Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Pole sana ndugu yangu,jaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo lako kwa njia bora pasipo kutikisa imani yako kwa Mungu..
 
Ilikuwa miaka ya 2001 tulikuwa tunaendaga sana coco siku ya jumamosi na jumapili, mshikaji wetu akatuacha baada ya maongezi na huyo demu akamwambia anakaa mitaa ya Morocco (nanukuu) Kwa hiyo wakaamua watembee maana sio mbali walipokuwa wanakaribia karibia na kanisa wakati mshikaji anaendelea kuongea akajikuta yupo pekee yake

Mshikaji akajua labda yule mdada amesimama kuangalia vizuri haoni mtu.

Akajaribu kujiridhisha labda arudi kidogo kumuangalia hakuona mtu zaidi ya watu wengine waliokuwa wanarudi kutoka beach.

Mshikaji hakudumu na tokea hapo alikuwa ni mtu wa kuumwa mpaka 2003 mwanzoni tukampoteza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Itakuwa uyo jini kaamua kumchukua mazima akalr raha huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jini lenyewe limeshakuambia linashindwa nanini mbona? Limekuambia ulipokuwa na huyo mchumba wako wa awali lilishindwa kwasababu yeye ni muombaji sana.

Very simple mfuate mchumba wako kesi itaisha. Atakuombea na kukupeleka kwa mchungaji.
Mpaka sasa jini ameshampata jamaa,kakubali kuzivaa nguo zake na kuzitoa tena na kumkabidhi jini. Maana yake sasa nguvu za jamaa zote zinategemeana na jini anachotaka mpaka kwenye maamuzi. Mfano jamaa akifikiria kumfuata huyo demu,jini anajua nini anafikiria,kwa hiyo anaweza kupiga hata hatua 5,baada ya hapo anasahau wapi alikuwa anaenda,hapo mpaka sasa hawezi kufanya tena kitu cha kumuumiza jini,ndio maana ameacha hata kutoa humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa jini ameshampata jamaa,kakubali kuzivaa nguo zake na kuzitoa tena na kumkabidhi jini. Maana yake sasa nguvu za jamaa zote zinategemeana na jini anachotaka mpaka kwenye maamuzi. Mfano jamaa akifikiria kumfuata huyo demu,jini anajua nini anafikiria,kwa hiyo anaweza kupiga hata hatua 5,baada ya hapo anasahau wapi alikuwa anaenda,hapo mpaka sasa hawezi kufanya tena kitu cha kumuumiza jini,ndio maana ameacha hata kutoa humu

Sent using Jamii Forums mobile app


Hakuna kitu kama hicho.
 
Nenda kwa Prophet T B Joshua, nenda pale kwa Martha akuandikishe uende
Habar zenu wadau

Naomba mnisaidie maana nipo njia panda sielewi nifanye nini. Waswahili wanasema mficha maradhi Kifo humuumbua.

Mimi sitaki kusubiri Kifo kinikute. Ileweke nimekuwa humu JF kwa muda mrefu, Mara nyingi nimekuwa msomaji tu, wa matukio ya watu, pamoja na kujielimisha, Mara chache sana nimekuwa nikichangia mijadala pale inapobidi. Hii ndio thread yangu ya kwanza. Hivyo sijaandika kwa ajili ya kuburudisha/kumtisha mtu, ninachokiwasilisha hapa Ni ukweli mtupu. Lengo na madhumuni Ni kupata ushauri na msaada pale inapobidi.

***** ****** ******** ******** ******
Iko hv, Mimi Ni mfanya biashara mdogo ninaejishughulisha na uuzaji wa nguo za kiume katika sehemu Fulani hv hp jijini DSM. Kiufupi Nina maduka mawili ya nguo za kiume, hiyo ndio ajira yangu inayonifanya niishi hapa mjini. Sasa mnamo Tar 27 Dec ya mwaka Jana (2018)nipo ktk moja ya ofisi yangu na endelea na majukumu yangu ya kawaida, tena nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi mida ya Kama saa 7 mchana kuelekea saa 8 hv, alikuwa mteja ambae Ni mwanamke ( Alikuwa mrembo sana, mweupe Ana asili Kama ya kiarabu hv) ila rafudhi Ni yakipemba. Kama kawaida nikawa namsikiliza, akaniambia nimchagulie nguo nzuri anataka ampelekee mme wake, Yani shati na suruali.
Wakati naendelea kumchagulia nikawa namuuliza anavaa size gani? Akacheka akasema yupo Kama wewe, kwa kila kitu...Tena akaongeza na kusema nguo nitakazo zipenda Mimi hata yy atazipenda.
Nikawa namtania, nikamwambia kwa jinsi ulivyomzur hvy nataman mume wako niwe Mimi, akaniuliza Kweli? Nikamwambia hakuna mwanaume chini ya jua anaweza kukukataa msichana mrembo Kama wote tukacheka.
Zoezi la kuchagua nguo likaendelea tukafanikiwa kupata nzuri akazipenda. Tumezoea wabongo tunapenda discount, lkn kwake ilikuwa ni tofauti, akauliza nikiasi gani alipe, nikamwambia akalipia bila kuomba punguzo la Bei Kama tulivyozoea kwa wateja walio wengi. Wateja wa namna hii hutokea ila ni marachache sana, hvy nilifurah maana inakuwaga bingo unapata faida nzur.
Nikiwa namfungia hz nguo, aliniuliza...umeoa? Nikamwambia hapana akacheka akasema, nilijua tu...huwez kuoa mapema 7bu unapenda pombe na wanawake wa aina tofauti tofauti, kifupi we Ni mzinifu. Hii ya pombe ilinistua kidogo, amejuaje mm nakunywa pombe, ila sikutaka kumuonesha hadharani.
Akaniambia, Kuna sehemu anaenda hvy akirudi atauputia mzigo wake, ila nimuhifadhie, akaniuliza huwa nafunga saa ngapi? Nikamwambia, akaniomba namba ya simu Kama sitojali nimpe ili Kama atachelewa anijulishe nisije chelewa kufunga kwa 7bu yake. Nami sikuona Tatizo, kwanza Ni mteja lakini pia Ni mrembo sana Kama tunavyojijua sisi wanaume, basi nikampa namba, akaaga na kuondoka.
************
Hapo ndipo kizazaa kilipoanza. Hata hapa naandika thread hii, Sina amani kabisa. Kufika mida ya Kama saa mbili na robo usiku, sms ikaingia kwenye simu yangu.inasema "Zawadi niliyo kununulia umeipenda"? Mmmh, mm nikahisi itakuwa mtu kakosea namba, coz ilitokea namba mpya, baada ya Kama dk 10 hv, ile namba iliyotuma sms ikawa inanipigia, kupokea nasikia sauti ya msichana, akaniuliza...mbona hujajibu sms yangu hau unapenda zawadi yangu, nikamuuliza unajua unaongea na Nan?
Akasema ndio Ni Fulani (akataja jina langu), nikashangaa nikamwambia mbona hakuna mtu nilimwagiza zawadi akasema, Tena umechagua na kuzijaribisha mwenyewe Mara hii umesahau? Akawa anacheka akaniuliza umeshanikumbuka? Nikamwambia ndio...nikamuuliza umejuaje jina langu wakati sikumtajia, (Nilimdanganya jina) Mara nyingi Sina destruri ya kukwambia jina langu la ukweli mtu nisie mjua, Hilo likanishangaza...nikachekecha akili nikahis labda ameangalia kwenye tigo pesa maana nilimpa namba ya tigo, swali lililozidi kuniumiza akili anawezaje kuja dukani kwangu kuninulia nguo Ikiwa hanifahamu, wakat aliniambia Ni za mumewe?
Nikamuuliza si ulisema unampelekea mumeo? Akaniambia kwani wewe hufai kuwa mume wangu? Akiwa anacheka, akaendelea.....na si ulisema hujaoa au ulinidanganya? Nikabaki na kigugumiz nisiamini ninachokisikia, akaniambia nimeamua kukutunuku. Usiku mwema, nitakuja kukutembelea siku nyingine akakata simu. Nikabaki na maswali chungu nzima, kupiga ile namba ikawa haipatikan...baada ya hapo ndio vitimbi vilipoanza.

Itaendelea.......

NB: Nimechoka kuandika nitaendelea kesho ila kiukweli mwezenu nipo njia panda sielew, mwaka nimeanza na mauzauza

Sehemu ya Pili



Sehemu ya Tatu




Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mpenzi jini nae anapitia Jf.....tukikushauri an block njia mapema
 
Mwambie nenda sumbawanga kaibe kwa mtu mwenye uchawi alafu akirudi salama uje utuhabarishe.

Kuna vijana watu walikwenda kuiba miwa kwa babu fulani wakajua hakuna shida, baada ya siku mbili kupita babu akatangaza walioiba waende wakamuombe samahani lakini hawakwenda.

Siku 5 zilipita baada ya lile tangazo kisha akatoa nafasi ya mwisho na akasema asije akalaumiwa lakini bado hawakwenda.

Baada ya wiki kuisha tangu wizi utokee mmoja wa wale vijana alidonolewa mguuni na kuku aliyetotoa vifaranga kisha mguu ukaanza kuoza ikabidi ukakatwe na hadi leo ni kilema napo alipona baada ya kwenda kumuomba msamaha mzee wa watu.

Kijana mwingine alipata ugonjwa,macho yalivimba hadi yakatoka nje na yakawa yanatoa maji. Alikwenda kufanyiwa upasuaji wa macho lakini hakuchukua muda akafa.

Watatu alikua ni binti kati ya miaka 18-20 yeye yeye inasemekana alikula tu lakini hakubeba miwa kwenda nayo popote lakini aliugua ugonjwa wa ajabu kama mtu mwenye polio.

Mwili wake ulikonda sio kawaida, mguu mmoja ulikua mwembamba kama fimbo kuanzia paja hadi karibu na unyayo pote palikua sawa na mguu mmoja ulikua kama mwenye matende na alikua akikojoa mkojo sisimizi wanajaa muda huo huo mahali alipokojoa.

Ndugu wakampeleka hospitali kubwa wakampima magonjwa yote hadi kisukari lakini hawakuona kitu. Baadaye wakaenda kwa waganga na mganga akawaambia hana uwezo wa kutibu labda aende alikofanya wizi kwa mzee fulani (akataja jina) ndio akaombe samahani ndipo atapona.

Basi wakaenda kwa yule babu wakaomba samahani na babu akawaeleza kuwa wamechelewa hawezi lakini atajaribu, binti alipigwa kofi zito na kuambiwa toka hapa na ukome kuiba kisha akawaeleza nendeni. Usiku bimti alikua akitokwa jasho sana na baada siku tatu mwili ukaanza kurudi hadi akapona kabisa.

FANYA JEURI USIKUTANE NA KONKODI UTAKUA SALAMA LAKINI UKIKUTANA NA CHAWI HALISI UMEKWISHA.

Karibu Sumbawanga haurogwi bila kupewa nafasi ya kujitetea.
Jeuri zako ndio kaburi lako, unaambiwa ukaombe samahani na ukienda hana shida tena na wewe lakini ukidharau wanatuma makombora ya Atomic popote yanakufikia hata uwe nje ya nchi

Mkorintho wa 6
Hapo kwenye kofi niache kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Kaka yangu, nimesoma uzi wako mwanzo mpaka mwisho najikuta nataka kudondokwa na machozi, pole sana kwa kipindi hiki kigumu, ila amini kwa mungu yote yanawezekana. Ushauri wangu Kaka, mruhusu mama awashilikishe watu wengine kama ulivyo tushilikisha na sisi, lakini pia nenda kanisani unakosali au popote awashilikishe watumishi wa mungu, hana uwezo wa kushindana na nguvu ya mwenyezi mungu. FANYA hivo usijekushauriwa kwenda kwengine tofauti na kanisani, ikiwezekana kabisa hata huyo EX Wako aliyekuwa kizuizi mwanzo umshilikishe japo haitakuwa rahisi kukuelewa. MUNGU AWE NA WEWE KAKA YANGU
 
TATHMINI :-

1) Ni ngumu sana kwa msichana uliyempenda haswaa kama ulivyosema mwanzoni kwenye sehemu ya kwanza akuulize jina then umdanganye kwa kumtajia jina la uongo....!

2) Kama kweli wewe ni Mkristo na hukuwahi kufanya ushirikina basi baada ya kutokewa na hayo mambo siku ya kwanza tu...LAZIMA ungemtafuta kiongozi wa kiroho / dini akuombee.

3) Kwa hali hiyo kama ni kweli usingethubutu kumpelekea nguo kigamboni ukiwa peke yako, lazima ungeenda na mtu kwa kuogopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom