Nimekuta picha mtandaoni nahisi ni mpenzi wangu

Daktari wa Meno

JF-Expert Member
Sep 5, 2019
509
1,610
Takriban miezi 6 sasa natumia Telegram kwa ajili ya masuala fulani ila baada ya kujiunga nilitumiwa link na mshikaji wangu nami nikajiunga kwenye group moja la najua mnaelewa.

Sasa nikawa napata material ya lile group (videos na pictures) ila wiki moja sasa imepita nimeona picha ambazo hadi sasa zimenipa maswali mengi sana. Kuna siku nakumbuka alinipigia simu kuwa anaenda kwa shangazi yake ila alidai atalala huko. Ilifika usiku nikajaribu kumtafuta hakuwa hewani na wala WhatsApp hapatikani. Ila mchana tulikuwa tumewasiliana na akaniaga kuwa anaenda huko kwa Aunt yake japo sikujua alivaa vipi.

Sasa kuna picha nimeziona nimehisi ni yeye kwani nguo ambazo zinaonekana kwenye picha zile asilimia zaidi ya 70 naamini ni zake pia na nguo ya nani niliona ni yake kabisa. Nimehifadhi zile picha ila nakosa njia sahihi ya kumuuliza kama ni zake ama lah.

Naombeni ushauri jamaa zangu nifanye nini ili kukabiliana na hili, je nimuulize au niendelee na uchunguzi hadi nikibaini ukweli bila kumuuliza.

Nipo njia panda.
 
Utateseka mpaka lini? Ukimuuliza atakubali? Kama unampenda na huwezi kumuacha futa hizo picha. Kama humpendi usimuulize futa picha mwambie kuwa huwezi kuwa nae kwasababu Mimi mjomba wako na ndugu tumekutafutia mchumba mwingine.

Ukimpekua kuku humli na ukitaka kula na kipofu usimguse mkono lakini hao wa mitandaoni ni kama jiko la shamba tu.
 
Takriban miezi 6 sasa natumia Telegram kwa ajili ya masuala fulani ila baada ya kujiunga nilitumiwa link na mshikaji wangu nami nikajiunga kwenye group moja la najua mnaelewa.

Sasa nikawa napata material ya lile group (videos na pictures) ila wiki moja sasa imepita nimeona picha ambazo hadi sasa zimenipa maswali mengi sana. Kuna siku nakumbuka alinipigia simu kuwa anaenda kwa shangazi yake ila alidai atalala huko. Ilifika usiku nikajaribu kumtafuta hakuwa hewani na wala WhatsApp hapatikani. Ila mchana tulikuwa tumewasiliana na akaniaga kuwa anaenda huko kwa Aunt yake japo sikujua alivaa vipi.

Sasa kuna picha nimeziona nimehisi ni yeye kwani nguo ambazo zinaonekana kwenye picha zile asilimia zaidi ya 70 naamini ni zake pia na nguo ya nani niliona ni yake kabisa. Nimehifadhi zile picha ila nakosa njia sahihi ya kumuuliza kama ni zake ama lah. Naombeni ushauri jamaa zangu nifanye nini ili kukabiliana na hili, je nimuulize au niendelee na uchunguzi hadi nikibaini ukweli bila kumuuliza.

Nipo njia panda.

IMG_1277.JPG

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom