Nimelikoroga: Nilidraw pattern mpya ya simu jana usiku leo nimeisahau,nifanyeje wakuu?

Daah hapo uwe unakumbuka email na password ya google .. bonyeza volume up and power off kuna step kadhaa
 
ashomile Email na password vyote navikumbuka ila wadau wa mara ya kwanza walisema nihold volume up + power on buttons,lakini wewe unanambia kuwa nihold volume up + power off buttons,now which is which?
 
Ok simu yako ni hizi android version ambazo zinazuia wizi kwa FRP (Factory Reset Protection) hivyo hakikisha unaijua na unaikumbuka email na paswed uliyoweka kwenye simu.

Zima simu.

Bonyeza power button na volume up button kwa pamoja.

Itakuletea recovery interface.

Nenda kwenye wipe data/ factory reset.

Kisha shuka mpaka kwenye yes.

Kubali.

Ikimaliza kuwipe utakubali Reboot.

NB. Tumia volume down kushusha, volume up kupandisha wakati wa selection. Power button ni kwa ajili ya kuchagua.
Mkuu mfano umesahau password inakuaje hapo?
 
Download software inaitwa Miracle Star 2.7 ni vyema ukaipata ya Telecom isiyo na paswed.

Pia download na drivers kwa ajili ya simu za Media Tek. Zisearch google kwa jina hili mt65xxx usb drivers.

Badilisha tarehe ya pc yako na mwaka uwe 2014.

Ziinstall hizo softwares zote mbili.

Nenda kwenye miracle loader ifungue.

Itakuletea interface ina ribbon nyingi upande wa juu kulia. Ibonyeze ribbon ioiyoandikwa 'Unlock/ fix'

Ukishaibonyeza utaona neno 'Clear setting/ frp' libonyeze hilo neno.

Kisha bonyeza start button.

Itakuuliza kama unataka kuback up. Kataa.

Itakutaka uichomeke simu na usb.
Chomeka (simu iwe imezimwa) itajiprocess yenyewe na mwisho itakwambia done.

Utakua umeshamaliza tatizo.

NB. Disable antivirus au iseti isiichukulie miracle kama kirusi.

Mkuu mfano umesahau password inakuaje hapo?
 
Hapo ninachojua ni kwamba unahold volume buttons zote mbili na power button kwa wakati mmoja mpaka utapata hizo options
Utaitumia volume up kwenda juu na volume down kwenda chini na power utaitumia kama OK kwenye selection
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom