Nimekubali Tanzania Kuna chuki kubwa, upo umezekano tunauana kimya kimya

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nimemsikiliza Mwingira, nimemsikiliza Nape,nikamsiliza WA zamani wa Jumuhia ya wazazi wa CCM, nimemsikiliza huyu mzee mwanajeshi mstaafu kiongozi wa organizashen ya mambo ya nje, nikamsikiliza Gwajima, nikaona ushahidi wa Makomandoo, nikaona namna sabaya alivyotesa, Makonda alivyotesa, Muro alivyoshughulikia watu, nikatafakari korosho mtwara,gesi, madini ,wamachinga, watumishi hewa, wastaafu nk naomba niseme kwamba Tanzania watu wana chuki ila wanachekeana.
Tunaweza kuuana tukichekeana, maridhiano na toba ya kitaifa ni muhimu KULIKO kauli mbiu ya kazi iendelee. Kazi ikiendelea ni pamoja na kazi za kihalifu so tuseme wazi kwamba ni muda wakuliponya Taifa. Kama Mwingira ambaye mke wake alikuwa DC Nyamagana aliwindwa kufa Nani yupo salama? Kwamba wanampa madaraka mkeo then wewe wanakusukia njama kuua na ukae Kimya Hadi wachukuliwe na Mungu? Wasipochukuliwa wataua wangapi?

Tunaweza dhani TU maendeleo kumbe tunapoteza muda
 
Labda ueleze ni kundi lipi linaweza ua au kuuana.
Tuonavyo ni vurugu za ccm kwa maccm.
 
Hilo liko wazi , Watanzania wengi hawana amani moyoni mwao wana waza maumivu mengi wanayo fanyiana .

Chuki kati ya vyama vya siasa vilivyo nje ya madalaka na chama kinacho ongoza.
Chuki kati ya polisi na wananchi
Chuki kati ya Wazanzibar na wabala
Chuki kati ya watawala na warawaliwa kwa ujumla
Chuki kati ya Kanda moja na Kanda zingine


Chanzo Cha chuki zote ni utawala usio zingatia haki na usawa kwa wote.
 
CCM haijawahi kuwapenda raia zaidi ya kujenga chuki,
Kazi kubwa iliyokuwa inafanuwa na awamu ya tano ni kuwinda wasema ukweli
 
Ila Kuna kitu nime note hapa, kazi iendelee , hii kauli mbiu inabidi mama aibadilishe, isije ikawa imewapa confidence mpaka wakaamua kufungua kesi ya ugaidi kwa mwenye kiti wa Chadema.
 
SIJAIJUA POINTI YA MTOA MADA

UNAAMBIWA HAKUNA NCHI RAHISI KUONGOZA KAMA NCHI AMBAYO RAIA WAKE HAWAJITAMBUI
Hata mimi...Yeye mwenyewe anaonyesha ana chuki zake so anataka sote tuwe na chuki kama yake
 
Back
Top Bottom