Nimekuwa mtanashati mno hadi kuwa kero kwa wengine

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,954
Wakuu nadhani mko poa,kama kichwa cha habari kinavyojieleza,nimekuwa mtanashati mno hadi naonekana kero kwa watu wangu wa karibu nini nifanye ili nijiepushe na hali hii ???

Kama ujanipata hebu ngoja nikupe mfano wa ninachokieleza,nikisalimiana na mtu kwa kushikana mikono,basi siwezi kuvumilia bila kujifuta na kitambaa au kwa kunawa maji tena wakati mwingine hata mbele za wale nilioshikana nao mikono kiasi cha kwamba wananiona na wanamaindi na wale wanaonijua huwa hawanipi mikono kwa kuniona kama naringa hivi.
 
Unaringia nini? Je uliwahi kudhurika baada ya kupeana mkono na mtu? Unakumbuka ulianza lini tabia hiyo?
 
Kujifuta mikono ninayo na huwa inakuja automatically tu.na si kwamba nafuta mpaka basi. Ni lazima nipanguse kwenye Nguo kidogo hapo ntakuwa na Amani. Na wakati nafanya hivyo hata alonipa mkono hawezi hisi chochote kwani nafanya kwa akili.
Ila hiyo ya kunawa sijawahi.
 
Huo siyo utanashati,ni majivuno,maringo na dharau mkuu
 
Hilo la kupangusa mikono tena kwa kuibia ni kawaida na majority wanafanya!! Lakini kunawa mikono kabisa ni total embarrassment kwa muhusika kama anakuona!
 
Huo siyo utanashati,ni majivuno,maringo na dharau mkuu
Ndio wife wangu anavyoniambia kuwa watu wananiona mimi ninamajivuno,lakini nasema ukweli kabisa kutoka moyoni mwangu sipo hivo ila uwa najiona nimechafuka sana tena sana.
 
Kujifuta mikono ninayo na huwa inakuja automatically tu.na si kwamba nafuta mpaka basi. Ni lazima nipanguse kwenye Nguo kidogo hapo ntakuwa na Amani. Na wakati nafanya hivyo hata alonipa mkono hawezi hisi chochote kwani nafanya kwa akili.
Ila hiyo ya kunawa sijawahi.
Sijui nifanyaje ili niiache hii tabia,maana huwa najihisi kama nimeubeba uchafu mikononi mwangu miaka 10 ?? Na huu wa mikono ni moja kati ya mambo mengi ya ninayoambiwa kuwa nimekuwa "mtanashati mno" wakati mimi mwenyewe najiona niko poa tu.
 
Kwa hiyo unatembea na bobo la maji masaa yote kwa ajili ya kunawa siyo?
Hata kama ni kitambaa unatumia kujifutia huo siyo utanashati ni usharobasha, subiri wataalamu watakuja kukuelezea vyema!
Kunawa maji ni kama nipo na maji karibu,lakini kiujumla nina tabia ya "utanashati iliyopitiliza" kama mkuu chige alivyotoa ushuhuda kwa mama yake basi nami niko hivyo,yaani hadi my wife wangu huwa namkera mno.
 
Unaringia nini? Je uliwahi kudhurika baada ya kupeana mkono na mtu? Unakumbuka ulianza lini tabia hiyo?
Tangu mdogo, na ndio maana michezo mingi yenye asili ya kuchafuka nilikuwa sishiriki.
 
Kweli unaringa...Jirekebishe, we nakupa mkono tunasalimiana halafu unaenda kuuosha au kujifuta kama sio dalili za DHARAU ni nini sasa?? JIREKEBISHE MKUU...Utanashati hauko hivyo!!
Poa,japo kuna kipindi nilijaribu kama wiki hivi nikachemka nikajikuta nimerudia bila ya kujijua.
 
samsun, post yangu nilikuwa nai-edit nikajikuta nimei-delete!! Lakini kama nilivyosema, hapa lazima ule vitofa toka kwa wadau kwavile hawafahamu lakini hilo ni tatizo!! Na hata yale niliyoongea kuhusu mother wala usidhani nimeongeza chumvi... sana sana nimepunguza!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom