Nimelipitia faili la Pandora sijawaona Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete wala Magufuli. Hata Mbowe hayumo Tanzania ni safi!

Hata kama ufisadi upo lakini haujafikia viwango vya kutisha kama tulivyoona kwenye lile faili la Pandora.

Heshima ya Tanzania kimataifa ni ya kujivunia.

Mungu ni mwema wakati wote!
Ndiyo maana tunawaambia wale anti Dkt JK na anti Dkt Magufuli, hawa viongozi si mafisadi ila mchwa ni hawa wateulr wao na tena wanakosa uzalendo tu. Hii nchi naamini kila mmoja akiwa muadilifu, mchapa kazi nchi itapiga hatua
 
Mpe heshima basi mama yako wa nyumbani utajua umuhimu wa heshima kwa kila mama. Namheshimu sana mama yako kama ninavyo mheshimu mama yangu. Nadhani umenielewa.
Nchi hii tukisema tuwapange wezi, majambazi na mafisadi, watu wa jinsia zote 6 utawakuta.
 
Tanzania inahitaji tuzo ya "Guiness World Record" kwenye sekta ya Wizi na Ufisadi.

Pia, inatakiwa kutunukiwa "Hati Ya Kutambua Mchango WaKe Endelevu Wa Kuzalisha, Kukuza, Kuchochea Na Kuhamasisha" vipaji vya Wizi na Mafisadi katika nchi za Kusini mwa Jangwa La Sahara na Afrika Ya Kati (SADC Countries & Cental African Countries).

Huko Magharibi Mwa Africa tunawaachia wenyewe waamue, kuna nchi mbili zinachuana vikali kwenye medani hii ya Wizi na Ufisadi. Kuna nchi inaitwa Ghana na Nigeria.
 
Tanzania hakuna wizi ni udokozi tu huu....nafikiri pia ni kwasababu ya thamani ndogo ya currency yetu.....Kenya ni balaa
currency si kigezo kwenye nchi yenye rasilimali kama yetu ama ni wabobezi katika kuficha ama ni wadokozi wa wadogo ama wanaficha hapahapa kwa namna wanayojua wao
 
Back
Top Bottom