Nimekuta shilingi 100 mbovu kwenye begi la kazini, huu siyo ushirikina?

Hapana mkuu kuwa na amani kabisa. Naomba kujua kama hilo begi ulinunua mtumba au jipya kabisa.
1. Kama ni mtumba kuna uwezekano muuzaji au mteja alipokua analitazama alidondosha hiyo senti bila yeye kujua.
2.Kama ni jipya basi kuna mawili
(a) Watu unaokaa nao kama ni mke au mume, watoto au dada wa kazi katika harakati zao au michezo ghafla wakaweka au kutupia.
(b)Kwa asilimia chache sana amini katika hayo mambo unayofikiria ambayo kuyakabiri inapaswa kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kwani nguvu za giza au shiriki hyo haitakua na nguvu kabisa.
 
Wahi kwa mganga Mkuu kuna mti atakuwa anajaribu KUKUROGA 🤣🤣🤣🤣
Sijawahi kuweka hela, kwenye begi hilo, nikiwa katika harakati za kulifua nikakuta shilingi mia yenye kutu, imetoka wapi? Begi nalifua kila week end na huwa siweki hela humo na sijawahi kupokea hela mbovu kiasi kile ndani ya wiki hii, wajuvi mnijuze sijawekewa na wenzangu kama chuma ulete au kulostishana jamani.
 
Lazia bint Sultan, kwa nini uwe na hofu ya kurogwa na si vyengine? kwa nini usiwe na dhana kuna siku ulinunua kitu kwa 400/= na ulirejeshewa balance 100/= na kwa kuwa ulikuwa busy hukuiweka hiyo coin ya 100/= kwenye pochi badala yake ukaona bora uitupie kwenye begi lako la kazini? hebu weka dhana njema juu yako mwenyewe acha kuwa hasi hata kwako mwenyewe.
Lakini pia kama wewe ni mtu wa imani kama yangu (Muslim) amini kuwa Halikupati lenye kukupata ila tayari ilikwisha kadiriwa likupate hata walimwengu woote tuwe upande wako ili lisikupate ni lazima likupate, na pia halikukosi lenye kukukosa ila tayari ilikwisha kadiriwa likupate hata walimwengu tungekaa upande wa pili ulipate usingekupata, amini hivyo kalamu imeandika na wino ushakauka.
Mtegemee mola wako kwa kila hatua achana na dhana potofu.
Ni kweli uchawi upo lakini haudhuru ila iwe imekadiriwa wewe udhurike na huo uchawi, maana yake uchawi kama uchawi hauna nguvu wala maana yoyote ila ni makadirio ya muumba ndiyo yanayofanya kazi.
 
Umenitafakarisha, Asante.
 
Aliyeweka hiyo sarafu mbovu ni demu wako uliyemla juzi kati anataka awe na access na pesa yako yote.
Jiangalie.!
 
Kama unafanya ofisi zenye fursa za hapa na pale, ushirikina ni mkubwa sana.

Jipange! Umetupiwa mkosi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom