Nimelelewa na babu yangu aliekuwa mfanyakazi wa wakoloni

karue

Senior Member
Oct 31, 2018
191
347
Tujikumbushe kidogo tuliolelewa na baba au babu walioishi zama za wakoloni

Binafsi nimezaliwa mkoa wa Mara wilaya ya bunda .

Maisha yangu yote nimekaa na babu na Bibi uko kijijini.
Babu yangu kwa Sasa ni marehemu toka 2001

Babu alikua mfanyakazi wa wakoloni enzi hizo kutokana na historia yake.
Babu yangu maisha ya nyumbali alikua anayaendesha kikoloni koloni .

Haya ni machache nayo yakumbuka
1: hutakiwa kufika nyumbani kabla ya saa 12 jioni
2: hakuna kuongea kipindi unakula
3: mwanamke anaepika chakula hatakiwi kuongea muda wote wa mapishi
4: ni marufuku kuvaa nguo bila kuchomekea hata Kama uko shambani
5: mkiwa shambani anarusha jiwe linapofikia ndiyo mwisho wako wa kulima
6: babu alikuwa na sero ukifanya kosa unatupwa sero siku nzima pamoja na vibiko juu
7: babu alikuwa na ng'ombe wanaporudi kutoka machungoni vijana wote tunakaa karibu na zizi kuhesabu ng'ombe hiyo ni kila siku
8: usipoenda kanisani hakuna kula
9: babu ndiye alikuwa anawatafutia vijana wake mke wa kuoa,endapo ukienda kumwambia nataka kuoa yeye anafunga safari kwenda kumfanyia tathmini huyo mke wako asipomkubali kwa tabia na kazi anakutafutia yeye

10: Ni marufuku mwanamke/ wanawake kula meza moja na mwanaume/ wanaume

11: Mbwa wake wasipokula wanawake wanapeana adhabu ya kubweka usiku kucha kwa kupangiwa masaa,nakumbuka tulikuwa na mbwa 12

Yapo mengi Ila kwa machache ndiyo hayo.
Namshukru babu yangu kutokana na Sheria zake zote lakini alituweka katika msingi mkubwa Sana wa kupambana na kusimamia familia vyema

Je, wewe unakumbuka Nini vijana wenzangu wa zamani
 
Mbona hizo tabia zote ni za kawaida hapa kwetu Uhayani, mtoto hulelewa na ni dhamu ya hali ya juu na utii, sema tu siku hiza uswahili wameshavamia mila zetu na tamaduni watoto wanalelewa kiuswahili swahili.
 
Mbona hizo tabia zote ni za kawaida hapa kwetu Uhayani, mtoto hulelewa na ni dhamu ya hali ya juu na utii, sema tu siku hiza uswahili wameshavamia mila zetu na tamaduni watoto wanalelewa kiuswahili swahili.
Ni kweli kwa baadhi ya makabila Ila babu alikua anaogopeka Kijiji kizima kwa misimamo
 
Yote sina shida nayo ila hlo la kupeana zamu ya Kubweka hapo feminist wangeruka nae kizazi cha sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom