Nimemaliza kuongea na Rafiki yangu anayeishi Marekani, Ananiambia 'we are still working from home beacuse of Corona, America is becoming boring place'

Wewee jamaa wewee hata historia huijui. Kasome habari za wafalme huko tena wale waliobarikiwa zaidi uone kama hawakutesa na kuua maelfu kwa maelfu na bado Mungu aliendelea kuwabariki.
Kulikuwa na sababu za kufanya hivyo kipindi hicho,zama hizi hakuna aliyetumwa na Mungu kuua na kutesa viumbe wake!
 
Dah Tigershark umepanic tu!!
Huwezi kucheza kamari kwenye ugonjwa aisee, ni lazima uufahamu ndio uchukue hatua sahihi.
Approach iliyotumika ilitokana na kufahamu sayansi ya “immunology”. Unaweza kuanzisha jambo lakini akatokea mwingine ambaye akalifahamu na kuliboresha zaidi, hivyo usishangae.
Wazungu walitiwa hofu na “wana mipango” wakaingia mkenge wakapuuzia ukweli wa kisayansi na matokeo yake kilichowapata unakijua.
Corona ingekuwa kama Ebola bado nasi tungetumia sayansi hiyohiyo kukabiliana nayo. Ndiyo maana ya kupewa akili na utashi
Hatukuwa tunaufahamu ugonjwa wa Corona kwani ulikuwa mgeni na ndio maana kadri muda ulivyosogea ndivyo wataalamu wakazidi kutoa taarifa zaidi kwa kile wanachokigundua juu ya kuenea kwa ugonjwa huo!
Kuna nchi kama brazili wala hawakuwa na hofu na rais wao alifanya kama sisi,matokeo yake imewateketeza sana!
Kuna nchi za Africa ambazo hazikupata kisa hata kimoja!Kiufupi Africa haijaathiriwa sana na Corona,na hii inaweza kuwa sababu ya kijiografia au watu wa maeneo hayo wana immune kubwa by nature!
Burundi wakati sisi tumefunga shule na kusimamisha michezo wao walikuwa wanaendesha kampeni za uchaguzi na hawakuchukua hatua za kujikinga maana misongamano ilikuwa mikubwa!Wao nao wamevuka hili la Corona salama!
Tusidanganyane hapa eti tumetumia mbinu za kisayansi badala yake ukweli ni kwamba tulikuwa tayari kwa matokeo yoyote na tukaamua liwalo na liwe!
 
Don't use a noun and a pronoun together. Magufuli(noun)+ he(pronoun) is incorrect, rather Magufuli is...., or He is.....!

Ni maono tu ya mheshimiwa, ilà naamini matumizi ya limao, tangawizi nk vilitusaidia sana.
 
Kulikuwa na sababu za kufanya hivyo kipindi hicho,zama hizi hakuna aliyetumwa na Mungu kuua na kutesa viumbe wake!

Kama waamini hivyo sawa, ila sidhani kama Mungu wa kipindi chao ni wa tofauti na Huyu wa kipindi chetu.
 
..Ni bahati ya mtende.

..kwasababu kama ni kumuomba MUNGU, wazungu ndio waliotuletea habari za MUNGU tuliyemuomba.

..sasa imekuaje wao waliotu-introduce kwa MUNGU waathirike kuliko sisi?
Kwa asili mwanadamu ameumbwa na utambuzi wa asili wa uwepo wa Mungu, namna za kumuabudu na kumtafuta ndizo zilitofautiana.. So, kusema wametutambulisha kwa Mungu ni makosa na kuamini uongo wa hao wajinga..
 
Wewe ndio mpumbav,tupe sababu ya kwanini Corona haijaathiri sana nchi za EAC na majirani wa nchi hizo!
Stupid you!Je,approach tuliyoifanya ilikuwa na sababu za kisayansi nyuma yake au ni tulicheza kamari?Kichwa panzi kabisa!
Vipi kama Corona ingekuwa inapiga kama Ebola,tungekuwa wapi leo?
Kwa wenye imani na Mungu wataelewa na kumtukuza kwa jambo hilo.. Wapo wachache walioomba kwa dhati kbsa na Mungu aliwasikia, hata Rais hajawahi kujinasibu na sababu za kisayansi, zaidi amekuwa akimtukuza Mungu kwa hilo na kwa imani yake.. So, kama unaona ni kamari, well and good
 
Siku izi hakuna chama tawala wala upinzani, wote wanaamini TZ hakuna corona, na kama ipo basi sio ya kutisha kama ilivyo kwa wenzetu.

Mimi nahisi ni mazingira ya bara letu Afrika, maisha ya shida shida na vyakula tunavyokula ivi mara chipsi imepikwa kwenye mafuta ya transformer basi huenda miili yetu imekomaa kwa maradhi kama haya ya mafua na kikohozi mpaka yamekuwa kama kawaida.

Jambo jengine ni vile kutokuwa na khofu, asikwambie mtu, khofu mbaya. Wakati serikali ikiwa inatangaza wagonjwa, khofu ilikuwa kubwa. Yaani ukimuona mtu anakohoa tu, unawaza kwenda mbio na kumtenga. ukihisi kooni kuna kitu tu unaona corona hio hata kama ni ganda la njugu tu limekuganda.
 
