Nimemaliza taratibu zote September project hii

Ndugu zangu pole Na majukum pili pole kwa kuchelewa kwa ndege Yetu kule Canada, pili tusubiri makinikia,

Ila kama nilivyowaambia ninafungua project hii ni maalumu kwa mama ntilie Na watu wa magenge,
Sababu za kuwahusisha hawa ni kwamba wao wanapata hela kila siku Na pili ni watu wanaoitaji mtaji kuendeleza biashara zao,

Nimefurahi sana kuona proposal yangu imepokelewa vema,

Kwakuwa ni mwanzo ngoja nijilipue tu,

Mk

Nitadili Na kuwakopesha akina mama wa mahoteli madogo madogo, Na vijana wa uza genge,

Nimepata watu walio tiyari kupokea mkopo huu , idadi ni 37 nimeshawapata,

Mikopo Na aina ya urejeshaji

Mkopo wangu utakuwa Na riba ya 50% kwa mwezi Na viwango ni kama ifuatavyo

1. 50,000 anarejesha daily sh 2500 ndani ya mwezi mmoja

2. 100,000 anarejesha daily sh 5000 ndani ya mwsezi mmoja

3. 150,000 anarejesha 7500 daily ndani ya mwezi mmoja

4. 200,000 anarejesha 10,000 daily ndani ya mwezi mmoja


Nimefuata utaratibu wote wa usajili, Na nimepata kibali simple tu. Kodi muhim kulipa, sasa nipigane kufungua office niajiri kijana mmoja atakaye kuwa anazunguka kukusanya mrejesho hayo daily nadhan kamshahara ka 350,000 kanamtosha sana,


Zingatia siji kiholela kupigwa hela yangu, niko very strict. Lazima udhaminiwe, Na uweke kitu chenye thataman rehani,

Kwanini nimechagua aina ya urejeshaji uo?


1. Ni friendly haimuumizi mrejeshaji

2.dawa ya Deni ni kulipa taratibu kidogo kidogo sitaki madeni ya mkupuo yatakayoleta shida,

3. Mtu itamufanya awe Na uchungu wa kulipa yote maana makubaliano ni kwamba ukifeli kwa siku ndo mazima Mali yako imeenda hiyo,

4. Nimechagua hao KINA mama maana wanapata hela sana Na hawadhurumu,


Mungu hawabariki,

Jaman uwekezaji muhim


Mkuu na mimi hua naifanya hii biashara naomba muongozo wa kupata vibali vyote vinavyostahiki
 
Back
Top Bottom