Nimemkumbuka marehemu Prof Edward K.Shayo

kilemi

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
547
107
Huyu alikuwa mwl. wa hisabati pale UDSM aliyependa sana mizaha akiwa darasanai, mojawapo ni hii hadithi hapa:

Hapo zamani za kale akili zilikuwa zinauzwa. Basi mtu mmoja akaenda kununua akili akakuta bei zifuatazo akili no.1=US$1000, akili no.2=US$5000 na akili no.3=US$10000!!
Alipouliza kulikoni bei tofauti akajibiwa:
Akili no.1 ni ya wasomi na wanasayansi, ni akili ambayo imetumika sana hivyo uwezekano wa kuchakaa mapema ni mkubwa sana!!

Akili no.2 ni ya waandishi wa habari, haijapimwa na ikajulikana ilivyo (buy on your own risk) inaweza ikawa imetumika sana, mf. kwa sasa waandishi wa magazeti ya raia mwema, au ikawa mpya mf. waandishi wanaosubiri maagizo ya boss, leo wamchafue nani au wamsifie nani!!

Akili no.3 ni akili ya wanasiasa, hiyo ni mpya kabisa! Hutumika mara moja tu kwa muda wa miaka mitano! Mfano mwanasiasa anayeagiza barabara za flying over zijengwe mara moja, wakati ya Nelson mandela ilimshinda; au kuipa nguvu takukuru wakati boss mwenyewe Richmond ilimshinda.

Alihitimisha kwa kusema: KIDUMU CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI!!!
Mungu amkaze pema peponi!!
 
Marehemu Prof.Edward K.Shayo Huyu bwana alikuwa Profesa Makini kweli kweli ,Lakini aliponunua akili no.3 basi ndo ikawa mwisho wa uhai wake!!! Mungu ailaze mahali pema peponi.ZIDUMU FIKRA ZAKE MAKINI.Wale mlioshikwa Maths.mnamjua vema.
 
Ni kweli mkuu. Hakufurahia kuona watu wanafukuzwa chuo kwa kufeli somo lake na hivyo alijitahidi watu wasome waelewe na baadae waende zao wakafie kwenye mikono ya wababaishaji wengine.
Sisi tuliosoma mathematics for non majors, Laplace transformation, enzi hizo tunamkumbuka. Alikuwa muungwana sana.
Na hata kujiunga kwake na siasa ni kutokana na kuona mambo yalikuwa yana suasua.
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Huyu ana mchango mkubwa kwa maendeleo ya wanasayansi wa Tanzania through vitabu, kile kilichoitwa kijiji cha sayansi maana alikuwa ndio incharge kabla ya kutolewa kwasababu ya political ambitions zake na ufundishaji wake pia. Ingekuwa busara mtu kama huyu naye michango yake ikapata kupewa enzi.
 
Mkuu watu makini kama hawa ndio wanaweza kukumbukwa sana na pia itakuwa ni faida kwao kama wakianzisha award kwa wanafunzi wanasoma Hisabati UDSM kama tuzo za kumbukumbu kwake
 
He was good in math and computer!

alikuwa na upendo mno na nchi kiasi cha kuingia kwenye siasa akiamini watu watamuelewa, matokeo ya kura ya urais kama sikosei Tabora alipata kura moja! hii nchi yetu tunalaana nyingi sisi!!!
 
Marehemu Prof.Edward K.Shayo Huyu bwana alikuwa Profesa Makini kweli kweli ,Lakini aliponunua akili no.3 basi ndo ikawa mwisho wa uhai wake!!! Mungu ailaze mahali pema peponi.ZIDUMU FIKRA ZAKE MAKINI.Wale mlioshikwa Maths.mnamjua vema.

Kiongozi,

Kwa kumbukumbu yangu, Huyo Prof. hakuwai kumkamata mwanafunzi katika somo lake - Vector Analysis [I - III] - Aliyekuwa anafeli sana ni KARAI!

BTW: Kijiji cha science alichoanzisha kimefia wapi

RIP - Shayo EK
 
He was good in math and computer!

alikuwa na upendo mno na nchi kiasi cha kuingia kwenye siasa akiamini watu watamuelewa, matokeo ya kura ya urais kama sikosei Tabora alipata kura moja! hii nchi yetu tunalaana nyingi sisi!!!

CCM walipomfrustrate na kijiji cha wanasayansi pale Arusha ndio akaamua kuingia siasa akitarajia kuwa angeweza kufanikisha malengo yake ya kuisaidia nchi hii!! He was better by far kuliko hawa watawala tulionao lakini historia ya chama tawala inaonyesha kwamba hawataki watu wenye akili kama Shayo, Kolimba, Mangula, warioba etc; Kama hawatawamaliza basi watawatenga kichama ili wapotee pole pole!!
 
Huyu alifanya kampeni safi kabisa zisizo na doa. Akaonekana kituko na kichekesho kila alikopita.
 
Kiongozi,

Kwa kumbukumbu yangu, Huyo Prof. hakuwai kumkamata mwanafunzi katika somo lake - Vector Analysis [I - III] - Aliyekuwa anafeli sana ni KARAI!

BTW: Kijiji cha science alichoanzisha kimefia wapi

RIP - Shayo EK

Kweli kabisa, kwenye functional analysis mwenzake mshimba alikamata 75% ya darasa, lakini yeye akapitisha wote!
 
Huyu alifanya kampeni safi kabisa zisizo na doa. Akaonekana kituko na kichekesho kila alikopita.

Wakati akiuza kadi za Demokrasia Makini alisema "Msiombe uanachama mkitegemea kupata pesa, ila mtapata matatizo ya kusumbuliwa na watawala wadhalimu na wala rushwa ambayo matunda yake ni ushindi na faraja kwenu"
 
Kuhusu maswali mengi sana darasani:
Mwan: Samahani prof. hapo sijakuelewa kidogo!
Prof. Shayo: Hivi wewe huwa unasoma magazeti? Sasa usipoelewa huwa unampigia simu mhariri kuuliza, au unajadiliana na aiye jirani yako?
 
RIP Prof.Shayo,nakumbuka kampeni yake aliyokuwa akifanya katika Corolla yake... Wengi walimbeza,na kumdhihaki.
 
only in math. not in computer... just put record right!
hapana alikua mmoja ya wasomi w mwanzo mwanza hapa Tz kubobea pia katika Technolojia ya Computer, ila uprofesa wake ulitokana na mafanikio yake ktk mathematics, alikufa akipigania Technolojia, aliamini ktk dunia ya leo hakuna maendeleo kama nnchi itaendelea kulala katika Technologia, Amka Tanzania.
RIP SHAYO.
 
Akili no.2 ni ya waandishi wa habari, haijapimwa na ikajulikana ilivyo (buy on your own risk) inaweza ikawa imetumika sana, mf. kwa sasa waandishi wa magazeti ya raia mwema, au ikawa mpya mf. waandishi wanaosubiri maagizo ya boss, leo wamchafue nani au wamsifie nani!!
hapo sijaelewa, nimekua napasoma mara mbili mbili bila kuelewa, aliepaelewa abandike ufafanuzi.....na atakua amenisaidia.
 
Huyu alikuwa mwl. wa hisabati pale UDSM aliyependa sana mizaha akiwa darasanai, mojawapo ni hii hadithi hapa:

Hapo zamani za kale akili zilikuwa zinauzwa. Basi mtu mmoja akaenda kununua akili akakuta bei zifuatazo akili no.1=US$1000, akili no.2=US$5000 na akili no.3=US$10000!!
Alipouliza kulikoni bei tofauti akajibiwa:
Akili no.1 ni ya wasomi na wanasayansi, ni akili ambayo imetumika sana hivyo uwezekano wa kuchakaa mapema ni mkubwa sana!!

Akili no.2 ni ya waandishi wa habari, haijapimwa na ikajulikana ilivyo (buy on your own risk) inaweza ikawa imetumika sana, mf. kwa sasa waandishi wa magazeti ya raia mwema, au ikawa mpya mf. waandishi wanaosubiri maagizo ya boss, leo wamchafue nani au wamsifie nani!!

Akili no.3 ni akili ya wanasiasa, hiyo ni mpya kabisa! Hutumika mara moja tu kwa muda wa miaka mitano! Mfano mwanasiasa anayeagiza barabara za flying over zijengwe mara moja, wakati ya Nelson mandela ilimshinda; au kuipa nguvu takukuru wakati boss mwenyewe Richmond ilimshinda.

Alihitimisha kwa kusema: KIDUMU CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI!!!
Mungu amkaze pema peponi!!
Aliitwa Prof Leonard .K. Shayo.

Hakika alikuwa mahiri wa kujenga hoja na uchambuzii makinii..Nilikuwa namfuatilia sana kupitia makala zake katika gazetil la mwananchi jpili.

RIP Prof .
 
hapo sijaelewa, nimekua napasoma mara mbili mbili bila kuelewa, aliepaelewa abandike ufafanuzi.....na atakua amenisaidia.

Akili namba 1, imetunika sana! hivyo unaweza kununua akili ya mwandishi wa habari iliyotumika sana kwa 5000 ikala kwako, au ukanunua ambayo haijatumika kwa 5000 badala ya no.3, ukawa umefaidi sana!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom