Nimemaliza shule muda mrefu, nahitaji kuchukua cheti changu je, Hatua zipi nifuate?

Kabagala

Member
Sep 2, 2014
10
15
Habari JF members. Naomba ushauri!

Naitwa Otto Kabagala .

Nimemaliza kidato cha nne tangu 2009 na sijachukua cheti changu maana niliyakasirikia matokeo yangu (Nilipata grade 4 ya 30)

Sasa naona umuhimu wa kuwa na cheti changu, je, Naweza kufanyaje ili nipate cheti changu?

Naombeni msaada wenu wanajamii forums, na Mungu awabarikini!
 
Kaka yangu alimaliza o level 2004. Cheti cha o level tulikifata shuleni kwake mwaka huu 2020.. na amepewa bila shida.. alibeba living certificate siku tuliyokifata shule kuepusha kubambikiwa madeni ya ada
 
sasa kwa matokeo hayo, hicho cheti utakipeleka wap au lengo ukitunze tu?
 
Kuna watu wanaajiriwa serikalini taasisi kubwa kwa kazi kama telephone operator, security guard bandarini, ma dereva BOT, TRA etc kwa cheti kama hicho na wanalipwa mishahara mikubwa.. kuliko watu wenye degree wanaoajiriwa wizarani ama tamisemi
ok mkuu..sikuwa nalijua hilo?
 
Na mimi toka nihitimu o level 2015 sikukitafuta tena sasa inabidi nikakichukue huenda kikanisaidia mbeleni.
 
hahahahahaa.................nilifikiri labda hicho cheti kimepotea!!! kumbe umauliza ukakifuate wapi?!!!! hakika sishangai hiyo four uliyopata!
 
Back
Top Bottom