Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

Ulifanya kosa kubwa sana kama hukuwa na mpango nae tokea 2008 na bahati nzuri kikazi mko mikoa tofauti si ndiyo ilikuwa nafasi nzuri ya kukata mawasiliano? Kama uliendelea kuwasiliana nae kwa kipindi chote hicho 5yrs basi anakufaa hizo kasoro zingine zitarekebishwa mbele kwa mbele maana inaonyesha chance yako kupata mwanamke mwingine ni ndogo ( from 2008 to 2012 hukuweza kupata girlfriend mwingine).
 
mimi naamini kabisa ulitaka kuzaa na huyo dada la sivyo ungetumia kinga,, cha maana hakikisha unamtunza mama mpaka mtoto atakapozaliwa halafu mkubaliane cha kufanya juu ya mtoto.
 
Kwanza ww elimu yako haijakusaidia ktk kote,yaan unatafuta master halafu unakua na uhusiano na bint ambye humpend na unagonga kama uko mbinguni,yaan hata mimi nakushnda m2 ambaye cna future nae sigongi peku,ww unazan kondom ziliwekwa ajir ya ukimw n mimba au uldanganywa kama Adam?
Ushauri,mwache ajifungue 2,ulee ila ukome usirudie tena,m2nze ukisema umkatae walai upati tena mtoto,na hta ukimpata mwanamke unaempenda akikwambia ana mimba yako jua kekundu.
 
yaani mlikua mnapigana kavu kavu aisee...tutaangamia wengi sana. Mi ningekushauri ubebe mzigo tu maana ungekua humtaki ungetumia protection...starehe umepewa saivi unataka kukimbia
 
habari!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi Univeversity) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.

Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia hama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.

Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.

Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?


Clean your own mess!
Marry her and learn to love and appreciate her. She loves and adore you, nafikiri ni kitu ambacho watu wengi humu tungependa ("to be loved"). Usiende mbali, angalia wenzako wanavyolilia mapenzi, wewe huyataki unataka kupenda kungine ambapo hilo penzi lako laweza lisirudishwe.

Au be a coward, and irresponsible muache azae huyo mtoto aje alelewe na baba mwingine.
 
Mbona maelezo yako umeyatoa vizuri tu na umeonesha kabisa unachokitaka, hufikirii kutoa mimba, unataka mtoto azaliwe salama, hutaki kuwa na watoto wa mama tofauti( hufikirii kuja kuzaa na mwingine) sasa unaomba ushauri upi kiongozi?
Kajitambulishe kwa binti haraka iwezekanavyo. Huyo ndio kashakuwa mkeo tena, kama uliweza kuwa nae kwa miaka 5 tena mko mikoa tofauti nini shida sasa rafiki?
Peleka posa, toa mahari kuwa na binti hasa kipindi hiki yu-mimbani, anahitaji sana ukaribu wako aisee, hata kama harusi itasubiri kidogo ila usithubutu kutoa hiyo mimba wala kumtelekeza huyo mama. Amekusaidia kukupunguzia mahamu yako wakati wa chuo umjali sasa na yeye please. Tena una bahati unasema anakupenda sana, huoni fahari kuwa na mke anaekupenda sana? Angalia usije kupata gume gume likaja kukusumbua katika ndoa

Nimeona like haitoshi.
Usipofuatilia ushauri huu pamoja na mingine, ujue kuna janga unalitafuta. I can only wish you whatever you deserve!
 
wewe kaka unatuletea comedy hapa jf, hutaki kuzaa watoto wa mama tofauti at the same time hutaki kumuoa huyo dada, kwanini uli-do bila kutumia rambo?

hilo ni chaguo ulilokupa mungu. huwezi kufanya mapenzi kwa mtu usiyempenda labda utuambie huyo dada alikubaka
 
I hate hiyo sentensi, maana nilishaambiwa hivyo wakati nimeenda home kujifungua mtoto wangu wa ujanani. i met vijana ambao tumekuwa nao kitaa nikiwa nasukuma mtumbo; halafu mtu ananiambie, "hivi Kaunga, matangazo ya condoms wewe hujawahi yaona?"

Ukweli mchungu
kwani uongo kaunga..?
wewe ulijiachia tu...ulitegemea nini?
 
5 years kwenye relationship na mtu usiyempenda??acha kutudanganya..tena unasex nae bila condom afu unasema humpendi??aisee elimu yako haijakusaidia!
 
kwani uongo kaunga..?
wewe ulijiachia tu...ulitegemea nini?

Ndio maana nilisema ukweli mchungu.
Mimi niljiachia kwa kuwa kwanza na tamu that way; lakini pia nilitaka mtoto, na sijawahi juta. He is a reason for everything right now, l mean my sonushka!
 
Kaunga, kumbe wewe ndo huwa unanifuata? Eiyer, njoo umtoe huyu mkeo, kaniganda kama ruba lol

I hate hiyo sentensi, maana nilishaambiwa hivyo wakati nimeenda home kujifungua mtoto wangu wa ujanani. i met vijana ambao tumekuwa nao kitaa nikiwa nasukuma mtumbo; halafu mtu ananiambie, "hivi Kaunga, matangazo ya condoms wewe hujawahi yaona?"

Ukweli mchungu
 
Last edited by a moderator:
wewe kaka hukuwa na nia ya kumuacha huyo dada. tangu 2008 na mpo mikoa tofauti, leo ni 2012 kapataje mimba yako? ingekuwa kweli humpendi kama ulivyosema, alipomaliza chuo na kupata kazi tu ungeachana kabisa naye, sasa wewe nanii yake unaitumia, alafu unasema humpendi, tukueleweje? huyo oa tu ndugu yangu
 
Huyo kama humpendi jua hata ukimwambia atoe hatakubali. hiyo ndo imekula kwako madhee. naomba mumlee mtoto kwa mapendo. mtu mzuri ni yule aliye lelewa na baba na mama. mwambie ahudhulie clinic. Mia
 
Kumbe ndo maana wewe ni philosopher?
It's good though to have someone call you 'mom'

Ndio maana nilisema ukweli mchungu.
Mimi niljiachia kwa kuwa kwanza na tamu that way; lakini pia nilitaka mtoto, na sijawahi juta. He is a reason for everything right now, l mean my sonushka!
 
Ndio maana nilisema ukweli mchungu.
Mimi niljiachia kwa kuwa kwanza na tamu that way; lakini pia nilitaka mtoto, na sijawahi juta. He is a reason for everything right now, l mean my sonushka!
kumbe tamuuu eeeh ngoja nijilipue na mimi siku moja nifaidi utamu..
 
Kumbe ndo maana wewe ni philosopher?
It's good though to have someone call you 'mom'

You have no idea, ukishapata ndio utaelewa. He is big, 11 yrs now!

Sio hivyo tu, anasema l am the best mom in the whole world!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom