Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

Miaka 34 ni umri mkubwa na hauwezi jua Mungu kakupangia vp make takea 2008 mpaka mwaka huu ni muda mrefu sana. kama haukuweza pata mwingine hapo katikati mpaka mimba ukampatia nakushauri Muombe mungu akupe moyo wa kumpenda na kumuoa ili mtunze mtoto wenu mtarajiwa. ni hayo tu.
 
Mkuu pole sana ?Sasa wewe unaomba ushauri gani kwa wanajamvi? Unataka wakupe ushauri gani sasa ikiwa majibu yote ambayo ingetakiwa ujibiwe ushayatolea maelezo?
Mwanamke humpendi,ume mpa mimba,umekuwa naye 5yrs,

wewe unampenda sana huyo mwanamke sema hujajua na hujijui ni kiasi gani unampenda..Hivi wew hushangai umekuwa naye kwa 5yrs tena mkiwa mikoa tofauti na umeweza kumpa mimba na mda wote huo hukumtafuta huyo unayezania kuwa unampenda au unapenda awe na sifa uzipendazo.

Mim naomba unipe sababu ni kwanin unasema humpendi huyo mwanamke mwenye mimba yako ni nini? Au kipi kinachofanya usimpende?

Ukitoa sababu ndiyo hapo watu watapata pakuanzia kukushauri.

Kaa jipange upya mkuu ungejua ni jinsi gani unampenda huyo mwanamke hata usinge anzisha huu uzi hapa.Sema tatizo lako hujijui.
 
ni wako huyo, kama hukumpenda why uliendelea kuchovya chovya?au hujui bandu bandu humaliza gogo? sasa ndo unaye huyo ubebe tu mazima. Ila mi hapa sipati point yani mtu humpendi uliwezaje kuwa na uhusiano nae kwa miaka almost 5??hainiingii akilini, ninachoona hapa ni unyama na kukosa fadhila kwa kumtumia binti wa watu kwa miaka 5 alafu leo unasema humpendi. Ungetafuta mazingira mazuri ya kumwambia ukweli mapema ambao haungeleta madhara ili uachane nae mapema aangalie ustaarabu wake na ajaribu bahati yake kwingine. Sasa by now ukiamua kumuacha ndo waweza sababisha madhara makubwa sana.
 
Nachelea kusema ni mtoto wa nje ya ndoa kwani bado sijaoa. Nawaza kutooa kabisa ili nisiwe na mke niseyekuwa na furaha naye na pia nisiwe na watoto wenye mama tofauti tofauti
kama ni hivi mlipie basi mahari halafu mwache akae kwao uwe unazaa naye tu mpaka upate idadi kamili ya watoto unaohitaji
 
kama ni hivi mlipie basi mahari halafu mwache akae kwao uwe unazaa naye tu mpaka upate idadi kamili ya watoto unaohitaji

Angel nashukuru kwa ushauri lakini hapo nitakuwa nimemgeuza mtoto wa watu kiwanda cha kunizalia watoto.
 
Acha hizo wewe .ukishaachia mambo yako sasa unataka kusepa.utapata dem naye atakufanyia hivyo na hapo ndipo utakapokua
 
Hebu sema ukweli...Una mpenzi mwingine? Angalia usije ukaruka majivu ukaenda kukanyaga MOTO.!
 
hapo dawa ni wewe kuanza kumpenda,kwanza inaonekana wewe una hofu ya mungu which is good!!mungu awabariki sana
 
mimi naona limuepukalo mtu lina kheri naye...huyu bwana mimi naona afuate moyo wake kwani ndoa sio ya kujaribisha kama nguo, asije akamuoa huyo dada 'basi tu' akaishia kumtesa dada wa watu..ebu tuangalie mbali kidigo. Pia inawezekana huyu bwana ana mtu wake mwingine anayempenda kwa dhati ndio maana anakuwa hajui anataka nini zaidi....ila NINIMLAUMU sana huyu jamaa kwa kumpotezea muda huyu dada, kwani ungemwambia na ukastick katika msimamoo wako kuwa hutegemei kuja kuwa naye km mke na mume ungepungukiwa nini? kuwa makini, muhimu hapo jicommit kumtunza mtoto, ila suala la mapenzi na huyo dada liweke wazi ili asije umia mtu either wewe, yeye au mtoto au huyo 'unayempenda' wewe....na hata ukija kuoa mwingine umjulishe kuwa una mtoto tayari usije fanya siri ikakutokea puani....kuwa muwazi, fuata moyo wako!
 
Wewe ndio unaconfuse the whole issue. Kumbe mlimaliza mwaka 2008 na ulifanya hivyo ili asiache chuo sasa baada ya hapo ulikuwa na ulazima nae gani. Inamaana ulipendezewa kupewa malovey dovey kwahiyo ni lazima uchukue majukumu yako ndio ishatokea kuwa utakuwa na mtoto wa nje.

Endeleza uhusiano na kutunza mimba hii itasaidia kutokumdhuru mama na mtoto kutokana na hali yake ya ujauzito kwa sasa. Akishazaa ndio bwaga manyanga hiyo kitu ya kuwa hutaki watoto na mama tofauti hauko tena kwenye uwezo wako labda ukane mimba tokea sasa.

Swali langu kumbe unajua unachokitaka kwanini uliishi nae goddamn more 5 years ya kumpa matumaini....halafu mnasoma Masters ambazo kufikiria logic things doesn't even help you.
 
watu wengine bwana ndio maana kuzimu watakutana wengi sana wa sampuli kama yako...sasa kutesa mwanadamu mwenzako kwakuwa anakupenda ndio ujanja?? sikusapoti kabisa ndugu.don't abuse her love for you..this is purely an abuse of which no reasonable man can agree with..
 
umenikumbusha ile statement ya 'sitaki nataka'. Inaweza kuwa vigumu sana kumuacha na hasa akiamua kung'ang'ania kwa kuwa ana kiumbe chako tumboni. Mimi nashindwa kuelewa sehemu moja tu. Unashindwaje kama mwanaume kukaa naye vizuri na kupata hitimisho la mahusiano yenu kama mlivyokaa mlipokutana hapo mwanzo wakati mnatongozana. Ustaarabu wa leo hii kuachana wala si ugomvi. Kaeni chini mpate suluhisho . Ukumbuke pia kwamba umri wako hausimami
 
lakini jamaa hampendi....raha ya ndoa kupendana.....mapenzi ya kuoneana huruma hayafai....
kaka mwenye thread.....nakushauri fuata moyo wako.....

Preta preta preta, uliwahi kuona mtoto akilelewa na mama wa kambo au baba wa kambo? kosa ni la mleta mada kupiga kavukavu sasa asije akapelekea mateso kwa mtoto siku za baadae..
 
habari!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi Univeversity) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.

Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia hama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.

Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.

Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?



Endelea nae mpaka ajifungue salama na umsaidie malezi ya mtoto na baadaye utafute unayemuhisi atakufaa kuwa mke wa ndowa. Tilia maanani kuwa kati ya sifa za huyo mke wako wa baadae utakaemtafuta, ni ya kuwa tayari kumlea mwanao.
Hali uliyojiingiza haikupi uhuru wa kuamuwa kupata kila unachotaka hivyo lazima upangue matarajio yako yaende na hali inayokukabili. Kama utaamuwa kumfunza hayo mambo unayoyataka awe nayo mkeo mtarajiwa itakuwa solution nzuri zaidi.
 
chal, hebu kaa chini kwanza uanze kufikiria upya, kwani unaweza jikuta unakataa pema, unakimbilia pabaya, Pili fikiria kama ingekuwa ni wewe ungejisikiaje?????????. Huyo ndio mke sahihi kwako. Kaeni chini mzungumze kama kunatofauti mzimalize muanze maisha upya. Niliwahi kukutana na tatizo kama lako ila mimi niliahidiwa ndoa, nikajitunza vema, nikitegemea sikumoja tutafunga ndoa. Matokeo yake niliachwa njia panda.Niliumia sana siku na jinsi, baadae nikaja kuolewa na ninafurahia maisha vema sana . Ila upande wa pili Mwenzangu yaliyompata mpaka leo anajuta, alishakuja na kunitolea machozi lakini ilikuwa toooo late. ameoa mke si mke ni matatizo, ukisikia ndoa ndoano ndiyo yake. So please kaa chini ufikirie usije juta baadae.
 
habari!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi Univeversity) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.

Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia hama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.

Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.

Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?

Kama hukumpenda mbona "uboho"wako ulisimama?na ukamuingizia mpaka kapata mimba binti wa watu?Kwani ukipanda korosho unatarajia kuvuna nn?au unataka kumtema kiaina?
 
Nachelea kusema ni mtoto wa nje ya ndoa kwani bado sijaoa.
Nawaza kutooa kabisa ili nisiwe na mke niseyekuwa na furaha naye na pia nisiwe na watoto wenye mama tofauti tofauti
Acha utoto mdogo wangu, cha kufanya badili mawazo yako jitahidi na kumwomba Mungu akusaidie ili uanze kumpenda huyo dada mfunge ndoa na kuanza maisha ya pamoja kama mke na mume na kulea mtoto wenu. Natamani sana ningeonana na wewe nikakushauri sana. Kwa sababu unaposema humpendi lakini bado ulikuwa radhi kufanya naye ngono mpaka kumpa ujauzito, nadhani kuna tatizo moja tu kuna vitu au tabia unataka awe navyo ambavyo nafikiri ukimkubali utakuwa umetatua tatizo kubwa sana kwani hutaona tena mapungufu aliyo nayo kama unavyoona sasa. Kitu cha msingi ni kwamba yeye ni mwanadamu, tena mwanamke na wewe ni mwanaume. Kwa hiyo, huo ndio msingi (au katika falsafa yaani philosophy tunaita substance) hayo mengine ya mvuto, tabia, na mengine ni accidentals ambazo zingine zinaweza kujengwa kwa mazoea tu.
Nakushauri na kukusihi sana usimwache huyo dada na kamwe kamwe msifikiri kufanya abortion kwani hapo mtakuwa mmedondoka shimoni kabisa. Cha msingi kubaliana na hali na ufute ndoto za kutooa kwani hutaweza na utaishi maisha ya kihuni kabisa.
 
Duniani kuna kazi ...kwa nini mlikuwa mnabanjuana bila protection kama ulikuwa humpendi?
 
basi mpe sumu huyo dada maana hueleweki....
wanaume wa siku hizi ndo maana k yangu ipo closed kwa muda....upepo sio mzuri kabisaaaaaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom