Nimemkumbuka Nyerere namlilia tena Nyerere. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimemkumbuka Nyerere namlilia tena Nyerere.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaa la Moto, May 31, 2011.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa nina miaka 50+ na nimekuwa na mawazo sana hadi kumlilia Nyerere. Nimejaribu kumuangalia nyerere na nimelazimika kulia kabisa. Hakika watanzania tumepoteza lulu. Wale watanzania wa kizazi cha jana wanaweza wasijue hili lakini wale wa kizazi chetu tutamkumbuka daima. Nimegundua kwa nini wanasiasa umtumia Nyerere kwenye midomo yao. Nimegundua kwa nini tumepoteza tumaini kuu katika maendeleo ya nchi yetu.
  Wakati namfikiria Nyerere nimeshangaa sana jinsi mtu huyu alivyokuwa na maono makubwa sana kuhusu nchi hii. Jamani Nyerere alikuwa na maono makubwa sana kuhusu nchi hii ya Tanzania na alikusudia kuijenga nchi hii.

  Nimegundua Nyerere alijua kitu kile kile wanachojua wachumi wetu kuwa nchi inapata maendeleo kwa kuwa industrialized na kwa kujua hilo aliifanya nchi kujenga viwanda vingi sana ili kuongeza uchumi wetu. Sidhani kama alikosea. Hapana, alijua nini alikusudia kufanya na wapi alikusudia kuifikisha nchi hii. Leo kama laiti tungelipata viongozi wenye maono kama Nyerere tungekuwa na nchi iliyo na neema ya viwanda kuliko nchi nyingi za Africa ukiondoa Africa kusini. Leo kwa mfano Kenya inaonekana imekuwa kiviwanda lakini kwa sasa hivi kwa maono aliyokuwa nayo Nyerere hakika tungelikuwa mbali kuliko hata Kenya.

  Ebu tujikumbushe kidogo. Nyerere akijua umuhimu wa kujenga taifa lenye viwanda kwanza aliunda taasisi iliyokuwa ikijulikana kwa jina la NDC (NATIONAL DEVELOPMENT CORPORATION) ambalo kwa kiswahili lilijulikana kama (SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO) ambalo lilipewa jukumu ya kuleta maendeleo ya kiviwanda na kwa kweli lilifanya kazi ya kutengeneza viwanda vya kila aina kiasi kwamba kila kitu kingeweza kuzalishwa hapa Tanzania. Kwa Nyerere viwanda na mining ilikuwa ni maendeleo. Wakati yeye alianzisha shirika hilo wenzetu waliomfuata wao walianzisha tume ya kuua yote aliyoanzisha Nyerere kwa kuunda tume ya ubinafsishaji wa mali ya umma (kwa maana nyingine tume ya kuharibu mipango yote ya Nyerere).

