Nimekumbuka hii nikacheka sana; tuliowahi kukojoza kitandani tukiwa boarding njooni tutor ushuhuda

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
4,575
2,000
Wakuu Kwema!

Leo Taikon nimekumbuka Maswahibu yaliyonikuta nikiwa Advance huko Matema Beach High School, Kyela mkoani Mbeya.

Taikon ni mtu wa Stori, mjanja mjanja, mcheshi, na mtu wa watu. Taikon ni mtu anayeongea na kila mtu. Hapendi mtu akwazike.

Siku zile nikafika shuleni, Kyela ikiwa ndio mara yangu ya Kwanza kabisa kufika Mkoani Mbeya.
Maisha Mapya yakaanza, nilifika kipindi cha baridi, ilikuwa mwezi wa tano, weeh! Kulikuwa na winter sio mchezo, kumbuka Mimi nimezaliwa na kukulia Makanya, huko Same ambapo Hali yake ya hewa ni joto Kali na jua linachoma mno. Hivyo ni Halali yangu kuona Hali ya hewa ya Kyela kuwa ya baridi na yenye kunikera.

Kwa Wale VIKOJOZI wote watakubaliana na Mimi kuwa hakuna kipindi kigumu kwao Kama msimu wa baridi, huwezi tenganisha msimu wa baridi na VIKOJOZI. Vikojozi wanaogopa na hawapendi msimu wa baridi kwani mfumo wa kukojoa hufanya kazi zaidi kuliko mfumo wa utoaji jasho.

Basi Taikon nikiwa tayari nimeshazoea mazingira, kijana msafi na mcheshi ambaye nilipenda Sana Stori za hapa na pale kwenye vijiwe au kutembelewa kwenye Cube/Room yetu na watu kuja kunisikiliza Stori zangu za uongo na kweli.

Siku hiyo isiyo na jina, nikawa nimelala, nikaota ndoto ya hovyo Sana.
Vikojozi watakubaliana na Mimi kuwa ili wakojoe yawapasa kuota ndoto aidha ya kutisha wanakimbizwa na majoka, au wanyama wakali au wanaota ndoto ya kujisaidia haja ndogo kumbe ndio wanalishusha kweli😎😎

Baada ya kuota ndoto Ile, nikashtuka. Maya weee! Nilikuwa nimekojoa tena mkojo ndio ulikuwa unamalizikiaπŸ˜ͺπŸ˜ͺπŸ˜ͺ
Ulikuwa wamoto kweli, nikapapasa kitandani, Doooh! Jamani! Jamani! Nilikuwa limelishusha kojo jingi mno, bado lilikuwa linaelea kitandani kutokana na kuwa Godoro sikutoa lile nailoni.

Mashuka na blanket yalikuwa tepe tepe!😫😫
Sasa nikafikiri nifanyejeπŸ€”πŸ€”πŸ€” Kojo ndio Hilo, nimeshakiharibu. Nikacheka saa ilikuwa saa tisa inaelekea saa kumi usiku hiyo.

Nikatulia tuli kusikilizia movement yoyote ndani ya lile bweni, nikaona kimya, nikachungulia dirishani nikaona pametulia mpaka Kule madarasani.

Nikatoka kitandani na kutoka nje kukagua Mandhari, nikaona Hali ni shwari. Upesi upesi nikarudi nikafungasha Yale mashuka na blanket nikayachukua kuyapeleka Bafuni. Nikafanikiwa kuyaweka kwenye beseni, na kuyaloweka kwenye maji. πŸ€—πŸ€—

Nikarudi kuchukua sabuni ya unga, mambo hayo yanafanyika haraka haraka WazeeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, sitaki kukutwa na yeyeto.
Basi nikiwa narudi nikapishana na mshikaji mmoja Kidato cha sita.

Nilihakikisha hanipitii karibu si unajua sijabadili nguo bado, yaani nimelowa mamikojoπŸ˜‚πŸ˜‚ na ninanuka kweli. Nikafanikiwa kumpita, naye alikuwa anaenda chooni, aliponipita nikamgeukia yeye akiwa anaendelea kwenda chooni asijue namtazama, nikasema watu wengine nao, kuamka amka kila saa🀣🀣🀣 yaani nilikuwa na gubu kweli.

