Nimelazimika kusubiri mazishi ndio tujaribu kuangalia ukweli wa kifo chake

Salimu Panzi

Member
Nov 27, 2015
7
45
MAMBOSASA AMEIBUA MASWALI MAGUMU 12 KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Inasadikika kuwa Leopold Lwajabe, aliyekuwa Mkurugenzi wa miradi ya Umoja wa Ulaya nchini (EU) katika Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye alikutwa ananing'inia mwisho wa wiki, kabla ya kifo chake alilazimishwa kuandika wosia, wahusika wakauchomeka ofisini kwake kwa siri ili kuficha mazingira ya kifo chake.

Lakini pia nimemsikia Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, akithibitisha hilo la kuhusu WOSIA. Mtu yeyote anayejua saikolojia, anaelewa kwanini Mambosasa amejitokeza kuzungumzia wosia

INASIKITISHA: YA NDANI KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Dotto James, Katibu Mkuu Hazina (mpwa wa Rais Magufuli) ambaye ni bosi wa Leopold Lwajabe anatuhumiwa kuwa na mkono katika sakata la kifo cha LWAJABE.

Juzi kabla mwili haujapatikana Dotto alikuwa na vikao vya siri na polisi wasio na unifomu kujadili statement waliyopika kuhusu marehemu. Yeye alijulishwa kifo Jumamosi usiku, na Jumapili alishinda na hao polisi.

Lwajabe alikuwa akilalamika juu ya watu wanaomfuata kutaka hela za kitengo cha EU hapo wizarani. Alipokataa walimtisha kuwa wanamjua kila kitu na kuwa yeye ni raia wa Rwanda.
Katika kipindi hiki cha kuhangaishwa kwake, familia yake huko Karagwe ilihojiwa na maafisa usalama kuhusu uraia wake mara kadhaa.

Alipotekwa mara ya kwanza wiki moja iliyopita, alisainishwa makaratasi ya ofisi na kisha akalazimishwa kuwapa password ya ATM card na fedha zake zikachukuliwa zote.

Alirudushwa na gari la Noah na kutupwa jirani na kwake Kinyerezi. Waliomrudisha hawakutaka kujulikana. Gari jingine liliendelea kuzunguka eneo hilo kwa siku mbili kuchunguza kina nani wanafika na kutoka.

Yeye alikuwa kama amechanganyikiwa na akawa anatoa hadithi zinazojichanganya. Mwenyewe alitishwa kuwa akisema yaliyomtokea watarudi kummaliza. Wamemmaliza kimya kimya! Alipotekwa mara ya pili, wiki hii iliyoisha juzi, polisi waliendelea kuwatuliza ndugu zake kuwa ataonekana ndani ya saa 72, wakawaonya wasisemeseme sana.

Chanzo kutoka ofisi ya ZCO kinadai watekaji wake si polisi ila ni watu wenye nguvu waliokuwa wanawaagiza polisi mambo ya kufanya. Lwajabe alifanyiwa unyama mkubwa. Alilawitiwa na kupigwa picha. Alilazimishwa kuandika barua kuwa amejiua kwa sababu ya matatizo yake binafsi na kwamba asilaumiwe yeyote. Alilazimishwa kuandika wosia na ukapelekwa na kuingizwa ofisini kwake. Wauaji walimfunga kamba na kumtupa kichakani Mkuranga.

Kisha waliwaelekeza polisi waende kuchukua mwili na kuuweka hospitali. Polisi hawakwenda na camera kuchukua picha za eneo wala kuchukua alama za vidole mwilini. Mmoja wa wapelelezi ni ndugu wa marehemu, na alipogundulika polisi walisitisha jitihada zote za kupika ripoti. Ukweli ulio wazi ni kwamba kuna kundi maalumu la siri serikalini lipo juu ya kila taasisi, na linachotaka ni fedha. Ni ujambazi wa kidola. Inasikitisha sana!

MASWALI YANAYOIBULIWA NA MAMBOSASA

Kauli ya Mambosasa kuwa Lwajabe alijiua na aliandika wosia huo uliokutwa ofisini mwake, imeibua maswali kadhaa.

Hapa naweka maswali 11 ya msingi ya haraka haraka ambayo Mambosasa angepaswa kuyajibu:

1. Mtu ambaye ameshaamua kujiua kwa kujinyonga mtini, hadi anaandika wosia na kuuacha ofisini, kwa nini atoke Dar es Salaam asafiri na kupita miti yote hadi Mkuranga, huku nyumbani kwake Kinyerezi kumejaa miti ya miembe ambayo ingemfaa kwa jambo hilo?

2. Lwajabe aliondoka nyumbani kwake akiwa amevaa shati. Amekutwa mortuary Mkuranga akiwa na tisheti. Kama Mambosasa ni mkweli, kwa nini hadi sasa dereva wake, karani wake na ndugu zake hawajahojiwa juu ya mabadiliko haya ya mavazi?

3. Kwa nini polisi waliamua kumuondoa eneo la "kujinyongea" na kumpeleka mortuary bila kuita ndugu zake, wakati walikuwa na RB namba za kupotea kwake? Walikuwa na haraka ya nini?

4. Kwa nini polisi hawakutumia forensic equipments ili kurahisisha uchunguzi?

5. Kwa nini polisi hawakutaka ndugu wa marehemu kushiriki katika post-mortem na kwanini hawakuwapa taarifa za awali za uchunguzi?

6. Kwa nini serikali ilijua wosia wa marehemu kabla ya kifo kutangazwa. Kwa nini polisi walikuwa wanamtafuta marehemu mezani kuliko vichakani?

7. Kabla ya kifo chake, kwa nini maofisa usalama mkoani Kagera walisumbua familia yake na kuchukua maelezo yao baada ya Lwajabe kutekwa mara ya kwanza? Kwa nini mdogo wa marehemu aitwaye Meneja Byase alihojiwa na TISS kipindi marehemu ametekwa mara ya kwanza? Walihoji kuhusu nini, na mbona Mambosasa hasemi haya?

8. Kwa nini Katibu Mkuu Hazina, Dotto James, alikuwa anamlazimisha Lwajabe aende likizo ya wiki mbili baada ya kuwa ametekwa mara ya kwanza?

9. Kwa nini polisi walikazana kutaka ndugu wa marehemu wasisemeseme na kwamba ndugu yao angeonekana ndani ya saa 72 baada ya kutekwa? Walijuaje? Lengo lao lilikuwa nini?

10. Kwa nini Katibu Mkuu Dotto alizuia kifo cha Lwajabe kutangazwa Jumamosi jioni wakati mwili ulishaonekana?

11. Lwajabe aliporudishwa mara ya kwanza baada ya kutekwa, gari la Noah jeusi lilikuwa linazunguka mtaani kwake. Watu walilitilia shaka, wakachukua namba zake na kuwajulisha polisi. Mbona hadi sasa polisi hawajatoa taarifa juu ya hatua walizochukua dhidi ya gari hilo wala hawajasema ni la nani?

Bora Mambosasa angekaa kimya. Kama anatumwa aseme, awaeleze wanaomtuma kuwa wanaoelezwa kumsikiliza wana akili timamu, na wanachukizwa kusema mengine ambayo wasingeyasema iwapo asingesema.

Ndiyo, walimtisha Lwajabe asiseme wazi alichotendwa, lakini hakuna siri ya watu wawili.

Sawa, wafanye mizaha hii, lakini watambue kuwa damu ya Lwajabe ina thamani kama ilivyo damu ya Mambosasa. Tuheshimu utu wa wenzetu! Utu wetu ni bora kuliko vyeo na madaraka ya wanaomtuma kudhihaki uhai wa Lwajabe!
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,048
2,000
Hivi ndugu wa Lwajabe watakua wanawaza nini juu ya hawa waliomtendea unyama huu ndugu yao. Idadi ya watu wenye ndugu waliotendewa unyama kama huu ikifika kubwa sijui nini kitatokea. Ndugu wa watu wa aina hii kama akina Azorry na Ben saa nane watakua na hasira sana mungu atuepushe tunakopelekwa
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,575
2,000

luvcyna

JF-Expert Member
Feb 24, 2009
1,854
2,000
Machozi ya kifo hiki yakafutwe katika uchaguzi huu, shime ndugu zangu Watanzania, ukawe mwisho wa mauaji haya
 
luvcyna

JF-Expert Member
Feb 24, 2009
1,854
2,000
Daah Wauwaji wa Lwajabe ndio unawakuta wametamalaki katika Kampeni za wakati huu.
 
luvcyna

JF-Expert Member
Feb 24, 2009
1,854
2,000
Bila kusahau Kifo cha mama yake na Mwandishi aluyebambikiwa Kesi na mpaka kufikia kumuomba Raisi amuachie mwanaye huru.

Ni ajabu waandishi bado hawaoni kuwa hawako Huru
 
Macbook pro

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
281
500

Hata wakiona hayo, shida ni kwamba wanaogopa kufa. Mie naomba siku moja katiba mpya ipitishwe. Haya yanatokea kwa sababu baadhi ya mihimili ya serikali haina nguvu, mhimili mmoja tu ndio wenye mamlaka.
 
luvcyna

JF-Expert Member
Feb 24, 2009
1,854
2,000
Hata wakiona hayo, shida ni kwamba wanaogopa kufa. Mie naomba siku moja katiba mpya ipitishwe. Haya yanatokea kwa sababu baadhi ya mihimili ya serikali haina nguvu, mhimili mmoja tu ndio wenye mamlaka.

Umenena vyema, ila usingizi walionao wangeamka wote kwa pamoja nyakati hizi wangeupata ukombozi wao wenyewe.

Hiki ndio kipindi waandishi wana umuhimu kuliko kipindi chochote kile lakini wameshindwa kukitumia.

Yaliyomkuta Kabendera yalipaswa kutolewa majibu kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote
 
Macbook pro

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
281
500
Umenena vyema, ila usingizi walionao wangeamka wote kwa pamoja nyakati hizi wangeupata ukombozi wao wenyewe.

Hiki ndio kipindi waandishi wana umuhimu kuliko kipindi chochote kile lakini wameshindwa kukitumia.

Yaliyomkuta Kabendera yalipaswa kutolewa majibu kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote

Mkuu nyakati zimebadilika, hofu ya kupotezwa imejaa na ipo kila mahali na jamii ya Watz haina ile roho ya kutetea wananchi wenzao wakiwa kwenye nyakati Ngumu kama hizo za kuwekwa vizuizini au wakati mwingine kuwekwa rumande.
 
Yuzo mawe

JF-Expert Member
May 31, 2019
484
1,000
MAMBOSASA AMEIBUA MASWALI MAGUMU 12 KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Inasadikika kuwa Leopold Lwajabe, aliyekuwa Mkurugenzi wa miradi ya Umoja wa Ulaya nchini (EU) katika Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye alikutwa ananing'inia mwisho wa wiki, kabla ya kifo chake alilazimishwa kuandika wosia, wahusika wakauchomeka ofisini kwake kwa siri ili kuficha mazingira ya kifo chake.

Lakini pia nimemsikia Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, akithibitisha hilo la kuhusu WOSIA. Mtu yeyote anayejua saikolojia, anaelewa kwanini Mambosasa amejitokeza kuzungumzia wosia

INASIKITISHA: YA NDANI KUHUSU KIFO CHA LWAJABE

Dotto James, Katibu Mkuu Hazina (mpwa wa Rais Magufuli) ambaye ni bosi wa Leopold Lwajabe anatuhumiwa kuwa na mkono katika sakata la kifo cha LWAJABE.

Juzi kabla mwili haujapatikana Dotto alikuwa na vikao vya siri na polisi wasio na unifomu kujadili statement waliyopika kuhusu marehemu. Yeye alijulishwa kifo Jumamosi usiku, na Jumapili alishinda na hao polisi.

Lwajabe alikuwa akilalamika juu ya watu wanaomfuata kutaka hela za kitengo cha EU hapo wizarani. Alipokataa walimtisha kuwa wanamjua kila kitu na kuwa yeye ni raia wa Rwanda.
Katika kipindi hiki cha kuhangaishwa kwake, familia yake huko Karagwe ilihojiwa na maafisa usalama kuhusu uraia wake mara kadhaa.

Alipotekwa mara ya kwanza wiki moja iliyopita, alisainishwa makaratasi ya ofisi na kisha akalazimishwa kuwapa password ya ATM card na fedha zake zikachukuliwa zote.

Alirudushwa na gari la Noah na kutupwa jirani na kwake Kinyerezi. Waliomrudisha hawakutaka kujulikana. Gari jingine liliendelea kuzunguka eneo hilo kwa siku mbili kuchunguza kina nani wanafika na kutoka.

Yeye alikuwa kama amechanganyikiwa na akawa anatoa hadithi zinazojichanganya. Mwenyewe alitishwa kuwa akisema yaliyomtokea watarudi kummaliza. Wamemmaliza kimya kimya! Alipotekwa mara ya pili, wiki hii iliyoisha juzi, polisi waliendelea kuwatuliza ndugu zake kuwa ataonekana ndani ya saa 72, wakawaonya wasisemeseme sana.

Chanzo kutoka ofisi ya ZCO kinadai watekaji wake si polisi ila ni watu wenye nguvu waliokuwa wanawaagiza polisi mambo ya kufanya. Lwajabe alifanyiwa unyama mkubwa. Alilawitiwa na kupigwa picha. Alilazimishwa kuandika barua kuwa amejiua kwa sababu ya matatizo yake binafsi na kwamba asilaumiwe yeyote. Alilazimishwa kuandika wosia na ukapelekwa na kuingizwa ofisini kwake. Wauaji walimfunga kamba na kumtupa kichakani Mkuranga.

Kisha waliwaelekeza polisi waende kuchukua mwili na kuuweka hospitali. Polisi hawakwenda na camera kuchukua picha za eneo wala kuchukua alama za vidole mwilini. Mmoja wa wapelelezi ni ndugu wa marehemu, na alipogundulika polisi walisitisha jitihada zote za kupika ripoti. Ukweli ulio wazi ni kwamba kuna kundi maalumu la siri serikalini lipo juu ya kila taasisi, na linachotaka ni fedha. Ni ujambazi wa kidola. Inasikitisha sana!

MASWALI YANAYOIBULIWA NA MAMBOSASA

Kauli ya Mambosasa kuwa Lwajabe alijiua na aliandika wosia huo uliokutwa ofisini mwake, imeibua maswali kadhaa.

Hapa naweka maswali 11 ya msingi ya haraka haraka ambayo Mambosasa angepaswa kuyajibu:

1. Mtu ambaye ameshaamua kujiua kwa kujinyonga mtini, hadi anaandika wosia na kuuacha ofisini, kwa nini atoke Dar es Salaam asafiri na kupita miti yote hadi Mkuranga, huku nyumbani kwake Kinyerezi kumejaa miti ya miembe ambayo ingemfaa kwa jambo hilo?

2. Lwajabe aliondoka nyumbani kwake akiwa amevaa shati. Amekutwa mortuary Mkuranga akiwa na tisheti. Kama Mambosasa ni mkweli, kwa nini hadi sasa dereva wake, karani wake na ndugu zake hawajahojiwa juu ya mabadiliko haya ya mavazi?

3. Kwa nini polisi waliamua kumuondoa eneo la "kujinyongea" na kumpeleka mortuary bila kuita ndugu zake, wakati walikuwa na RB namba za kupotea kwake? Walikuwa na haraka ya nini?

4. Kwa nini polisi hawakutumia forensic equipments ili kurahisisha uchunguzi?

5. Kwa nini polisi hawakutaka ndugu wa marehemu kushiriki katika post-mortem na kwanini hawakuwapa taarifa za awali za uchunguzi?

6. Kwa nini serikali ilijua wosia wa marehemu kabla ya kifo kutangazwa. Kwa nini polisi walikuwa wanamtafuta marehemu mezani kuliko vichakani?

7. Kabla ya kifo chake, kwa nini maofisa usalama mkoani Kagera walisumbua familia yake na kuchukua maelezo yao baada ya Lwajabe kutekwa mara ya kwanza? Kwa nini mdogo wa marehemu aitwaye Meneja Byase alihojiwa na TISS kipindi marehemu ametekwa mara ya kwanza? Walihoji kuhusu nini, na mbona Mambosasa hasemi haya?

8. Kwa nini Katibu Mkuu Hazina, Dotto James, alikuwa anamlazimisha Lwajabe aende likizo ya wiki mbili baada ya kuwa ametekwa mara ya kwanza?

9. Kwa nini polisi walikazana kutaka ndugu wa marehemu wasisemeseme na kwamba ndugu yao angeonekana ndani ya saa 72 baada ya kutekwa? Walijuaje? Lengo lao lilikuwa nini?

10. Kwa nini Katibu Mkuu Dotto alizuia kifo cha Lwajabe kutangazwa Jumamosi jioni wakati mwili ulishaonekana?

11. Lwajabe aliporudishwa mara ya kwanza baada ya kutekwa, gari la Noah jeusi lilikuwa linazunguka mtaani kwake. Watu walilitilia shaka, wakachukua namba zake na kuwajulisha polisi. Mbona hadi sasa polisi hawajatoa taarifa juu ya hatua walizochukua dhidi ya gari hilo wala hawajasema ni la nani?

Bora Mambosasa angekaa kimya. Kama anatumwa aseme, awaeleze wanaomtuma kuwa wanaoelezwa kumsikiliza wana akili timamu, na wanachukizwa kusema mengine ambayo wasingeyasema iwapo asingesema.

Ndiyo, walimtisha Lwajabe asiseme wazi alichotendwa, lakini hakuna siri ya watu wawili.

Sawa, wafanye mizaha hii, lakini watambue kuwa damu ya Lwajabe ina thamani kama ilivyo damu ya Mambosasa. Tuheshimu utu wa wenzetu! Utu wetu ni bora kuliko vyeo na madaraka ya wanaomtuma kudhihaki uhai wa Lwajabe!
Hivii kwa nini watu ni wanyama kiasi hichi?

They do not fear even a karma!!,

"A one who kills to machete,will die to machete in a return"

Mungu ailaze roho ya marehemu inapostahili.
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,340

Kuna Familia inamtumikia shetani!Inapenda roho za watu sana.Sasa mda umefika kwao na roho zao.
Mungu hadhihakiwi
 
change formula

Senior Member
Sep 8, 2020
124
250
MUNGU tunakuomba utuondolee mateso haya!! Mbona mambo haya ni mageni kwetu?!! Kwanini umeruhusu Kiongozi uyu atese na kuua watu wako?! Tunakuomba kwa uwezo wako Maanani MUNGU muumba mbingu na ardhi na kila kitu kilichomo, ujidhihirishe, mateso, manyanyaso, mauaji yamezidi sana Nchini kwetu, tuende wapi?!! Kwanini umeruhusu Kiongozi mnyonya damu!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom