Nimelipia nguzo TANESCO muda mrefu mpaka leo hawajarudi kunipa huduma

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
3,296
2,000
kuna binadam mnakera, hebu jiongeze bas

had namtafta mkandarasi it means nilishajipanga kwa njia hiyo ili mambo yangu yaende kwa haraka na siku alokuja mkandaras akaniletea na mpimaji hiyo n mwez wa saba nikakaa mwez wa tisa akaja mpimaji mwengine baada ya hapo kimyaaa na nilishaongea na mkandaras akanijibu sina haja ya yote hayo
.... sina haja ya yote hayo. Ana haja na hela yako
 

naiman64

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
6,463
2,000
Habari za muda huu,

Jamani ninaomba kuuliza, tulifanya process za kuomba umeme tangu mwezi wa saba mwaka huu, na tuliwatumia wakandarasi wa hapo hapo tanesco kutujazia na kutuchorea na kurudisha form tanesco Tanga Mjini.

Sasa siku hiyo hiyo alikuja mtu wa kufanya survey na akapima pima pale na kikubwa kilichotakiwa ni nguzo, tukakaa tukisubiri kuitwa kwenda kulipia nguzo iwekwe umeme uingie, tulisubiri mno kwenye mwez wa tisa nikapigiwa sim kama nilishapimiwa nikajieleza tayar wakanambia niende eneo husika niwaelekeze wao wanakuja, nikafika tukaelekezana wakaja wakapima tena baada ya hapo hicho kimya chake skukielewa ikabidi mimi nifunge safar mpaka hapo ofisini kwao.

Nikaomba kuonana na mtu wa kulitatua tatizo langu nikaonana na mama mmoja hivi hata usoni hakuangalii na jibu akataka tu namba na jina la form nikampa akanijibu ukiona tanesco wamekita nguzo kwenye hilo eneo ndio uje.

Nimesubiri kwa muda mrefu mnooo naomba kufahamishwa tatizo ni nini najua wahusika wapo humu nikimpigia yule mkandarasi majibu ni kama hayo sasa sielewi tangu mwezi wa saba had sasa naona zii.
Hao jamaa hiyo ndio kula yao Sasa usiponyoosha mkono utabaki kuangilia hiyo risiti na mwisho italiwa na panya hawaji hao, fungua pochi nyoosha mkono
 

ngome1838

JF-Expert Member
Feb 20, 2019
1,285
2,000
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Inasaidia nini kwani, endeleeni kupiga ila tunaamini atakuja Magufuli mwingine siku moja na mtanyooka tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom