianze kulilia milkshake, si watasema mizimu ya kwetu imepnda?

Nimekua nakula viazi baga ntatamani wapi.

ila baada ya muda ubibi unaisha! Lol
 
Lol! Unatafuta balaa wewe! Mwenzio kwenye diskasheni wanamsimulia stori za sun ciro wewe unaongelea sijui matofali na mashamba! Jamani wadada wa 30 wakaolewe na nani mnaoa watoto?!
Hakikisha una-maintain membership humu, utahitaji stress relieve za kutosha. 19 yrs!!! She could be ur daughter for pity's sake!!

hahahaha! umefikiria mbali mno!
 
Back
Top Bottom