  Nimekuwa nikifikiria ni viwanda vingapi viliasisiwa na Nyerere hata nimeshindwa kuhesabu kwa wingi wa idadi. Nakumbuka kulikuwa na viwanda vyote katika fani za ujenzi, Viwanda vya sementi Tanga,Twiga, Mbeya, viwanda vya nondo, viwanda vya misumali, Kiwanda cha mabati ambacho kiliitwa aluminium na kilitengeza pamoja na mabati pia vifaa vya nyumbani kama masinia glass za aluminium, mabakuli, masufuria na vitu vingine, aliasisi Kiwanda cha kutengeneza vioo kikiitwa kwa jina la Kioo ltd kikitengeneza sio vioo vya ujenzi tu bali hata vifaa vingine vya kioo kama glass, sahani nk, kulikuwa na viwanda vya kutengezeza mabomba ya aluminium na plastic, aliasisi ujenzi wa viwanda vya vifaa vya umeme kule Tanalec kiasi walizalisha hadi transformer na vitu vingine vya umeme, alianzisha viwanda ambavyo vilitengeza bidhaa za mbao kama ceiling boards na chip boards, kulikuwa na kiwanda cha kutengeneza almas kule Iringa hivyo hakukuwa na haja ya kusafirisha madini yetu kwenda kuyafanyia finishing nje. Ina maana yaliongezwa thamani hapa hapa kwetu, alianzisha viwanda vya kutengeneza packing materials kama kile kilikuwa kinatengeneza maboksi na kile cha kutengeza makopo ya packing! Alitengeneza viwanda vya kuprocess nyama na hakuishia hapo tu alitengeneza na viwanda vya kuprocess ngozi ili kuziongezea thamani, hatuwezi kusahau viwanda vya kutengeneza nguo kama mwatex, kiltex, urafiki na vyote vya aina yake. Akaanzisha viwanda vya kutengeneza mablanketi, nyuzi kule Tabora na hapo usisahau viwanda vya kutengeneza zana za kilimo, kwani sikuwa na haja ya kununua panga, jembe, slasher, wheelbarrow kutoka china, hakuishia huko tu akaanzisha viwanda vya kuunganisha magari kule Kibaha, akaanzisha viwanda vya kuunganisha matrekta, kujenga board za magari, viwanda vya kutengeneza betri za magari, Kiwanda cha kutengeneza betri za majumbani Cha National, hatungekuwa na haja ya kuagiza betri duni toka china. Sijasahau jinsi ambavyo alianzisha kiwanda cha kutengeneza pipi, biscuits, jiuice, kachumbali kule Iringa. Sijasahau kiwanda cha kusindika Kahawa alichokijenga kule Bukoba ambacho ni moja kati ya viwanda viwili tu Afrika vya aina yake. Nakumbuka kile kiwanda cha Amboni , kile cha kuzalisha mbolea kule Tanga. Sijasahau sabuni za rumi, mbuni na Ilula. Sijasahau Mashirika ya uvuvi aliyoasisi ili kuongeza pato kutokana na uvuvi maliasili ya baharini na ziwani, sijasahau shirika la Stamico alilounda kuratibu shughuli za madini yetu ambayo leo yanavunwa bila utaratibu na bila aibu tunaambiwa yametunufaisha na sasa watu wanapigwa risasi na kuuawa, Sijasahau kile kiwanda cha kutengeneza matundubali, kiwanda cha kutengeneza baiskeli za Swala na spea zote za baiskeli, kiwanda cha general tyre, kiwanda cha viberiti, viwanda vya maziwa, viwanda vya kusindika tumbaku, Pamba na Alianzisha benki kadhaa kuwasaidia wananchi mbali na zile alizotaifisha. Alitaifisha kiwanda cha sigara na kukiendeleza na sasa wamerudishiwa wakoloni wale wale mambo leo, usinikumbushe kiwanda cha bia, Tanzania distilleries kinachotengenza konyagi, kiwanda cha pombe ya walala hoi kibuku, Kiwanda cha mvinyo Dodoma, kiwanda cha vigae na unaweza kuendelea na orodha kama unakumbuka.

  Kila nikikumbuka namlilia Nyerere. Nasema namlilia Nyerere si kwamba hakuwa na mapungufu!, la hasha namlilia kwa sababu tumepoteza kiongozi aliyekuwa na maono ambayo yamepotea! tumepoteza kiongozi ambaye aliona ambako waliomfuata hawakuoana.
  Najua kuna hoja dhaifu kuwa utandawizi usingeepukika, Sawa lakini si utandawizi ungetukuta na mali zetu? mbona badala ya kuziboresha tumeziua huku tukiwadanganya watanzania kuwa watanufaika wakati si kweli? Nina kila sababu ya kumlilia Nyerere. Nalilia kifo cha maono yake, Naililia Tanzania isiyokuwa na tumaini maana kila aliyemfuata alikuwa na kusudi la kufaidi peke yake kwa kuyaua yale aliyoanzisha. Namlilia Nyerere!
  Kweli bado tuna tumaini la maono yale yaliyoanzishwa na Nyerere? Nani tena anaweza kurudisha tumaini hili? Nani atawarudishia watoto wa Kitanzania tumaini la nchi yenye viwanda tena akiwa mkweli mpaka nafsini mwake? Nasema nani???????????

  Je wewe unakumbuka aliyoanzisha Nyerere ambayo sikuyataja? ebu endeleza orodha hii ndefu alafu utagundua kwa nini namlilia Nyerere!
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Oh yeah Nyerere alitushinikiza kuufurahia umasikini wetu na kujiendeleza bila kupata misaada ya mtaroni; hakutaka Madini yetu yachimbwe na Wajuaji ambapo sisi hatuna na hatujui technology ya kuzalisha huu utajiji wetu ardhini...

  Alitaka tuuenzi mpaka hapa kama ni Wajukuu zetu au Vitukuu zetu wataweza kuwa na Elimu ya kutosha na ku-control 100% as Openheimer family in South Africa.

  Baada ya yeye kuondoka Vijiongozi wetu Uchwara na matumbo makubwa yaliyo na njaa wakaanza hizo biashara uchwara serikali inachukua only 3% what i can say is I hate this kind of monopolization and steal our wealth in most intensely and all its manifestations
   
 3. A

  Albimany JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Nakumbika alitawala miaka 25 alitaifisha mali za wahindi na viwanda vidogo vidogo na tulikua na mashirika mengi ila nakumbuka kama sikosei mashirika yale yalikufa moja ya baada moja wakati akiwa mtawala bado.

  Kama kuna sifa naiona ya kumpa Nyerere ni hii ya kukichagua kiswahili kua ndio lugha ya taifa,kwa hili nampongeza ila sijengine.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]In Nyerere's era, it would appear that every child in the country has had his/her chance of benefiting from our mother country's minerals after we establish our own capacity to exploit them, that a few elite predators today enjoy, but the large poor remainder of the population, who suffer sometimes because of the small but with wider ramifications decisions of the predator politicians, are destined to perpetual wildness of abject poverty.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]‘The unconscious mind is often sentimental'[/FONT]
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Si kweli kwamba haya mashirika yalikufa akiwa hai nadhani huu ni upotoshaji.
  Anyway, ebu tuangalie vision aliyokuwa nayo. Huu uroho wenu baadhi ya watanzania ndio mwanzo wa kufa mashirika haya lakini vision yake ilikuwa perfect! Na walioua mashirika hayo ndio bado mko madarakani. Ole wenu siku watanzania tukiamka usingizini mtatukoma!

  Unajua hata mimi ukinipa uongozi leo ujue naweza kutaifisha mali ya wezi wote wa raslimali zetu. Najua kuna watu wengi wamewaibia watanzania kwa nini wapete wakati watanzania wanatoswa? Hakika na mimi ningehukumiwa kwa dhambi hiyo ya kutaifisha.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimekumbuka na kiwanda cha tiper kinachosafisha mafuta. Nimekumbuka na vile viwanda vya korosho! Nimekumbuka shirika la kuzalisha vifaranga wa kuku.........looooohhhhhhh jamni ni vitu vingi. Je tuendelee kumhukumu kwa kushindwa kwetu kuvitunza na kuvienzi?????? Mungu wangu saidia Tanzania!!!!
  Nimekumbuka zile hotel za kitalii za Kilimanjaro, Kunduchi, Mwanza, Embassy, na endless list ya hotels za kitalii.......lohhhh
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndio maana leo wanakula mpaka budget inayumba! Sijui na hapo bado ni Nyerere?
   
 9. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  yoote hayo na alidiriki kutengeneza gari aina ya NYUMBU....ambalo wale waliyoyanunua hadi leo yanafanya kazi!!!

  ....bado turudi upande wa pili reli ya kati ilipita pote kwenye production hadi Tanganyika peckers.....

  na pia shirika la kusimamia wanaokuja juu SIDO.......

  tuendelee kulia!
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MACHOZI YANGU......CHANGANYA NA YAKO.....!
  Si vibaya kukumbuka mema ya huyu kiumbe ambaye sasa ni mfu....amekuwa nyama ya udongo...funza wanashangilia .....mchwa wanabadilishana...LAKINI ALIYOYATENDA HAKUNA AWEZAYE KUYAONDOA FIKRANI MWETU...! WAGANDA WANAONA WAMUENZI KWA KUWA "SISI" HATUONI ALICHOFANYA
  Nitabaki shabiki mkubwa wa mwalimu,mfuasi mwadilifu wa mwalimu,mwelekezi wa dhana za kijamaa na muumini wa azimio kuu la mji wa kipekee wa arusha
  BRAVO MWALIMU.....NINAKUKUMBUKA MWALIMU....NIKIPATA WASAA....UTAKUWA ROLE MODEL WANGU katika utekelezaji
   
 11. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Akasisitiza maadili ya viongozi..viongozi walikuwa na maadili na rushwa ilikuwa ni taboo!...waulize kina Kimiti..ila baada ya yeye..watu wakasema na 'atokomee zake'...ikawa kama mapanya pale paka anapokuwa hayupo!
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mzee mwenzangu,kwa kuwa mimi ni mkulima nakumba sana yale mashamba ya Mbeya ambayo sasa tunalima jatropa,nakumbuka yale mashamba ya mkonge tanga na morogoro,pia nakumbuka yale mashamba ya mvomero ambayo sasa yamekufa kabisa,

  lakini pia nakumbuka sana kauli zake juu ya madini yetu ambayo sasa yanatutesa na kutumaliza kwa kuuwawa

  kweli yakale hayavundi,babu ni babu tu alikuwa na muono wa mbali

  hata shilingi yetu ilikuwa juu sana kipindi chake

  kwa kuwa nilikuwa mwendesha matrector nakumbuka sana lile shirika lilikuwa likileta mafuta machafu na kusafishwa hapa Tanzania lakini sasa kwishineyi

  nyerere daima kwa maslahi ya taifa
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimekumbuka na vile viwanda vya mufindi na Bukoba vilivyokuwa vikisindika chai na vingine vikisindika Pareto.Laaaa yaani vyote hivi alikuwa anawafanyia watanzania sio? Alafu wamekuja wahuni (Samahani wengine wanawaita wajanja) wameharibu kila kitu na tunawakenulia meno, tunawapigia makofi na kuwaimbia ngonjera za pongezi. Ujinga wetu unatuponza kwa kufanywa maskini wa kutupa. Tukidiriki kusema tunaitwa wapinzani tusio na sera ohhh mara sisi wa msimu! lakini si ukweli hauzikwi?. Hivi ni kwa nini hatuoni na kufahamu? tunasubiri kiongozi akitoka madarakani tumuenzi kwa lipi? Jamani nitabaki namlilia Nyerere hakika alikuwa na maono ambayo ni wachache wanayo hata leo. Nasema wachache kwa sababu hata walio katika taasisi ya kumuenzi hawana uthubutu,,,,,, hawana uthubutu wa kusema! hawana uthubutu wa kusema hapana,,,,,,,,, hawana uthubutu,,,,,,,ndio nasema hawana uthubutu!!!!!!!!

   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  hakuna maneno yanayoweza kuelezea na kutosheleza juu ya mwalimu
   
 15. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  nawaomba niondoke ukurasa huu kwa mema tu......nikiendelea kuyasoma mnayoyadadavua...sononeko langu litazidi hili nililonalo......na nitakapopelekwa hospital,wataniambia nitoe 3,000 ya kufungua faili,1,000 ya kipimo,2,500 ya kumuona daktari pasipo kusahau DUO-COTEXIN kwa bei ya sokoni ni 12,000.....JUMLA 18,500
  Gharama ambazo mwalimu alisema serikali izibebe kwa kujali afya za wananchi ambao MTIKILA ametuongezea msamiati wa "MLALAHOI"
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mahesabu si vyepesi kumuelewa mwalimu, lazima ukitaka kumuelewa utafakari kidogo, utathimini kidogo na uone nini ilikuwa malengo na nini kinaendelea leo.
  Nakumbuka mzee Mwinyi wakati akiapishwa alijifananisha na kichuguu na mwalimu akimuona kama mlima. Alidiriki kusema anapokezwa kijiti........ lakini what a betrayal? Mwalimu aliyoyaacha mbona yalianza kuaribikia mikononi mwake? nahisi speed ya kifo chake ilikuwa ni utawala ovyo ovyo usiojali maslahi ya watanzania aliouona muda mfupi tu baada ya kuwapokeza kijiti. Nakumbuka alianza ku defend uuzwaji wa mabenki na viwanda uliokuwa umechukua kasi.......... nani anakumbuka speech yake mei mosi pale Mbeya? Ama kweli nina kila sababu ya kumlilia mzee huyu,,,,,,,,,,
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  ....Bila kusahau usafiri... KAMATA, TRC.... na ukienda jijini dar kulikuwa na UDA. Mabasi yalikuwa na vituo na kila kituo kulikuwa na ratiba na mabasi yanaenda kwa muda maalumu. Yalikuwa yametengenezwa maalumu kama town bus zinavyotakiwa kuwa...
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160

  Leo baada ya kuua usafiri huo nasikia wana mkakati wa ku- establish usafiri kama huo tena Dar kwa magari makubwa! Mungu weeeee
   
 19. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kulikuwa na mabasi ya he(e)karus kumbakumba ya UDA pia..hiki kilikuwa ni kivutio kukubwa kilichonifanya niifikirie Dar kila likizo ya shule ilipokaribia
   
 20. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Acha wewe, Mkuu anasema kweli. Kama angekuwa hai na bado madarakani watu wangemuondoa kama Mubarak, simply alikuwa Dikteta, isitoshe viwanda vingi vilianza kudorora akiwa bado madarakani. Jiulize kwanini Mwinyi alitoa ruksa kuagiza bidhaa nje, hali ilishakuwa mbaya.
   
Loading...