Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Hapa umecheza fresh. Watu watakuja kuomba namba ya huyo mlinzi.wewe utawaunganisha na jamaa ambaye tayari mpo naye kwenye mchakato.halafu unakula cha udalali.

Niliwahi kuwa na mtu wa namna hii (ingawa ni ndotoni tu) mwanzoni nilijua ni ndoto lkn kadri mda ulivyoenda nikaanza kugundua matukio yanafuatana.

Ilifika wakati hata kuwa na girlfriend ni shida na mbaya zaidi hata nikitaka kufanya mambo yangu hakuna kinachowezekana.

Na nikiondoka hapo nitapata usingizi wa ghafla na nitasemwa hadi nifurahi zaidi kuna adhabu anaweza kukupeleka juu sana alafu anakuambia Nakuacha hapa udondoke ufe.

Kadri mda unavyoendelea alikuwa hana mchana wala usiku akinihitaji lazima nipumzike sehemu na hapo ninakuwa nae hadi atakapofurahi pia wakati huo hakuna mtu atakuja kuniamsha na hata kama angekuwa Boss nipo ofisini anaweza na kunipa ruhusa nikapumzike kwa amani kabisa.

Mambo ni mengi lkn kuna mlinzi wa mahali fulani baada ya kumshirikisha akasema atanipa dawa ya kuogea itanisaidia maana anafahamu dawa ingawa baada ya mlinzi yule kuniambia hivyo nilichukuliwa na kupewa vitisho vikali na safari walikuwa mabinti kama saba hivi nikavushwa juu ya mawingu wakaniambia wananiacha nidondoke nife.

Niliwaomba sana wasifanye hivyo na wanipe mda nifikiri nikazinduka nikamwambia tena yule mlinzi akasema watakusumbua sana lkn hawatakufanya kitu.

Siku hiyo hakuja tena nikisubiri kesho yule mlinzi aniletee dawa na kesho jioni kama saa kumi na moja akaichukua tena akasema naona dawa yako unaletewa ila kwaheri.

Nilivyozinduka nakutana na simu ya mlinzi ananiambia tuonane nakupa dawa uweke kwenye maji ya kuoga kila unapooga kwa siku saba.

Hadi mda huu ni miaka zaidi ya 15 sijapata shida kama hizi ila natambua haya mambo yapo na mwanzoni alivyoondoka nilikuwa nina m miss maana sijawahi kutana na mtoto mzuri kama yule katika maisha yangu.

Matukio ni mengi siwezi kuyaandika hapa ila mtambue Haya mambo yapo hapa ulimwenguni na usipokutana nayo huwezi amini hata kwa kushikiwa kisu.
 
Humu watakuja watu kuyatete majini na uzi utaishia kuwa vita vya kidini.watu upande wa majini na walio kinyume na majini. Subirini tu.
 
Unamwelekeza ushirikina halafu unamwambia alale na biblia unadhani biblia inamzuia shetani?shetani naye anaijua biblia na anaisoma sana tu.hayo ya kuoga maji chumv na kunuiza tayari ni ushirikina.usichanganye madesa

Pole sana mkuu, huyo ni mpenzi jini amekutunuku

Kuna tiba moja rahisi sana inaweza kukusaidia ukiifanya kwa bidii. Chumvi!!

Nenda kanunue chumvi ya mawe sokoni alafu uwe unaweka kwny maji yako ya kuoga (nusu kiganja cha mkono)

Oga fresh ukimaliza yale maji ya mwisho (ndo yatakuwa na chumvi haswa) jimwagie na mikono kama unaoga hv huku unanenea maneno ya kujisafisha na kujinasua kwa huyo jini kisirani.

Nuia kila kitu, kama umelishwa vitu vichafu nuia vitoke, kama umechanjwa futa kama umetupiwa nuia litoke. Fanya hvyo kila siku asbh na jioni kwa siku saba, hatakusumbua tena huyo kibwengo.

Pendelea kulala na biblia kitandani

Pendelea kulala redio ikiwa on weka station za dini hasa praise power.

Mungu akuvushe salama katika janga hilo. Ila amini litaisha na utakuwa salama tu

Be Humble is free of charge
 
Jamani eeeh samahani sana kwa kupachika swali nje ya mada,

Ni kwamba pm yangu inaonyesha kuna SMS tatu,lakini nikifungua inaniambia empty msg hii naitatuaje niweze kusoma SMS zangu!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, huyo ni mpenzi jini amekutunuku

Kuna tiba moja rahisi sana inaweza kukusaidia ukiifanya kwa bidii. Chumvi!!

Nenda kanunue chumvi ya mawe sokoni alafu uwe unaweka kwny maji yako ya kuoga (nusu kiganja cha mkono)

Oga fresh ukimaliza yale maji ya mwisho (ndo yatakuwa na chumvi haswa) jimwagie na mikono kama unaoga hv huku unanenea maneno ya kujisafisha na kujinasua kwa huyo jini kisirani.

Nuia kila kitu, kama umelishwa vitu vichafu nuia vitoke, kama umechanjwa futa kama umetupiwa nuia litoke. Fanya hvyo kila siku asbh na jioni kwa siku saba, hatakusumbua tena huyo kibwengo.

Pendelea kulala na biblia kitandani

Pendelea kulala redio ikiwa on weka station za dini hasa praise power.

Mungu akuvushe salama katika janga hilo. Ila amini litaisha na utakuwa salama tu

Be Humble is free of charge
Amkabidhi Yesu maisha yake, halafu kila siku ale nguruwe. Jini na nguruwe ni maji na moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wanajamvi, kipekee kabisa nipende kuwashukuru, kwa michango yenu katika ushauri juu ya tatizo lililo nikumba. Pia, namshukuru Mungu naendelea vyema kabisa, ingawaje vita ni kubwa mno...kwa sasa nimeshauriwa nisiseme chochote (sio kwa ubaya) ila ni kwa ajili ya usalama wangu pia.

Kwa wale wenye hofu na wasiwasi mm ni mzima wa afya... Ingawaje kumetokea mambo mengi sana ya kunirudisha nyuma, ikiwa ni pamoja na matapeli waliochukulia tatizo langu kama fursa. Nimepoteza pesa nyingi sana katika kutafuta suluhu la jambo langu, lakini nikiri wazi Mungu aliejuu mbinguni ashindwi na kitu, naamii atarejesha kila nilichopoteza.

Kwa sasa nimefunga biashara zangu zote (kwa muda) ili niokoe maisha yangu. Kwa sasa nipo kambini na timu ya maombi sehemu fulani (nisingependa kupataja) wananifanyia huduma. Kiukweli kabisa Vita ni kubwa mno Mama yangu kaponea chupu chupu kumpoteza.

Pia niwaweke wazi katika hili...mimi ndio msaada mkubwa katika familia yangu, matatizo haya yamesababisha ni yumbe sana kiuchumi. Hapa nilipo sina chochote (fedha) timu ya maombi inakesha usiku na mchana kunipigania..ukweli ni kwamba kama si nyinyi wana JF kunisisitiza ishu ya maombi nisingekuwa hai sasa. Naomba muendelee kuniombea pia.

Nashindwa nisemeje lkn najisikia aibu na fedhea kubwa kwa watu wanaopigania maisha yangu kushindwa kuwahudumia hata chakula na maji. Sio malipo kama wengine walivyohitaji ni bure kabisa ila hawa nao pia ni binadamu. Kama kuna yoyote ataguswa katika hili naomba aje Pm nitampa utaratibu aweze kunichagia chochote alichonacho (Nisieleweke vibaya tafadhali) kama utaguswa katika hilo naamini kabisa Mungu hatukuacha kama ulivyo ulipotoa atakuongezea mara dufu.

Nawashukuru sana kwa msaada wenu wana Jamii Forum. Niwatakie mchana mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kwa kuchangamkia fursa. Nawe umeona uje utangaze biashara yako huku? Kweli JF kiboko. Wanawake wenye akili huwa hawapendi kabisa wajulikane au waonekane hata kidole.wewe unatuwekea picha za ngwala zako ili watu waanze kukutafuta ?maana nyie ndo mnaitwa mizoga mnawatega mafisi ambayo anytime yanataka kula wanawake mizoga.

Mnataka kuharinu uzi wa jamaa hapa kwa nini msitumiane pembeni mpaka uje kufanya matangazo kwenye uzi wa watu?

Wewe muongo ungeendelea kutupa hii stories si lazima uifanye iwe kama ya kweli.unakuja hapa eti umetapeliwa n.k na umeshauriwa usiandike....au aliyekuwa anaandika sehemu uliyokuwa una copy ameacha?amekushtukia?

Hivi ni lazima kila ukiandika story useme ni ya kweli?sisi wengine tukiwa free tunasoma tu wala si shida si lazima mpaka useme imekutokea.au ulitaka baadaye uaje uanzishe biashara flan hapa.....

Back
Top Bottom