Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chal, Jun 10, 2012.

 1. C

  Chal Senior Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  habari!
  Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi University) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.

  Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia kama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.

  Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.

  Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?

   
 2. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Duh! Mtoto wa nje ya ndoa huyoo yu aja ...........Kama kawaida ya wanaume wa siku hizi
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Toka 2008 na kapata ujauzito mwaka huu, hiyo ni good 5 years. Gaademu...
   
 4. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  mungu wa siku hizi ni vodafasta,wewe mtelekeze huyo dada uone malipo yako chapchap!
   
 5. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pole! Ulipokuwa unaingia ktk soft center pekupeku ulitarajia nini mkuu? after all, una uhakika gani kuwa hiyo mimba ni yako?
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  haukuwahi kusikia matangazo ya kutumia kifudusi(condoms)??????????
   
 7. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  muoe huyo dada,kwanza yaonyesha anakupenda sana,ina maana ukimuoa hawezi kuwa na macho ya nje,mtadumu ktk penzi,na mtalea mwanenu pamoja!
   
 8. C

  Chal Senior Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sifikirii kumtelekeza mtoto lakini pia sifikirii kumuoa mama yake mbaya zaidi sihitaji kuwa na watoto wa mama tofauti.
   
 9. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii kali,yani ww huna mapenzi na huyo binti lakini uliweza kupiga kavu???!! Sasa unataka msaada wa nn?!
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  lakini jamaa hampendi....raha ya ndoa kupendana.....mapenzi ya kuoneana huruma hayafai....
  kaka mwenye thread.....nakushauri fuata moyo wako.....
   
 11. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mbona maelezo yako umeyatoa vizuri tu na umeonesha kabisa unachokitaka, hufikirii kutoa mimba, unataka mtoto azaliwe salama, hutaki kuwa na watoto wa mama tofauti( hufikirii kuja kuzaa na mwingine) sasa unaomba ushauri upi kiongozi?
  Kajitambulishe kwa binti haraka iwezekanavyo. Huyo ndio kashakuwa mkeo tena, kama uliweza kuwa nae kwa miaka 5 tena mko mikoa tofauti nini shida sasa rafiki?
  Peleka posa, toa mahari kuwa na binti hasa kipindi hiki yu-mimbani, anahitaji sana ukaribu wako aisee, hata kama harusi itasubiri kidogo ila usithubutu kutoa hiyo mimba wala kumtelekeza huyo mama. Amekusaidia kukupunguzia mahamu yako wakati wa chuo umjali sasa na yeye please. Tena una bahati unasema anakupenda sana, huoni fahari kuwa na mke anaekupenda sana? Angalia usije kupata gume gume likaja kukusumbua katika ndoa
   
 12. C

  Chal Senior Member

  #12
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inawezekena uko sahihi kabisa osaka, lakini kwasasa hilo halina mjadala kwani imeshatokea.
   
 13. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #13
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Jaribu kumpenda kama akupendavyo, kumpata mwenye mapenzi ya kweli siku hizi si rahisi.........maana umesema una miaka 34, ujue wakati haukusubiri wewe na maji yakishamwagika hayazoleki.......just be a man about it
   
 14. C

  Chal Senior Member

  #14
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nachelea kusema ni mtoto wa nje ya ndoa kwani bado sijaoa.
  Nawaza kutooa kabisa ili nisiwe na mke niseyekuwa na furaha naye na pia nisiwe na watoto wenye mama tofauti tofauti
   
 15. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Maswali mengine bana? Unamajibu mkuu, chagua majibu 3 kati ya haya yatakupa mwelekeo
  a. Hutaki mtoto wa mama tofauti
  b. Humpendi mwanamke
  c. Unataka mtoto azaliwe salama
  d. Hutaki kutoa mimba
  e. Unataka mtoto
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,610
  Trophy Points: 280
  Priority yako kwa sasa ni kuhakikisha ujauzito wake uko salama mpaka hapo atakapojifungua kisha kutoa pesa za matunzo ya mtoto bila kukosa na kuvunja kabisa mahusiano ya kimapenzi na huyo mdada kabla hajapata mimba nyingine...Labda mtoto akizaliwa unaweza kubadili mawazo na kuamua kuishi naye kama mke.
   
 17. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe ***** kweli, yaani kukutishia kuwa ataacha Chuo, ndio kisa cha kuendelea kuwa naye!, kwanini na wewe hukumtishia kama ataendelea kukung'ang'ania utahama Chuo mbali ya Tz, eti aache Chuo, thubutu, alikuja Chuo kusoma au kukufuata wewe!, angejuana na maisha yake na familia yake, alikosa kabisa wengine hapo Chuoni, yaani unalo, huruma yako, itakukomesha, na kisa mpaka cha kumvulia nguo or hasa kuendelea kumvulia nguo, hukujua hilo lingeweza kutokea, tena kwa yeye kujitegesha kabisa, ilitakiwa usido naye kabisa, toka ulipoanza kumweleza ukweli kuwa hufeel kuwa naye, ungeacha kudo naye na utafute Girlfriend mwingine, amuone kabisa akija kwako kukupikia na kukusafishia nyumba, unafikiri angekuganda tena, na huyo GF wako ungemweleza ukweli, ili asibabaishwe na maneno ya wachonganishi na wambeya, but nakushauri usimwoe, kama vipi, mtoto akae na wazazi wenu or wako, oa unayemtaka, usijikoseshe raha katika ndoa my Bro.
   
 18. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inaelekea binti huyo anakupenda kwa dhati.pili binti anaujauzito wako hivi Mungu unataka akuoneshe nini ili ujue huyo ndio chaguo lako.
  Pole kwa mawazo yako finyu ambayo hayana uwezo wa kupambanua mambo kwani we ulivyo ingia kwenye uhusiano ulikuwa unamaana gani licha ya hivyo mlipo kuwa faragha ulisahau kutumia dawa ya penzi.
  Sina mengi ya kuandika maana Ndoa umeitaka mwenyewe.
   
 19. C

  Chal Senior Member

  #19
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nachelea kusema ni mtoto wa nje ya ndoa kwani bado sijaoa.
  Nawaza kutooa kabisa ili nisiwe na mke niseyekuwa na furaha naye na pia nisiwe na watoto wenye mama tofauti tofauti
   
 20. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ok! Huyo mdada yaelekea anakupenda sana, na alikuwa tayari kuacha chuo kwa ajili yako; Tatizo ni nini hasa?
   
Loading...