Nimekwama, nmetafuta kadi ya gari bila amfanikio na mke hatoi ushirikiano

Carnivora

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
3,651
5,986
Wakuu habari.

Mwenzenu nimekwama. Tena sana. Mimi ni mfanyabiashara. Si mdogo sana na wala sio mkubwa.

Katika mishe zangu nimenunua ka usafiri kanisaidie hapa na pale. Nina Toyota Spacio, namba DPX kabisa.

Kilichonikwamisha hapa ni kuwa, katika mishe zangu kuna pesa ilipungua kiasi cha mil 5. Nikafight hapa na pale nikapata mil 2. Milioni 3 nikakosa kabisa. Likanijia wazo nichukue gari yangu nikatafute mtu anipe mil 3 akae nayo week moja nitarudisha. Nikaongea wazo langu kwa wife. Akanijibu tu "kuwa makini". Nikiangalia pesa nyingi nimenunua mpunga vijijini huko na sijauuza bado ndio chanzo cha kukosa hiyo pesa. Mil 5 kwangu sio issue sana under normal days.

Asubuhi nikaamkia kwenye mishe kama kawaida. Nilipoona hali si shwari nikaenda home kufata kadi ya gari. Sikuikuta inapokaa. Tafuta weee in vain. Kumuuliza wife anasema naye hajui ilipo niangalie tu vizuri.

Nikajua amenifanyia hiyana. Tumegombana sana. Hajaitoa. Nimeamua kurudi huku nimefura kwa hasira.

Namuwaza sana yule mwanamke, kwake nimekwama. Lakini nawaza sana mishe zangu zilivyokwama.

MY TAKE:

Ni mwendo wa mfumo dume tu. Demokrasia wanawake wanaitumia vibaya na madhara yake tunayapata sisi wanaume.

Sent using my Nokia Torch
 
Sasa hata nikikupa huo mkopo na kadi huna unafikiri utakuwa mwaminifu kweli, itafute nikupe hela ila riba sh ngapi jamaa kakwambia ili nijue nakupa vip
 
Wakuu habari.

Mwenzenu nimekwama. Tena sana. Mimi ni mfanyabiashara. Si mdogo sana na wala sio mkubwa.

Katika mishe zangu nimenunua ka usafiri kanisaidie hapa na pale. Nina Toyota Spacio, namba DPX kabisa.

Kilichonikwamisha hapa ni kuwa, katika mishe zangu kuna pesa ilipungua kiasi cha mil 5. Nikafight hapa na pale nikapata mil 2. Milioni 3 nikakosa kabisa. Likanijia wazo nichukue gari yangu nikatafute mtu anipe mil 3 akae nayo week moja nitarudisha. Nikaongea wazo langu kwa wife. Akanijibu tu "kuwa makini". Nikiangalia pesa nyingi nimenunua mpunga vijijini huko na sijauuza bado ndio chanzo cha kukosa hiyo pesa. Mil 5 kwangu sio issue sana under normal days.

Asubuhi nikaamkia kwenye mishe kama kawaida. Nilipoona hali si shwari nikaenda home kufata kadi ya gari. Sikuikuta inapokaa. Tafuta weee in vain. Kumuuliza wife anasema naye hajui ilipo niangalie tu vizuri.

Nikajua amenifanyia hiyana. Tumegombana sana. Hajaitoa. Nimeamua kurudi huku nimefura kwa hasira.

Namuwaza sana yule mwanamke, kwake nimekwama. Lakini nawaza sana mishe zangu zilivyokwama.

Sent using my Nokia Torch

Nenda polisi kawataarifu kuwa umepoteza kadi ya gari na watakuandikia loss report. Baada ya hapo nenda TRA kafanye mchakato wa kupata kadi nyingine.
 
Siku zitakuwa zishapita.

Sent using my Nokia Torch
 
Sasa hata nikikupa huo mkopo na kadi huna unafikiri utakuwa mwaminifu kweli, itafute nikupe hela ila riba sh ngapi jamaa kakwambia ili nijue nakupa vip
Mkuu uko serious,?

Sent using my Nokia Torch
 
Mkuu samahani sana, ila jua kwamba mke wako ana akili kuliko wewe na ashaona hutarudisha hiyo pesa ndani ya wiki! Nakubaliana na mke wako kuficha kadi ya gari sababu umefanya kuweka gari rehani kwa haraka haraka mnoo!

Leo kamkumbatie huyo mamaa na umpende

Sent using Jamii Forums mobile app
Ana akili kuliko mimi? Unajudge kwa tukio moja. Sisi wafanya biashara ni risk takers. Ye anayetegemea mshahara wa Magufuli serikali mbona hata baiskeli hajanunua?

Sent using my Nokia Torch
 
Sio risk taker,na jua lilivyo kali hivi yani anafikiria kutembea kwa miguu,hahaa make up zote zinayeyuka na jua.
Atembee anaenda wapi? Gari mara nyingi ninayo mimi. Sasa kanifundisha kitu atakosa vinono vingi sana.

Sent using my Nokia Torch
 
Back
Top Bottom