Nimemaliza dozi ya malaria juzi jumanne,Leo naweza kunywa pombe?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,809
15,059
Habari watu wa Mungu?
Eti leo naweza kunywa bia walau chupa tano hivi,maana nilikua na malaria na nimemaliza dozi toka jumanne ya wiki hii, na kiukweli najiskia nimepona kabisa,so leo kuna sherehe mahali na kama ntaenda kwenye hiyo sherehe siwezi kujizuia kunywa bia kabisa.
Kwa wadhoefu wa hii Mambo,kuna madhara yoyote yanaweza kunipata?
 
Ningekushauri kama unajipenda, husiguse pombe kabisaaaaa.
Lakini hilo likishindikana, basi nakushauri uandae jinsi mazishi yako yatakavyo kuwa husije wasumbua watu watakao baki.
Andaa sanda kabisaaaaa
 
Acha wehu.
Mithali 23:29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?

30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;

32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.

33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.

34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.

35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
 
Habari watu wa Mungu?
Eti leo naweza kunywa bia walau chupa tano hivi,maana nilikua na malaria na nimemaliza dozi toka jumanne ya wiki hii, na kiukweli najiskia nimepona kabisa,so leo kuna sherehe mahali na kama ntaenda kwenye hiyo sherehe siwezi kujizuia kunywa bia kabisa.
Kwa wadhoefu wa hii Mambo,kuna madhara yoyote yanaweza kunipata?
yah..unaweza mzee kunywa K-vant kubwa ,nimemiss ku type RIP
 
Kunywa lakini usizidishe mana hizi pombe za kitonga/ganda la ndizi azijawai kumuacha mtu salama
 
Ningekushauri kama unajipenda, husiguse pombe kabisaaaaa.
Lakini hio likishindikana, basi nakushauri uandae jinsi mazishi yako yatakavyo kuwa husijewasumbua watu watakao baki.
Andaa sana kabisaaaaa
Na aseme anataka afukiwe na udongo aoze haraka? au ajengewe "marumaru" ndani akose mchwa wa kumtafuna mapema.
 
IMG_4396.JPG
 
Ningekushauri kama unajipenda, husiguse pombe kabisaaaaa.
Lakini hio likishindikana, basi nakushauri uandae jinsi mazishi yako yatakavyo kuwa husijewasumbua watu watakao baki.
Andaa sana kabisaaaaa
Acha kututisha,usitutisheee nakwambia.Mkuu kula Pombe wala hakuna hofu yoyote.
 
Yani leo ni siku ya nne toka umemeza dawa na bado unaogopa kutwanga mnvinyo? Nakumbuka Kuna siku nilikuwa nimemeza dawa za vidonda vya tumbo kesho yake nikaenda kijijini kusalimia wazazi kufika kule nikapata hamu yakupiga tungi ikabidi nimpigie dokta nimuombe ushauri bahati mbaya hakupokea cm yangu, kesho yake akanipigia nikamuuliza kama naweza kuanza kutumia pombe akanijibu ata siku ile unameza zile dawa ungemezea mzinga wa konyagi usingepata madhara sema dawa zisingefanya kazi mwilini. Nilijiona lofa mpaka leo.
 
Back
Top Bottom