Nimekutana nae akiwa na beseni la mchicha kichwani na mtoto mdogo mgongoni

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,778
Huyu binti alikuwa mrembo na mzuri wa aina yake. Hakika nilimpenda kwa dhati! Ilikuwa ni mwaka 2019 nilipomuhitaji kimahusiano zaidi, nikiamini kuwa atakuwa binti pekee nitakayefunga nae pingu za maisha hapo baadae.

Huyu binti hakutaka kunielewa kabisa, nilijaribu kujipendekeza katika maisha yake, kujaribu kumsurprise kwa zawadi za hapa na pale lakini ilikuwa kazi bure! Kauli pekee ninayoikumbuka ni ile ya "Wewe huna pesa za kunihudumia, tafuta kwanza pesa kisha rejea kwangu ndo uanze kuniimbisha ngonjera zako hizo zisizo na kichwa wala miguu". Na ndiyo siku ambayo niliacha tabia ya kumfuata fuata rasmi, kauli hiyo ilinipatia uchungu wa kuanza harakati za kuisaka pesa mahali ilipo huku nikiyavumulia maumivu ya binti huyo kuchakatwa mbususu na shombe shombe fulani hivi la kiarabu pale mtaani.

Miaka mitatu sasa, tumekutana mkoa mwingine kabisa wa utafutaji. Nimekutana nae akiwa na mtoto mdogo mgongoni, muafrika tiii, huku akiwa na kisu mkononi akikatakata mchicha na kuweka kwenye vijimifuko transparent!

Sio kwamba tayari maisha nimekwisha yawezea, ila kidogo nina msingi wa kuniwezesha kuoa na kutunza familia! Ama kweli, malipo ni hapa hapa duniani.

Sijamchangia hata fungu moja, nimemtazama kama dakika moja hivi na kumwacha pale akiwa anatiririsha chozi taratiiiibu!
 
Huyu binti hakutaka kunielewa kabisa, nilijaribu kujipendekeza katika maisha yake, kujaribu kumsurprise kwa zawadi za hapa na pale lakini ilikuwa kazi bure! Kauli pekee ninayoikumbuka ni ile ya "Wewe huna pesa za kunihudumia, tafuta kwanza pesa
Aisee una roho mbaya, yaani umekataa hata kununua mchicha wa mia?
 
Unajiwahi kusema una msingi tayari wa maisha
Maisha hayaendi hivyo huyo huyo pia kesho unaweza ukayatamani maisha yake

Msipangiane maisha kila mmoja ana yake
 
Huyu binti alikuwa mrembo na mzuri wa aina yake. Hakika nilimpenda kwa dhati! Ilikuwa ni mwaka 2019 nilipomuhitaji kimahusiano zaidi, nikiamini kuwa atakuwa binti pekee nitakayefunga nae pingu za maisha hapo baadae.

Huyu binti hakutaka kunielewa kabisa, nilijaribu kujipendekeza katika maisha yake, kujaribu kumsurprise kwa zawadi za hapa na pale lakini ilikuwa kazi bure! Kauli pekee ninayoikumbuka ni ile ya "Wewe huna pesa za kunihudumia, tafuta kwanza pesa kisha rejea kwangu ndo uanze kuniimbisha ngonjera zako hizo zisizo na kichwa wala miguu". Na ndiyo siku ambayo niliacha tabia ya kumfuata fuata rasmi, kauli hiyo ilinipatia uchungu wa kuanza harakati za kuisaka pesa mahali ilipo huku nikiyavumulia maumivu ya binti huyo kuchakatwa mbususu na shombe shombe fulani hivi la kiarabu pale mtaani.

Miaka mitatu sasa, tumekutana mkoa mwingine kabisa wa utafutaji. Nimekutana nae akiwa na mtoto mdogo mgongoni, muafrika tiii, huku akiwa na kisu mkononi akikatakata mchicha na kuweka kwenye vijimifuko transparent!

Sio kwamba tayari maisha nimekwisha yawezea, ila kidogo nina msingi wa kuniwezesha kuoa na kutunza familia! Ama kweli, malipo ni hapa hapa duniani.

Sijamchangia hata fungu moja, nimemtazama kama dakika moja hivi na kumwacha pale akiwa anatiririsha chozi taratiiiibu!

Na hili nalo mkalitizame
We nae sijui Lin utaacha uongo aiseh.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom