Nilufer
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 9,316
- 12,826
heshima yenu wana MMU
hapa nilipo kichwa kimenivurugika naomba ushauri wenu na faraja pia.
ni hivi ninaishi nyumba moja na jamaa na mke wake (ni wakurya). ni mwaka na miezi kama kumi hivi mke hayupo yupo jijini Nairobi kimasomo. sasa tangu mke ameondoka jirani yangu kaleta msichana mwingine anaishi naye kama mke na mume. miezi sita iliyopita mke alinipigia simu na kuniuliza kama mumewe anaishi na mtu kwani amebadilika sana na mawasiliano yanasuasua, mimi nikamjibu kwamba mimi niko bize sana si rahisi kujua anavyoishi. wiki moja baadaye akanipigia tena kunisihi nimwambie ukweli kwani amepata taarifa kwamba mumewe anamsaliti. mimi nikamwambia niko safarini hivyo sijui kinachoendelea.
kwenye mwezi wa kumi hivi alinipigia tena simu kuniuliza hayohayo mi nikamwambia kama anahisi chochote aje mwenyewe ajiridhishe na nikakata simu. leo asubuhi kanipigia na kunisimulia namna anavyopata shida huko chuoni kwani mumewe amekuwa mgumu kutoa huduma, kiasi kwamba anashindwa hata kurudi likizo kwani hana hata nauli na taarifa alizonazo ni kwamba mumewe anaishi na mtu ila mtu aliyemwambia hamuamini sana kwani ni mwanaume ambaye huwa anamtaka. basi nikaingiwa huruma kubwa nikajikuta namwambia ukweli kwamba kuna mtu anaishi naye. ila nikamuonya asinitaje coz sitaki matatizo.
kumbe baada ya kuongea na mimi tu akampigia mumewe na kumwambia kwamba anavunja ndoa.
sasa huyu jirani anahisi mimi ndiye niyemwambia na amenipigia simu (akiwa anatetemeka kwa hasira) kuniuliza kama nimeongea na mke wake. mi nimeruka kimanga, amedai anakuja tuongee vizuri jioni.
mimi nimeamua sitaki kukaa hicho kikao. na nimepanga kuzua safari coz naogopa kupigwa panga.
wenzangu mnanishauri nini?
KUMBUKA: TUKIO LIMESHATENDEKA LAWAMA HAZITANISAIDIA KWA SASA.
cc Sista Kaizer Heaven on Earth mwekundu Munkari charminglady gfsonwin 'Valentina' Mapi Mkoroshokigoli farkhina na wadau wengine

Last edited by a moderator: