Nimemaliza dozi ya Malaria leo, nikinywa pombe jioni au kesho je?

Intelsat

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
323
532
Wakuu nimemaliza leo dozi ya Malaria Mseto. Sasa hapa moja haikai wala mbili najuta sana kutumia hii dozi msimu wa sikukuu.

Nimemalizia vidonge vinne leo asubuhi sasa wakuu vipi nikizama maeneo leo usiku au kesho nikagonga gonga hivi viserengeti lite au Castle lite kuna shida?

Hali ya kiafya sio mbaya kabisa meaning naendelea na pilika za kuandaa sikukuu.

Nishaurini wakuu.
 
Wakuu nimemaliza leo dozi ya malaria mseto ALu sasa hapa moja haikai wala mbili najuta sana kutumia hii dozi msimu wa sikukuu. Nimemalizia vidonge vinne leo asubuhi sasa wakuu vipi nikizama maeneo leo usiku au Kesho nikagonga gonga hivi vi serengeti lite au Castle lite kuna shida??? hali ya kiafya sio mbaya kabisa meaning naendelea na pilika za kuandaa sikukuu nishaurini wakuu
Mkuu unataka Parapanda ilie nini? Angalia usije kwenda kumlaki bwana yesu mawinguni.
 
Hahaaaa!! Kipindi kile napiga ugimbi mpaka basi kama namaliza dozi namcheki daktari wangu kwa maoni. Nina rafiki daktari ila sikuwa nathubutu, anarahisisha sana mambo.

Kwa case yako subiri mpaka kesho mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mwaka nilikuwa nasumbuliwa na uvimbe was jino,Basi jioni nikapiga fragily(metronidazole).
Kesho yake nikapiga kilaji,,,,nusra niage dunia,unatapika Hadi nguvu za kutembea zinaisha
 
Kuna mwaka nilikuwa nasumbuliwa na uvimbe was jino,Basi jioni nikapiga fragily(metronidazole).
Kesho yake nikapiga kilaji,,,,nusra niage dunia,unatapika Hadi nguvu za kutembea zinaisha
Fragile niliambiwa ni mbaya sana hio mkuu siwezi ata kuitumia mana kuna point naweza kujisahau nikakata maji halafu afu nikakata na moto pia hio dawa apana
 
Wakuu nimemaliza leo dozi ya Malaria Mseto. Sasa hapa moja haikai wala mbili najuta sana kutumia hii dozi msimu wa sikukuu.

Nimemalizia vidonge vinne leo asubuhi sasa wakuu vipi nikizama maeneo leo usiku au kesho nikagonga gonga hivi viserengeti lite au Castle lite kuna shida?

Hali ya kiafya sio mbaya kabisa meaning naendelea na pilika za kuandaa sikukuu.

Nishaurini wakuu.
Acha uroho wa bia wewe hizo dawa zinakaasiku 7 mwilini.japo haina madhara ukinywa pombe ila ujue ndo umeuwa nguvu yote ya dawa.
Mi nakushauri kama una hamu ya pombe kunywa baltika ni kama bia ila haina kilevi itakusaidia
 
Nilimaliza dozi ya metakelfini halafu nikapiga pombe sana, walivunja mlango siku ya pili yake niko hoi chini sakafuni na nikaponea almanusura.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom