Nimekutana nayo mahali ikanifikirisha....!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,395
attachment.php

Hii nimekutana nayo mahali na ni nyumba ambayo inaishi wapangaji, sina uhakika kama ni miswaki ya familia moja.
Namna hii ya kuhifadhi miswaki imenifikirisha kidogo. Tunaambiwa kwamba maradhi kama Ukimwi unaweza kuambukizwa kwa kuchangia pamoja na vitu vingine lakini pia miswaki imetajwa. Ukiangalia namna miswaki hii ilivyowekwa naona ni sawa tu na kuchangia miswaki.

Labda tu niwaulize tu wenzangu, je huwa mnaweka miswaki yenu hapo nyumbani kwenu namna gani?
 
Attachments

  • Miswaki.jpg
    Miswaki.jpg
    300.6 KB · Views: 1,775
attachment.php

Hii nimekutana nayo mahali na ni nyumba ambayo inaishi wapangaji, sina uhakika kama ni miswaki ya familia moja.
Namna hii ya kuhifadhi miswaki imenifikirisha kidogo. Tunaambiwa kwamba maradhi kama Ukimwi unaweza kuambukizwa kwa kuchangia pamoja na vitu vingine lakini pia miswaki imetajwa. Ukiangalia namna miswaki hii ilivyowekwa naona ni sawa tu na kuchangia miswaki.

Labda tu niwaulize tu wenzangu, je huwa mnaweka miswaki yenu hapo nyumbani kwenu namna gani?

niliwahi kuangalia documentary moja ya maid wanavyowakomoa mabosi washenzi. mdada wa kazi alichukua mswaki wa boss bafuni, akautumia kusafisha choo halafu akaurudisha unapokaa,boss akaja akauchukua na kupiga mswaki kama kawa, tangu siku hio mswaki wangu haukai bafuni[na siishi nyumba ya kushare now ila nishazoea] na kabla ya kupiga mswaki nausafisha vizuri kwanza.
 
hahaha lakini mtambuzi ukimwi unaweza kuambukizwa kwa miswaki kukaa pamoja kweli ???ikiwa kila mtu anapomaliza kuswaki anasafisha mswaki wake na maji
 
Kama ni kweli hiyo ni nyumba ya kupanga Sio ustaarabu kuweka hivyo
Ni vyema kila mmoja ahifadhi kwake
 
Du wale watoto wadogo wanaopigishwa mishwaki na haouse girls!!! Mitihani ipo wakubwa. Ila nimejifunza kuwa kila mmoja katika familia awe na sehemu yake ya kuhifadhia mswaki wake.
 
Na kawaida ya mswaki at least kila mwezi unatakiwa kubadilisha hapo naona kuna mwingine tokea enzi zileee
 
niliwahi kuangalia documentary moja ya maid wanavyowakomoa mabosi washenzi. mdada wa kazi alichukua mswaki wa boss bafuni, akautumia kusafisha choo halafu akaurudisha unapokaa,boss akaja akauchukua na kupiga mswaki kama kawa, tangu siku hio mswaki wangu haukai bafuni[na siishi nyumba ya kushare now ila nishazoea] na kabla ya kupiga mswaki nausafisha vizuri kwanza.

Nawewe unatesa house maids? If not kwanini ufiche? Akikukosa kwenye mswaki atakupata kwingine tu
 
hii ni hatari sana kwa afya loh nyumbani ndo napaamini kwa sababu najua. afya zetu lakini kwingine mswaki wangu nautunza kwenye begi mweh heri nusu shalikuliko shali kamili
 
Back
Top Bottom