Nimekwenda kupumzika makaburini ili kumuenzi nyerere. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimekwenda kupumzika makaburini ili kumuenzi nyerere.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zezeta, Oct 14, 2012.

 1. z

  zezeta Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati tukiazimisha miaka 13 ya KIFO CHA mwalimu mimi niliamua kumuenzi kwa kwa kwenda kupumzika MAKABURINI.
  Najua wengi watanishangaa na kujiuliza maswali mengi, na wengine wanaweza niona kama nimechanganyikiwa zaidi ya yote nafahamu kuna mtu anaweza dhani nime acha kumuamini BWANA na kuambatana na imani za KICHAWI.
  LA HASHA hayo yote si sawa niliamua tu KWENDA KUPUMZIKA.
  Nilianza safari yangu KUELEKEA MAKABUNI huku nikiwa sijiamini amini, lakini kwa kua nimeamua ilinibidi nifanye ivyo, niliingia makaburini bila woga. UPEPO mwanana na sauti za ndege vili burudisha masikio na akili yangu barabara. Nilitafuta eneo la kukaa lilonifanya nione vizuri nyumba za milele walimo lala wapendwa wetu.

  Mwanzoni nilikua na woga lakini baada ya muda mchache nilipata ujasiri na kuya acha macho yangu kuangalia pande zote za bustani. Akili yangu ilijiuliza maswali mengi na kutoa majibu kadhaa huku moyo wangu uki dunda taratibu kuisukuma damu iliyokua ikisisimka mara kwa mara..
  Mara maswali yakanijia kichwani mwangu, nikajiuliza " IVI NI WANGAPI KATI YA WOTE HAWA WALIO LALA WAMEWEZA KUTIMIZA NDOTO ZAO KABLA HAWAJARUDI MAVUMBINI ?" Na JE! ni kweli wamelala wakiwa wametoa vyote ambavyo MUNGU aliwapa kuja kuvitoa DUNIANI? . HIVI NI KWELI NAFSI ZAO ZIMEZAMA MAVUMBINI ZIKIWA NA FURAHA ZIKISEMA IMANI TUMEILINDA NA KAZI TUMEMALIZA? NA WANGELI ONGEZEWA SEKUNDE MOJA WASINGELIKUA NA LAKUONGEZA KABISA?
  Sikuweza kupata majibu Ila GHAFLA woga ukaniingia nikaanza kutetemeka. NILIPOJIWEKA SAWA NIKAGUNDUA KUA, MIMI NATAMANI KUISHI MAISHA YA NDOTO ZANGU, KUTOA VYOTE NILIVYONAVYO ILI NITAKAPO RUDI UDONGONI NIRUDI NIKIWA MTUPU, SWALI JE NITAFANIKIWA?
  Niliamua kuondoka lakini nafsi yangu ikiwa na deni kubwa la kutimiza ndoto zangu kabla sijafa na nilipofika nyumbani ndipo nilipojiuliza vizuri ivi ni kweli NILIAMUA KWENDA KUPUMZIKA MAKABURINI?


  (N.B USIJARIBU KUIGA... ILA AMUA KUTAFUTA KUSUDI LA MAISHA YAKO)
   
 2. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  binafc huwa nahudhuria makaburi mara kwa mara,ni sehemu 2livu ambayo mtu aweza tafakar kuhusu maisha yake na hata kubadil mwenendo kama c mzuri, huwa cogopi kwani mama yangu kipenzi amelala huko so nikienda hayo maeneo najihisi kuwa naye karibu !!
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Alifanya vizuri sana kuwanyan'ganya wamissionary shule na waislamu na wakristu kusoma pamoja. Hilo limeleta amani sana . Halafu lingine, pale alipomkatalia kisakolojia kwame Nkurumah na mwenzake Nasser, kutaka kuunganisha africa . Leo hii Boko Haram wangesambaa africa nzima na maisha ya watu yangeharibika sana pamoja na mali.
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Napita tu
   
 5. hasason

  hasason JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 1,558
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  ungeniomba ushauri ningekushauri pia upende kuwatembelea wagonjwa ambao kwa namna nyingine unaweza kuwasaidia wapate ahueni ili watimize ndoto zao wale walio karibu na mauti utakuwa umefanya kitu ambacho ni sawa na kumfufua mfu na kumpa second chance lakini kwa wafu usiwatembelee sana kwasababu wamekwisha lala Yesu aliwaambia wacha wafu wazike wafu wao kwasababu walikuwa wakijisumbua na maswala sana ya msiba badala ya kusikiliza gospel ya Yesu Kristo ili wapone roho zao watakapo kufa(lala) waridhi ufalme wa mbinguni sio hapo tu hata ndugu zake Yesu na mama yake walipokuwa wakimtafuta wakifikiri amepotea aliwajibu yampasa kukaa nyumbani kwa Baba yake akiwapa makuhani na wazee wa sunagogi habari njema wakati akiwa mtoto wa miaka 14 na kuna mahali pengine walimtafuta akawaji ndugu zangu dada kaka mama yangu ni hawa wanaosikiliza injili na kuiishi hawa ndio ndugu zangu lakini pia kuna sehemu alifika nyumbani kwa martha lakini maria alikuwa bize sana kumuandalia chakula lakini martha alikuwa ameketi miguuni pa Yesu akisikiliza habari njema mpaka maria akamshataki kwa Yesu kwa anamtegea kufanya kazi lakini Yesu alimjibu kuwa amechagua fungu lililo jema!
  Hi mistari haiko mbali sana na maisha ya wakristo wa leo mf. tukichukulia suala la makanisa kuchomwa kweli sio jambo jema lakini tuliambiwa KANISA ni MIILI yetu kwakuwa miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu je ni wangapi wetu tumeyalipua wenyewe makanisa yetu kwa matendo yetu yasiyompendeza Mungu kwa kufanya uasherati ulevi hasira wizi dhuluma wivu masengenyo n.k.
  yeyote aliharibuye hekalu la Roho mtakatifu(mwili) nami nitamuharibu yeye!
  Good to you God send his only begoten son for him who will believe will not be condemed but all who received him gave them to be the sons are the ones who believe the Gospel!
  Even you may gat that all you have to do is just believe and live your belie thats the GOSPEL!
   
 6. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hongera!
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Leo mi nitaadhimisha hii siku kwa kutembelea machinjio zetu kuona kama nyama tunayokula inachinjwa kwenye mazingira gani?
  Kama mazingira hayaridhishi, nitamuuenzi baba wa Taifa kwa kuwa Vegetarian kama yeye.
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  mbona hakuna shida mkuu...cheki hapo napunga upepona kutafakari wema wa Mungu kwangu....
   
 9. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Kwa nini usiende kwenye nyumba za ibada ukatafakari neno la Muumba wako?
  Huko makaburini unatafakari nini mwenzetu?
  Ibada za wafu ni chukizo mbele za Mungu.
   
 10. Mtukuru

  Mtukuru Senior Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :spy::spy::spy::spy::spy:
   
 11. p

  prince pepe JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana. Umenifanya nitafakari vitu vichache lakini muhimu sana katika uhai wetu wanadamu. Mwenyezi Mungu aendelee kukutia nguvu
   
 12. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Una siku ngapi tangu utoke Milembe...!!??
   
 13. z

  zezeta Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijaruhusiwa bado kutoka MILEMBE.... nimeandika haya nikiwa chini ya ulinzi wa madaktarii... nadhani unaweza kunisaidia kuwaambia hawa watu kua nimepona:rant:
   
 14. z

  zezeta Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa ushauri , ila sijaguswa kufanya hivyooo
   
 15. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duuuh! hii kali
   
Loading...