Mimi naamini na kumwamini Mungu. Lakini napata ukakasi wa kusema Mungu ndiye aliyetusaidia kwa sababu mataifa karibu yote ya Afrika hayakuathirika sana na korona. Ndiyo maana nimesema jaribu kushughulisha akili zako kidogo uone eg Kenya, Uganda etc vifo ni vichache ku-compare na Ulaya na Amerika. Hata China ukichukuwa population na kulinganisha na vifo bado idadi iko chini. Hivyo unaponiambia Mungu alitusadia sisi mimi nitakubishia kwa sababu kuna nchi nyingine ambazo ziko sawa na sisi au hata vizuri kuliko sisi. Kitu ambacho hujui ni kuwa Tanzania ule mwezi wa 4 na 5 kulitokea vifo vingi tu lakini vilifichwa. Sasa sisi tuliopoteza watu wengi kuliko Uganda na Kenya tikisema Mungu alitusaidia hawa majirani zetu watasemaje? Mungu husadia tu watu wanatimiza wajibu wao. Huwezi kupuuza hatari halafu ukasema eti Mungu atakusadia. BTW mbona hajatusaidia kwenye magonjwa mengine kama malaria ambayo yanaua hata watoto wadogo?
Yaani idadi ya vifo ilifichwa lakini bado unaijua ni kubwa kuliko ya wengine, how!? Na unajiona umeelezaa. Kwa wenye akili umewaonyesha upumbavu wako.. Ujanja na ujuaji juaji mwingi, mbele giza..
 
Yaani idadi ya vifo ilifichwa lakini bado unaijua ni kubwa kuliko ya wengine, how!? Na unajiona umeelezaa. Kwa wenye akili umewaonyesha upumbavu wako.. Ujanja na ujuaji juaji mwingi, mbele giza..
Unafikiri ni watu wote walikuwa wajinga kama huyo aliyewaamuru wafiche? Ujinga kama huu lazima wapo wenye busara wanajitolea kuonyesha ukweli. Na ndiyo maana anatetemeka sana kuondolewa uchaguzi huu kwa sababu anajua madudu aliyofanya siri yatalipuka. Huyu siku ya kuondoka ndiyo ataishia pabaya sana kwani maadui aliotengeneza ni wengi mno japo wanamchekea kwa kijino cha pembe.
 
Wewe utakuwa kilaza mkuu duniani
Watu wanashangaza mno. Nadhani kwa sababu sisi watanzania wengi hawana utamaduni wa kutafiti mambo. Unajua watu hajui kuwa nchi nyingi za Afrika kwa sababu ambazo bado hatuzijui hazikuathirika sana na huu ugonjwa. Hali ya Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia nk kwa kuathirika ni sawasawa kabisa. Tofauti ni kwamba rais wa Tanzania amekataza watu wasipimwe na wale wanaofariki wasitangazwe. Tena kwa idadi ya vifo vilivyotokea Tanzania tunaongoza kulinganisha na nchi nyingine za East Africa ila tofauti ni kuwa Magufuli alipuuzia tangu mwanzo hivyo watu wengi wakafariki kwa mpigo kile kipindi cha mwanzoni na baadae herd Immunity ikafanya kazi.
 
Tuache siasa tuache majungu Magufuli ni mwanasayansi asiekuwa muoga na anaejua nini anafanya. Sio kwamba ana miujiza ila alichoweza kuwaaminisha watanzania ni kwamba corona ni mafua ya kawaida sana kawaida ila haiwezi kushindana na uwezo wetu wa kukabiliana na hali tete au hali ngumu.

Alichofanya Magufuli ni kawaondolea watu hofu na kuiona corona kama mafua ya kawaida that how he won against corona. Hili si swala la kiasiasa ni swala kutambua mambo pia tumshukuru Mungu pia kuwa katupa kiongozi anaweza kuona na kutambua hatari na madhara yake leo tungekuwa na lockdown maisha ya watanzania yangekuaje?

Magufuli he is the hero against corona in the world. Kampeni zinaendelea, wapinzani pamoja na chama tawala wote wanajaza watu kwa maelf kiukweli wakati wa corona tungekuwa na Rais toka CHADEMA mnajua maamuzi yangekuwaje.
Kwhyo ukiongea na mtu wa marekani tayar uzi!!!dah!hizi smart phone hizii....
 
Kwa wenye imani na Mungu wataelewa na kumtukuza kwa jambo hilo.. Wapo wachache walioomba kwa dhati kbsa na Mungu aliwasikia, hata Rais hajawahi kujinasibu na sababu za kisayansi, zaidi amekuwa akimtukuza Mungu kwa hilo na kwa imani yake.. So, kama unaona ni kamari, well and good
Inamaana sisi ndio tunamjua sana Mungu kuliko hao wanaoangamia?Kwanini tujisifu kwa hilo?
 
Kama waamini hivyo sawa, ila sidhani kama Mungu wa kipindi chao ni wa tofauti na Huyu wa kipindi chetu.
Mungu wa kipindi hicho angekuwa ameshashusha gharika kwani yanayotokea leo ni zaidi ya sodoma na gomola!
Yes,Mungu amekuwa na huruma sana na binadamu zama hizi!
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom