Nimelipa faini kwa kosa la kukwepa shimo barabarani

Ushirombo

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
3,558
2,697
Jamani jana nimelipa faini elfu 30 huko Kibada kwa kosa la kukwepa shimo barabarani, jamani hivi hata kukusanya mapato isiwe kwa kuoneana hivyo,eti kosa obstruction other road users,na nyinyi kwanini barabara inakuwa na mashimo? Naichukia sana hii,na jana kidogo tupigane na trafiki bahati nzuri wale matrafiki wengine wakanisihi eti huyo jamaa ni kawaida yake kuonea watu.

Nampelekea laana na umasikini trafiki huyo.
 
Umeileta siku ya wajinga sasa sijui nikujibuje. Kwa nini hukuchukua details za hilo eneo korofi na usilipe faini ili mkutane mahakamani?
 
Hawa Traffic wa TZ somtimes wanakariri mambo sana..Siku moja nilikuwa kwenye eneo ambalo huruhusiwi ku-overtake mbele yangu kuna hizi Toyo za tairi 3 imejaza mizigo mingi inatembea kama kinyonga na nimeifikia nimepunguza speed hadi 20 lakini wapi na kuna umbali hadi ufike mahali panaporuhusu kuovertake...Nikampigia honi jamaa wa TOYO akabana pembeni nikampita nikiwa kwenye line yangu ile ile mbele traffic wakanipiga mkono ...kwa nini nimeovertake..Nikawaambia sikutoka kwenye lane yangu ni sawa tu na kumpita mtu wa baiskeli sehemu isiyo ruhusiwa overtake je ni kosa? Hataukuelewana kabisa nkawatema..
 
Jamani jana nimelipa faini elfu 30 huko Kibada kwa kosa la kukwepa shimo barabarani, jamani hivi hata kukusanya mapato isiwe kwa kuoneana hivyo,eti kosa obstruction other road users,na nyinyi kwanini barabara inakuwa na mashimo? Naichukia sana hii,na jana kidogo tupigane na trafiki bahati nzuri wale matrafiki wengine wakanisihi eti huyo jamaa ni kawaida yake kuonea watu.

Nampelekea laana na umasikini trafiki huyo.
Huu ni ujinga,
Siku moja niko Kiluvya mbele yangu kulikua na Lorry halikua na mwendo kabisa. Nikalipigia honi ili liwashe "double hazard" na kweli dereva alinielewa hivyo akawasha "double hazard". Hiyo ilikua ni tiketi kwangu kua ingawa line ya kutenganisha barabara ilikua ya moja kwa moja (huruhusiwi ku-overtake) lakini kwa "double hazard" ile ya Lori niliruhusiwa ku -overtake, ile narudi tu upande wangu Traffic hawa hapa wakanipiga mkono. Kucheki speed sijazidi 50.

Wakadai nime overtake pasiporuhusiwa, nikawauliza nini maana ya lile Lori kuwasha ile "double hazard", mmoja akajibu kua Dereva wa Lori sio traffic hivyo hana mamlaka ya kuniruhusu ku overtake pasiporuhusiwa. Nilimjibu tu sawa nikaingia ndani ya gari na kuondoka zangu.
 
ajali ile ya.mbeya iloua basi zima ni.kosa la.dereva.kukwepea shimo ndani, yawezekana ulikwepea ndani.ambapo.ni kosa
 
hii mada inahitaji msaada wa kisheria nadhan pia inahitaji uhalisia wa eneo hilo la tukio huku ukilinganisha mawazo ya pande zote mbili yaani upande wa trafic na dereva..hapa kuna maelezo ya upande mmoja ninapata shaka kutumia msemo wa kila mwamba ngoma..............anyway ninapata shaka kulaumu na kuhukumu kwa expert judgement...hukumu ya upande mmoja.....its ok
 
kwel mkuu inaumiza sana
 
Hawa askari wakati mwingine sijui ni kutaka attention au inferiority!! Kuna haka kadada katraffick kamening'ang'ania saa 11 alfajiri utafikiri hakana kazi nyingine. Kweli insurance yangu ilikuwa imeisha siku chache zilizopita na nilikuwa nimepanga kwenda kulipa the next day lakini dada kakomaa anataka kuchomoa funguo za gari maana leseni nilimuambia simpi hata atoe ushuzi gani

Nilivyoona hakuna dalili za kuelewana nikamwambia ngoja nipaki gari vizuri nimpe funguo, nikaipa moto moja kwa moja. Siku nyingine tumekutana bar nikamkazia macho nikaona hana amani ikabidi tusalimiane tu. Kama ni mapato wakawakabe wenye migodi kwa spidi hii hii sio sisi makapuku
 
ajali ile ya.mbeya iloua basi zima ni.kosa la.dereva.kukwepea shimo ndani, yawezekana ulikwepea ndani.ambapo.ni kosa

Ufafanuzi zaidi tafadhali (kukwepea ndani na nje) what if shimo limeanzia nje limeingia half the lane unayoitumia mwendeshaji
 
Kuna siku Trafki kanisimamisha nikapaki pembeni nimsikilize anasemaje akaanza kuniomba leseni, mara bima iko wapi ??? mara saiti mira ziko wapi ?? mara indiketa ziko wapi nikabaki namshangaa huyu askari vipi chizi nini toka lini Baiskeli ikahitaji hivo vitu ????
 
Jamani jana nimelipa faini elfu 30 huko Kibada kwa kosa la kukwepa shimo barabarani, jamani hivi hata kukusanya mapato isiwe kwa kuoneana hivyo,eti kosa obstruction other road users,na nyinyi kwanini barabara inakuwa na mashimo? Naichukia sana hii,na jana kidogo tupigane na trafiki bahati nzuri wale matrafiki wengine wakanisihi eti huyo jamaa ni kawaida yake kuonea watu.

Nampelekea laana na umasikini trafiki huyo.

Pole sana ila vumilia tunatafuta za kufidia gap la mcc
 
Back
Top Bottom