Nikabadili nguo nilizokuwa nimevaa nilizozikojolea, nikavaa zingine. Nikachukua Sabuni ya unga, nikawa namsubiri yule jamaa arudi ili niendelee na mishe zangu.

Dakika zinaenda naona harudi, kucheki saa imeingia saa kumi za usiku. Na hapo watakaoamka wataongezeka kujifanya wanapenda kusoma😏😏😏,
Nikaziwe zile nguo kwenye mfuko na Ile sabuni nikatoka nazo, muda huu nikiwa na tahadhari kwani najua Yule kijana yupo Uani.

Nafika namkuta anaongea na simu, Saa kumi hiyo, alikuwa anaongea kikurya. Aliponiona akashtuka, pia akashangaa ule mfuko nilioubeba. Mimi sikumjali Sana nikaingia upande wa pili wa bafu, Kwa waliosoma Matema Beach watakubaliana na Mimi kuwa Bafu la chini lilikuwa kubwa mno.

Nikatoka tena, nikaenda kuchukua Redio ili nimkere Yule jamaa aondoke nifanye shughuli zangu Kwa UhuruπŸ˜›πŸ˜›πŸ˜› nikarudi nikiwa na Redio, nikaiwasha. Nikaweka mziki mkubwa.
Hila yangu ikafanikiwa, akaondoka.

Nikatoka zile nguo nikaziloweka na kuzisuuza pamoja na Yale mashuka na blanket Kwa Sabuni.
Sikutaka kuyafua nilikuwa nafanya hima ili nisikutwe na mtu mwingine. Nikamwaga maji, nikasuuza mara tatu mpaka harufu ya Kojo ilipotoka. Kisha nikaziacha nimeziloweka.

Muda wote nafanya hayo nilikuwa namuomba Mungu nisiaibike WalahiπŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‚
Yaani ndio Kwanza nimeingia hata miezi miwili sina naangusha Kojo, nitaishije Mimi na ninavyopenda kutania watu🀣🀣🀣.

Nikafanikiwa, nikarudi Bwenini, sasa Ile Cube/Room yote ilikuwa na harufu ya miikojo licha ya Kupunguza manguo yenye mikojo.
Nikatandika shuka jingine nikafunguq dirisha hewa iingie japo kulikuwa na baridi Sana lakini Bora baridi kuliko Fedheha 😊😊😊
Nikatoka perfume nikapuliza kitandani kisha nakupuliza hewaniπŸ˜‚πŸ˜‚ baada ya Nusu saa, Wanafunzi wa kiislam wakaanza kuamka kama unavyojua. Hata hivyo hawakuwa na athari.
Taikon miguu juu ninatathmini tukio zima namna lilivyoenda.

Wenzangu kwenye Ile room walikuwa wakikoroma mno na hiyo ndiyo nafuu yangu.
Awali mikoromo Yao ilikuwa kero kubwa kwangu siku za nyuma, Ila Kwa siku Ile ilinipa daraja kubwa, niliiona Kama mziki mzuri wa USHINDI🀣🀣🀣 kwani nilikuwa najua Kwa kukoroma Kule hakuna mwenye afadhali, wote walikuwa kwenye usingizi mzito ambao hata ningeamua kuwahamisha kitanda ningeweza.

Kulikucha!

Nikiwa wakwanza kuondoka eneo la tukio kwenda darasaniπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ kuepusha hatari yoyote ya ishu kubumbuluka.
Wiki Ile sikushinda Room yangu tofauti na siku za nyuma ambapo room yangu ndio ilikuwa kijiwe kikuu cha Stori na Mimi ndiye Host😎😎
Nilikuwa nakuja Kwa kuchelewa mida ya saa nne tena kuja kulala tuuπŸ˜€πŸ˜€

Lengo lilikuwa ni kuyapa mazingira ya kitanda changu muda wa ku-recover yarudie Hali ya awali, harufu iondoke kabisa

Nilifanikiwa, na hakuna aliyewahi kunshtukia.

Nilimshukuru Mungu Sana.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Je wewe ulifanyaje siku uliyoangusha Kojo?
Tiririka chini.

Taikon wa Fasihi.
Mshusha Kojo
Kwa sasa, Mikumi.
0693322309
 
Jemima Mrembo

Member
Jul 19, 2021
88
150

Lo, nyie ndio mkiingiza TU, mmekojoa, halafu haisomami Tena hadi kesho
 
Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
3,120
2,000
Na mimi ilinitokea bwana. Nikiwa kidato cha sita kwenye shule moja maarufu na kongwe huko Arusha. Kitanda kilikuwa cha deka. Bahati nzuri nilikuwa nalala kitanda cha chini. Sijui ingekuwaje kama ningekuwa nalala kitanda cha juu. Ningepata aibu na fedheha kubwa sana.

Basi bwana usiku wa manane nikajisikia kukojoa nikiwa usingizini. Wakati najiandaa kuamka ili niende msalani kukoja, lahaula!! kumbe ndio mkojo unamalizika. Kigodoro chembamba na karatasi ya nailoni ilishachanika siku nyingi, hivyo mkojo wa kutosha ukamwagika sakafuni.

Basi kwa haraka sana ya kiaskari, nikachukuwa taulo na kukausha godoro na kupiga deki na kuhakikisha siachi alama yoyote. Wakati huo wote wanafunzi wenzangu wanakoroma kwa usingizi mzito, hiyo ikawa pona yangu ya kutokugundulika.

Nichakuwa taulo langu na shuka na kwenda bafuni kufua na kuanika chapuchapu na kurudi kuendela kulala (kulalia upande wa godoro ambao haujaloana).
Kulipokucha maisha yakaendelea. Bahati nzuri yule mwenzangu aliyekuwa ana lala kitanda cha juu, hakuwa na mazoea ya kukaa kitandani kwangu wakati wa mapumziko. Mara nyingi hata tukiwa bwenini wakati wa mapumziko alikuwa anapanda kitandani kwake na kukaa huko juu. Hivyo nilipona siri yangu haikujulikana.

Naomba Nawasilisha ROBERT HERIEL
 
Black belts

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
2,236
2,000
Dah,nimecheka, Mimi nilikuwa nakojoa kitandani mpk nikiwa na miaka 12 mwaka 1988,

nilikoma kukojoa kitandani baada ya marehemu sister kunipigisha "kindumbwe ndumbwe chaliaaaaa" maeneo ya morogoro mitaa Ya Karume street Hadi uhuru street kwa kina Mabukila na kina Abeid mziba, kumalizikia mlapakoro street Hadi boma road kote,
Baada ya fedhea hiyo nikaacha na kukojoa kitandani
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,824
2,000
Na leo ukilala utaota jiandae mapema kuvaa pampasi.

Note. Nimekusoma huku nacheka tu mpaka machozi.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,259
2,000
Dah! Mimi ndiyo nimekojoa kitandani kuanzia nikiwa mdogo mpaka nikiwa primary, pre form one, na form one kabisa! πŸ™„ Mbaya zaidi nilisoma boarding! Tena Seminary!! Nilifedheheka sana kwa kweli!! 😨
Namshukuru Mungu tu watoto wangu wote wawili, hawajarithi kabisa huu upuuzi wa baba yao! πŸ˜ͺ

Na kiukweli credit zote ziende kwa yule Mzee Sheki......! (RIP) ambaye alikuwa ni Mganga wa jadi na bingwa wa miti shamba! πŸ™

Baada ya kutaka kuacha shule kwa sababu ya aibu (Maana nilikuwa ni bonge la Handsome, nikapewa cheo kizuri tu pale shuleni! Nilikuwa beki no. 5 kisiki! Wa kiwango cha Nadir Haroub Cannavaro wa Yanga), halafu ikifika usiku, ni kuota tu ndoto niko sehemu salama kabisa ya kujisaidia!! 😁😁Mzee nalimwaga tu la kutosha!😁😁😁 Ile namaliza tu, 🀭 tayari nishaharibu!πŸ₯΅ Dah!! Hali ile iliniathiri sana!!

Aisee yule Mzee alinipa dawa ya kutumia kwa wiki 2 ya mitishamba! Na akasema baada ya hapo, kama sitapona basi nirudi tena! (Bro ndiye aliyenipeleka baada ya kumwambia ukweli)! Nilipomaliza tu zile dawa (zilikuwa ni za kunywa na kujifukiza), hakika na ule ugonjwa uliisha kabisa. Na mpaka leo sijawahi kupitiwa hata kwa bahati mbaya. πŸ€—
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
4,575
2,000
Na mimi ilinitokea bwana. Nikiwa kidato cha sita kwenye shule moja maarufu na kongwe huko Arusha. Kitanda kilikuwa cha deka. Bahati nzuri nilikuwa nalala kitanda cha chini. Sijui ingekuwaje kama ningekuwa nalala kitanda cha juu. Ningepata aibu na fedheha kubwa sana.

Basi bwana usiku wa manane nikajisikia kukojoa nikiwa usingizini. Wakati najiandaa kuamka ili niende msalani kukoja, lahaula!! kumbe ndio mkojo unamalizika. Kigodoro chembamba na karatasi ya nailoni ilishachanika siku nyingi, hivyo mkojo wa kutosha ukamwagika sakafuni.

Basi kwa haraka sana ya kiaskari, nikachukuwa taulo na kukausha godoro na kupiga deki na kuhakikisha siachi alama yoyote. Wakati huo wote wanafunzi wenzangu wanakoroma kwa usingizi mzito, hiyo ikawa pona yangu ya kutokugundulika.

Nichakuwa taulo langu na shuka na kwenda bafuni kufua na kuanika chapuchapu na kurudi kuendela kulala (kulalia upande wa godoro ambao haujaloana).
Kulipokucha maisha yakaendelea. Bahati nzuri yule mwenzangu aliyekuwa ana lala kitanda cha juu, hakuwa na mazoea ya kukaa kitandani kwangu wakati wa mapumziko. Mara nyingi hata tukiwa bwenini wakati wa mapumziko alikuwa anapanda kitandani kwake na kukaa huko juu. Hivyo nilipona siri yangu haikujulikana.

Naomba Nawasilisha ROBERT HERIEL

🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
4,575
2,000
Dah! Mimi ndiyo nimekojoa kitandani kuanzia nikiwa mdogo mpaka nikiwa primary, pre form one, na form one kabisa! πŸ™„ Mbaya zaidi nilisoma boarding! Tena Seminary!! Nilifedheheka sana kwa kweli!! 😨
Namshukuru Mungu tu watoto wangu wote wawili, hawajarithi kabisa huu upuuzi wa baba yao! πŸ˜ͺ

Na kiukweli credit zote ziende kwa yule Mzee Sheki......! (RIP) ambaye alikuwa ni Mganga wa jadi na bingwa wa miti shamba! πŸ™

Baada ya kutaka kuacha shule kwa sababu ya aibu (Maana nilikuwa ni bonge la Handsome, nikapewa cheo kizuri tu pale shuleni! Nilikuwa beki no. 5 kisiki! Wa kiwango cha Nadir Haroub Cannavaro wa Yanga), halafu ikifika usiku, ni kuota tu ndoto niko sehemu salama kabisa ya kujisaidia!! 😁😁Mzee nalimwaga tu la kutosha!😁😁😁 Ile namaliza tu, 🀭 tayari nishaharibu!πŸ₯΅ Dah!! Hali ile iliniathiri sana!!

Aisee yule Mzee alinipa dawa ya kutumia kwa wiki 2 ya mitishamba! Na akasema baada ya hapo, kama sitapona basi nirudi tena! (Bro ndiye aliyenipeleka baada ya kumwambia ukweli)! Nilipomaliza tu zile dawa (zilikuwa ni za kunywa na kujifukiza), hakika na ule ugonjwa uliisha kabisa. Na mpaka leo sijawahi kupitiwa hata kwa bahati mbaya. πŸ€—Hii usiombe ikutokee ugenini, utaita maji mma
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom