Nimekuta jina limeseviwa "lv'' kwenye simu ya mke wangu.

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
4,143
5,609
Habari wanajamvi,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, katika harakati za kuipekua simu ya mke wangu nikakuta jina limeseviwa ''lv" , na tunajua msimamizi wa mke ni mumewe, so kuchunguza kila linaloendelea ni lazima kwa mkewe. Je hili ni neno ama herufi ?, manake ukitaka kulitafsiri kwa lugha ya malkia utapata maana nyingi sana , linamaanisha nini haswa?
Karibuni wadau bila kuchafua hali ya hewa.
 
Huwa wanamaanisha 'love' mkuu, ila nadhan isikupe shida vitu vidogo sana hivi.
Note: usipende sana kuipekua simu ya mke wako utapata stress, Jiamini.
 
NA wewe tafuta namba mojawapo save kabisa"LOVE " Halafu kausha mpe simu yako ashinde nayo akija kukuuliza na ww uliza nani amemsave lv...jibu atakwambia shoga yake....mbwa kala mbwa acha pressure
 
Habari wanajamvi,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, katika harakati za kuipekua simu ya mke wangu nikakuta jina limeseviwa ''lv" , na tunajua msimamizi wa mke ni mumewe, so kuchunguza kila linaloendelea ni lazima kwa mkewe. Je hili ni neno ama herufi ?, manake ukitaka kulitafsiri kwa lugha ya malkia utapata maana nyingi sana , linamaanisha nini haswa?
Karibuni wadau bila kuchafua hali ya hewa.
Ungemuuliza mkewe hilo neno alimaanisha nn alivyoliserve usilifafanue ujuavyo ww wakati hujui mhusika alimaanisha nn. Au piga no hiyo ujue ni ya nani
 
Back
Top Bottom