Nimekutana nacho asubuhi

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,444


Leo wakati nawahi kutafuta ridhiki nimekutana na hii kitu njiani karibu na shamba la mahindi mara kwa kwanza nilishtuka nikakumbuka kuna Yesu na Mtume nikataja jina la Yesu na Mtume Mohamed nikarudi tena kuchukua picha ya hii sufuria ndani yake mlikuwa na magome ya miti yai na maji kama unavyo ona. Hili advataizi naona mhusika anajua kwa nini ameweka tunguli hapo shambani kwa vile nimeaga Sumbawanga na nina mtegemea Yesu na Mtume Mohamed S.A.W naamini hakuna kitakacho nipata kwa kuangalia tunguli hiyo.
 
Mkuu umekosea sana!!!ungecheki yai kama sio viza unalikaanga unapata kifungua kinywa!!


Umefikiria kama mimi,ingenikuta mimi hiyo nishabeba sufuria zamani,hayo matakataka yake namwaga nishapunguza bajeti ya sufuria ya ugali mchana....
 
Tafsiri yake ni kwamba angekuroga lakini ameshindwa kwa sababu unaye Yesu aliye hai, ndio maana pale kaweka ka msalaba na damu nyekundu

Hahahahaha. Sasa ww umekuwa mtabiri wa juju!? Umejuaje kwamba huyu jamaa ana yesu. Au kwa sababu kasema. Na umejuaje kama hio juju imemkwepa. !? Huenda ndo chanzo cha nuksi. Yafaa kufuats ushauri wa wataalam
 
Huyo kuku aliyetaga hapo ana akili kweli, yaani ameamua kurahisisha kazi kwa mlaji...hapo ni kuweka maji na kuchemsha tayari kwa staftahi
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom