Nimelitathimini jengo la Makao Makuu ya CHADEMA pale Ufipa na nimeridhika chama hicho hakijali Maendeleo ya Vitu

Miaka yote hiyo kumbe mnatokea hapa, nimesikia mnazindua CHADEMA Digital Marekani na bado makao makuu ni hapa.
KAMA HAMJAWEZA KUJENGA OFISI MTAWEZA KUJENGA NCHI?
View attachment 1884546
Ni kweli cdm kukosa ofisi yenye hadhi yao kwa muda wote huu ni fedheha kwao. Lakini ccm hawana uwezo wa kuwacheka maana 80%+ ya majengo yake ni ya kurithi kwa shuruti toka mfumo wa chama kimoja. Na ukitaka kujua ni ya kurithi na kama sio umiliki wao wa dola wasingekuwa na chochote, zunguka nchi nzima, majengo ya ccm ndio machakavu na ya kizamani zaidi, mengi yana hali mbaya hata kupiga rangi yamewashinda. Nitajie uwanja wa mpira ccm waliojenga baada ya mfumo wa vyama vingi, kaangalie uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hapo Tabora nk, ndio utajua nasema nini.
 
CDM kulipana posho ndio wanajua. Ofisi yao hawawezi kuijenga wakipewa nchi si watauza kila kitu.
CDM ovyo kabisa.

..watoto wa juzi hamjui kwamba kuna majengo ya ccm yalijengwa wakati wa mfumo wa chama kimoja kwa kutumia michango ya wananchi, fedha za serikali, na hata kuweka tozo maalum ktk bidhaa.

..pia yapo majengo ya ccm yamejengwa kwa kutumia misaada toka nchi za nje.
 
Sijui Chadema wanakapendea nini hako kajengo miaka yote.

Jiulize pia kwa nini CCM wanapenda CHADEMA itumie sehemu kubwa ya rasilimali zake kujenga jengo kubwa lenye “hadhi” la makao makuu.
 
Miaka yote hiyo kumbe mnatokea hapa, nimesikia mnazindua CHADEMA Digital Marekani na bado makao makuu ni hapa.
KAMA HAMJAWEZA KUJENGA OFISI MTAWEZA KUJENGA NCHI?
View attachment 1884546
Watu wana vichwa vikubwa ila hawana akili humo ndani, sjaona faida ya majengo hayo makubwa, so what is the impact for these big for nothing buildings, humo humo ndimo mnakaa kulihujumu taifa, wezi wote mnawafugia humo humo. Huna akili wewe
 
Miaka yote hiyo kumbe mnatokea hapa, nimesikia mnazindua CHADEMA Digital Marekani na bado makao makuu ni hapa.
KAMA HAMJAWEZA KUJENGA OFISI MTAWEZA KUJENGA NCHI?
View attachment 1884546
Acha ujinga basi,nchi haijengwi kwa pesa za viingilio kwenye chama,nchi inajengwa kwa Kodi,unajuaje kwamba Chadema haiwezi kujenga nchi,kwani imeishawahi kutawala nchi hii?hii nchi haijengwi kwa michsngo ya ccm na watu wake,nchi inajengwa na Kodi zinazokusnywa na majizi ya ccm
 
Miaka yote hiyo kumbe mnatokea hapa, nimesikia mnazindua CHADEMA Digital Marekani na bado makao makuu ni hapa.
KAMA HAMJAWEZA KUJENGA OFISI MTAWEZA KUJENGA NCHI?
View attachment 1884546
Pamoja na yote lakini kufananisha mali ambazo kwa 85% zilitaifishwa kutoka kwa mali za umma/ wananchi na kuzimilikisha kwenye chama halafu unalinganisha na chama ambacho kinapambana kwanza na chama tawala ,pili serikali, tatu vyombo ya ulinzi na usalama,nne tume ya uchaguzi na tano msajili wa vyama vya siasa halafu ndani ya makucha hayo yote bado chama kinaitesa serikali tangu mwaka 1992 hadi 2021 August 7 kwakweli hujatenda haki kabisa katika mlinganisho wako huo.
 
Na sababu ya hao wengine kushindwa hata kumiliki ofisi nzuri ni ulemavu wa akili.
Chama cha mapinduzi kina mali nyingi za unyang'anyi kutoka kwa wananchi zilizo patikana kabla ya vyama vingi yakiwemo majengo, kumbi, maeneo ya wazi, na viwanja pamoja na magari kwa wakati huo, hivyo ni ujinga kufananisha na chama ambacho kimeanza na moja kujipanga kikiwa hakina kitu chochote .
 
Wakati mwingine ccm mnakosa akili!!Nenda pale Moro mtaa wa mazimbu halafu niambie ANC ilikuwa na majengo ya ofisi mangapi hata kule kwao S.Africa hadi wakafanikiwa kuchukua nchi kutoka kwa makaburu!!!!
 
Sababu ya hao wengine kua na jengo kubwa la ghorofa, ni kutapeli wananchi. Kudhulumu rasilimali za taifa, na unyonyaji uliopitiliza!
Tatizo hawa vijana waliozaliwa juzi, wengi hawafahamu kuwa majengo ya CCM na mali zao za sasa, tulilazimishwa kuchangia watz wote, kipindi hicho wakati wa Chama kimoja kupitia kila unaponunua bidhaa adimu kwenye maduka na ndio majengo na viwanja vya michezo mnavyoona nb leo...'to bei fair' mali zingerudi serikalini na kila chama kianze 'on fair ground ' mara baada ya kuanzishwa vyama vingi.........
 
06 August 2021

MAONO YA CCM VS CHADEMA

MADA : SIASA, UHURU NA MAENDELEO



Source: STAR TV HABARI
 
Kama CHADEMA wameweza kuwatoa kamasi kiasi hiki CCM wakiwa kwenye kijumba hicho, sijui itakuwaje wakianza kuwapiga makombora wakiwa kwenye mjumba mkubwa, hivi umeliwaza hilo?

Nafuu ya CCM ni kuendelea kuwakandamiza CHADEMA waendelee kuwa kwenye vijumba vyenye hadhi kama hiyo. Wakikusikia, au kama kuna aliyekutuma kuweka ujumbe huu hapa, siku zenu huko ndani ya CCM zitaishia hapo.
 
Hivi makao makuu ya CUF bado ni haya hata baada ya hayati Maalim kjiondoa CUF?
1628389126700.png
 
Back
Top Bottom