Nimelipia nguzo TANESCO muda mrefu mpaka leo hawajarudi kunipa huduma

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
16,048
2,000
Habari za muda huu,

Jamani ninaomba kuuliza, tulifanya process za kuomba umeme tangu mwezi wa saba mwaka huu, na tuliwatumia wakandarasi wa hapo hapo tanesco kutujazia na kutuchorea na kurudisha form tanesco Tanga Mjini.

Sasa siku hiyo hiyo alikuja mtu wa kufanya survey na akapima pima pale na kikubwa kilichotakiwa ni nguzo, tukakaa tukisubiri kuitwa kwenda kulipia nguzo iwekwe umeme uingie, tulisubiri mno kwenye mwez wa tisa nikapigiwa sim kama nilishapimiwa nikajieleza tayar wakanambia niende eneo husika niwaelekeze wao wanakuja, nikafika tukaelekezana wakaja wakapima tena baada ya hapo hicho kimya chake skukielewa ikabidi mimi nifunge safar mpaka hapo ofisini kwao.

Nikaomba kuonana na mtu wa kulitatua tatizo langu nikaonana na mama mmoja hivi hata usoni hakuangalii na jibu akataka tu namba na jina la form nikampa akanijibu ukiona tanesco wamekita nguzo kwenye hilo eneo ndio uje.

Nimesubiri kwa muda mrefu mnooo naomba kufahamishwa tatizo ni nini najua wahusika wapo humu nikimpigia yule mkandarasi majibu ni kama hayo sasa sielewi tangu mwezi wa saba had sasa naona zii.
 

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
36,450
2,000
Mkandarasi akishakuchorea, unatakiwa kupambana mwenyewe. Eneo linakuaje surveyed mara mbili? Ni wakati gani ulipewa control number ya kulipia July ama September.
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
16,048
2,000
Mkandarasi akishakuchorea, unatakiwa kupambana mwenyewe. Eneo linakuaje surveyed mara mbili? Ni wakati gani ulipewa control number ya kulipia July ama September.
Huwezi amini hiyo control namba yenyewe siijui ina tarakimu ngapi nilishakwenda hapo ofisini kwao wakaniambia nikiona nguzo imewekwa niende sasa naona siku zinakimbia tu
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
16,048
2,000
jibu ulishapewa hapa
nguzo zinasimikwa ki awamu, awamu A,B,C
interval ya awamu wanajua wenyewe
hawaweki nguzo kwa mtu mmoja mmoja, ( labda utoe hongo ndefu )
shida naona muda ni mrefu imagine tangu mwez wa saba had sasa wa kumi na moja kwa kweli ustahmilivu wa kusubiri unanishinda ndio mana nauliza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom