nimekuta acc YANGA nyeupe na ntaiacha nyeupe;-mwalusako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nimekuta acc YANGA nyeupe na ntaiacha nyeupe;-mwalusako

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Nov 9, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  TUHUMA za matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 100 ndani ya klabu ya Yanga zimechukua sura mpya baada ya katibu mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako kueleza kuwa alikuta fedha kidogo kwenye akaunti ikilinganishwa na zile zinazodaiwa kufujwa.

  Mwalusako ambaye hakutaka kukiri kufujwa kwa fedha hizo au la, alieleza kushangazwa na ufujaji huo wa fedha na kutaka suala hilo aulizwe aliyekuwa katibu mkuu , Lucas Kisasa kwa kuwa ndiye anayehusika moja kwa moja.

  "Tangu niingie madarakani kila kitu kinakwenda sawa, ila hizo fedha mimi sikuzikuta ,sijui chochote kuhusu hilo kama zilikuwepo au la.

  Kisasa ndiye aliyekuwa mtendaji ni vema akaulizwa yeye, ninatumaini atakuwa na majibu ya kutosha kuhusu fedha hizo.

  "Kimsingi, mimi siwezi kujua undani suala hilo kwa sababu klabu pia ina matumizi yake ya hapa na pale, hivyo ukimtafuata (Kisasa), bila shaka utapata ufafanuzi wa kutosha,"alisema Mwalusako.

  Hata hivyo, Kisasa alipotafutwa kwa simu zake mbili za mkononi, hazikuwa na majibu zaidi ya kuita bila kupokewa.

  Mwalusako, kwa upande wake aliongeza kuwa ni kweli wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wamekuwa wakitoa michango yao kila kukicha, lakini hadhani kwamba michango kama inaweza kufikia kiasi kilichotajwa.

  Alisema kuwa yeye ni katibu wa kuajiriwa ambaye anafanya kazi kwa misingi ya katiba ya klabu ya Yanga na kwa kuifuata maelekezo ya kamati ya utendaji, hivyo hana shaka kwamba kila kitu kinaenda sawa tangu alipotwaa madaraka.

  "Mimi ni katibu wa kuajiriwa wa klabu ya Yanga nafanya kazi kwa kufuata katiba iliyopo na pia kupokea maelekezo kutoka kamati ya utendaji, sasa katika hilo sina shaka hata kidogo kwamba kila kitu kinakwenda sawa tangu nilipoingia madarakani,"alisema.

  Jana, Mwananchi iliripoti kwa mara ya kwanza tuhuma za baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuutaka uongozi wa klabu yao chini ya mwenyekiti, Imani Madega kuweza wazi kuhusu fedha za malipo ya kadi za unachama zinazodaiwa kufikia mlioni 100.
  Hata hivyo, Madega aliiambia Mwananchi kuwa ni majungu ambayo yamekuwa yakienezwa kwa lengo la kuonyesha kuwa uongozi wake umetumia vibaya fedha za ada ya uanachama wa klabu hiyo.
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Yale yale, ufisadi kila sehemu!!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280

  we acha tu mkuu kila sehemu...jamani mmhhhhhhhhhh
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nimesikia madega anataka kugombea ubunge so nadhani atakuwa amechota za kampeni
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  aisee unajua wana YANGA awakumjua aliposema mi naona niondoke kabla ya muda laiti kungekuwa na auditing kwenye uongozi wa michzo najua madega angemfwaata LYUMBA segadance.....
   
 6. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kula uwache kama ulivyokuta kweupe? Manji si yupo ataleta zingine za EPA.
  pesa nyingi sana amekula madega kiasi kwamba amenona kama anapuliza moto -shavu hilo.Chalize msimpe ubunge huyu hana maana -taarifa si ndio hizo tunataka nini tena.
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Only in bongo can someone declare publicly and proudly that he hasn't done anything to elevate the financial situation of a club he was responsible for leading. He seems to display a high degree of acceptance of the "fact" that he is not in the know.

  Sasa ukatibu mkuu maana yake nini?

  Good for nothing unashamed loser.
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  .......nilijua yataibuka tu...hasa baada ya kuwadunda...ha!ha!ha!aaa
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha! Mnyama Kazua Jambo Jangwani, yaani club ina uwanja inakosa hata Milioni moja kwenye acount LoLi! Haturudii tena kuwakandamiza
   
Loading...