Nimekutwa na tatizo la presha, msaada tafadhali wa dawa za asili za kutokomeza hii pesha

Sasa mkuu hizi dawa si naskia unazitumia till end of ur life? Je ukitumia hizi dawa unaweza kuonja kilevi mara moja moja?
Kwani kumeza dawa for life kuna shida gani?
Ni nidhamu tu na mindset yako.

Kama una pressure haushauriwi kutumia zaidi ya Bia Moja kwa siku au Mbili kwa siku kulingana na Jinsia yako.

Kwa hiyo pombe piga tu ila sio kupitiliza, alafu mwambia daktari wako akuangalizie dawa hazina interaction na Pombe kama wewe ni mpenzi au Online mwenyewe tumia apps zinaitwa Interaction Checker

Hapa siongelei zile spiritis kali naongelea vinywaji ordinaly vyenye % ndogo.
 
Wakuu salama hapa

Tangu mwezi wa 1 mwanzoni nilijiskia hali fulani ya kuumwa kichwa nikapima magonjwa mbalimbali hakuna tatizo

Mdogo wangu akanishauri nipime presha kweli nikakuta nayo ipo juu

Nikajiuliza nimeitoa wapi manake naishi maisha simple nakula vyakula simple visivyo na chumvi nyingi Wala mafuta mengi

Pombe nakunywaga lakini sio kupita kiasi ni mara moja moja tu,sivuti sigara,so nikashindwa kupata jibu

Kuna wakati nilikumbwa na stress sana hasa za kifamilia mke mzinguaji mno,nikahisi labda ni stress nikaanza kupotezea

Nikaanza kuishi kwa kubadili life style nikapunguza kabisa pombe ,nakula vitunguu swaumu na kula vyakula vyenye madini ya potassium kama viazi na ndizi

Lakini bado presha imeendelea kuwepo japo inshuka kiasi ,na sometimes inapanda

Sasa wiki moja nyuma nimeenda kupima malaria manake nilikuwa najiskia nina homa,nikapima na presha nikakuta ipo juu kiasi dokta akaniuliza baadhi ya maswali nikamjibu akaniambia nipime kipimo cha cholesterol,Figo na malaria lakini majibu yako safi kabisa

Akanipa madawa kibao ya presha yale ya kumeza kila siku maishani,je nauliza hakuna single dozi hata ya kienyeji ya kuondoa Ili tatizo ,hizi dawa sijaanza kumeza

Umri wangu miaka 33 ,ushauri tafadhali.
Tatizo mnaharakisha kuoa. At 33 umeoa! Unatakiwa kuoa ukiwa 40 na kama ukiwahi uwe 35.
 
Kwani kumeza dawa for life kuna shida gani?
Ni nidhamu tu na mindset yako.

Kama una pressure haushauriwi kutumia zaidi ya Bia Moja kwa siku au Mbili kwa siku kulingana na Jinsia yako.

Kwa hiyo pombe piga tu ila sio kupitiliza, alafu mwambia daktari wako akuangalizie dawa hazina interaction na Pombe kama wewe ni mpenzi au Online mwenyewe tumia apps zinaitwa Interaction Checker

Hapa siongelei zile spiritis kali naongelea vinywaji ordinaly vyenye % ndogo.
Asante mkuu,so pombe Kali hazifai kutumia sio?
 
Wakuu salama hapa

Tangu mwezi wa 1 mwanzoni nilijiskia hali fulani ya kuumwa kichwa nikapima magonjwa mbalimbali hakuna tatizo

Mdogo wangu akanishauri nipime presha kweli nikakuta nayo ipo juu

Nikajiuliza nimeitoa wapi manake naishi maisha simple nakula vyakula simple visivyo na chumvi nyingi Wala mafuta mengi

Pombe nakunywaga lakini sio kupita kiasi ni mara moja moja tu,sivuti sigara,so nikashindwa kupata jibu

Kuna wakati nilikumbwa na stress sana hasa za kifamilia mke mzinguaji mno,nikahisi labda ni stress nikaanza kupotezea

Nikaanza kuishi kwa kubadili life style nikapunguza kabisa pombe ,nakula vitunguu swaumu na kula vyakula vyenye madini ya potassium kama viazi na ndizi

Lakini bado presha imeendelea kuwepo japo inshuka kiasi ,na sometimes inapanda

Sasa wiki moja nyuma nimeenda kupima malaria manake nilikuwa najiskia nina homa,nikapima na presha nikakuta ipo juu kiasi dokta akaniuliza baadhi ya maswali nikamjibu akaniambia nipime kipimo cha cholesterol,Figo na malaria lakini majibu yako safi kabisa

Akanipa madawa kibao ya presha yale ya kumeza kila siku maishani,je nauliza hakuna single dozi hata ya kienyeji ya kuondoa Ili tatizo ,hizi dawa sijaanza kumeza

Umri wangu miaka 33 ,ushauri tafadhali.
Mkuu pole sana hujasema una kilo ngapi mwilini mwako? Nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia presha yako uguwa pole.
 
Thanx nitakufuata PM uzito mara ya mwisho nina 66 kg

Mtafute clinical dietitian Kwa ajiri ya Tiba Lishe Na mpangilio WA mazoezi, Kipindi pia unaendelea na matibabu mengine hapo hospitali
 
Normal pressure inatakiwa isizidi 120/80 wewe umepimwa una ngapi?
Haina kipimo maalumu,ila mara zote nlizopima haiwajawahi kushuka chini ya 170, mara ya mwisho nimepima ikawa 180 namba ya chini sikumbuki,nikaondoka hospital nikaenda mahali niliporudi tena kucheck imepanda kutoka 180 mpaka 220
 
Angalia wajasiria mali wa ‘tiba mbadala’ wasiku fannye fursa kwa vitiba vyao visivyo eleweka..
 
Haina kipimo maalumu,ila mara zote nlizopima haiwajawahi kushuka chini ya 170, mara ya mwisho nimepima ikawa 180 namba ya chini sikumbuki,nikaondoka hospital nikaenda mahali niliporudi tena kucheck imepanda kutoka 180 mpaka 220
Tazizo lako niSawa na langui, inawezekana kabisa pamoja na kuwa tatizo la presha ya kupanda vile vile una ‘white coat syndrome’
 
Mkuu hata mimi ni mhanga wa hilo tatizo natumia dawa za hosptal lakin hivi pande kupitia ndugu yangu mwenye tatizo hilo alipata dawa ya kienyeji ambayo yeye alikuwa na presha kubwa sana na amepona na mie ni shuhuda kuwa walikuwa na presha kubwa ...kwa hiyo amenitafutia na mie nimeanza kutumia kweli naona improvement maana nimeacha kabisa za hosptal naona mwanga nikimaliza dose kama ntakuwa fresh tutawasiliana.
 
Dawa yako uiinunua kiasi gani na inatumika kwa muda gani mpaka kumaliza dozi?
 
Kweli kuna wenye ‘bahati zao’ ambao huwa wanapona kabisa presha kwa kutumia tiba za kienyeji ....case hizi ni chache sana
 
Tazizo lako niSawa na langui, inawezekana kabisa pamoja na kuwa tatizo la presha ya kupanda vile vile una ‘white coat syndrome’
Niliambiwa na super specialist mmoja pale JKCI juu ya hiyo ‘white coat syndrome’ akasema ikitokea umeonwa na daktari asiye mzoefu na asiyetaka kuumiza kichwa kwa kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kutoa hitimisho, vipimo vilivyoletwa na hiyo ‘white coat syndrome’ vinaweza kupelekea mtu kudubikwa madawa ambayo hastahili, na kusabisha hypotension ambayo ni deadly pia.

Hivyo ni muhimu kuwa tunajipima wenyewe mara kwa mara nyumbani ukiwa ume-relax. Angalau hata mara moja kila miezi 3! Hii itasaidia kujua hali yako; na unaweza kwenda na majibu ya vipimo hospitalini pale unapoenda ili kuepusha hilo nililolisema hapo juu.
 
White coat syndrome ndo nini mkuu
Hali ya uoga na hofu ya mazingira ya hospitali (white coat yale ambayo madaktari uvaa) ambayo upelekea vipimo vya BP kuwa juu kuliko kawaida yako. Lakini hii lazima iwe proved kwa mtu kuwa anafanya vipimo sehemu nyingine isiyo hospitali ili kudhiirisha kwamba ni white coat syndrome ama siyo.
 
Back
Top Bottom