Nimekubali Ndoa Ni Ngumu Kwa Wote, Japo Ni Raha Pia, Unasemaje?

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,348
559
nimeiona hii kutoka kwenye blog moja nikaona tuijadili hapa.

SIFA ZA MWANAMKE (SIFA NJEMA)
1. Awe mwema
2. Mwenye hekima
3. Mwenye adabu
4. Mwenye busara
5. Awe mkarimu
6. Msafi (mwili na nyumba)
7. Mpole
8. Mwenye huruma
9. Mdadisi
10. Mvumilivu
11. Mcheshi (kiasi)Yampasa mke aanze siku kwa kauli nzuri hata kama anaumwa:-- Amsalimie mume

- Amwage mumewe akimtakia kazi njema baada ya kumuandalia
(a) Maji ya kuoga
(b) Kifungua kinywa
(c) Nguo za kuvaa siku hiyo

Mume atokapo kazini:-
(a) Mkaribishe kwa tabasamu, mkaribishe kwa furaha.
(b) Mpigipige mgongoni
(c) Vaa nguo nzuri (mwanaume hupenda anachoona) macho huvutiwa kwa kuona
(d) Waeleze watoto wako unavyompenda baba yao ( watoto nao watawapenda wote)
(e) Kila mmoja wenu ajue kile anachopenda ua anachotaka

ILI KUMHESHIMU MUME
1. Muombee kila siku - Yeye alivyo hekima, busara, ulinzi, baraka, ujuzi, uelewa, kiroho, mafanikio, kushinda majaribu nk - angalia na tarajia majibu ya maombi - Mshukuru Mungu kwa kazi anayofanya kwa familia yako - Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mume wako- ombea mtazamo wako.
2. Kumbuka Mungu amemuweka mume wako kuwa kiongozi wa nyumba yako pamoja na wewe.
3. Angalia sifa za mumeo na uzikubali na ongeza mara kwa mara
4. Mwambie mumeo ni namna gani unamfurahia na kumpenda
5. Usitoe sifa zake mbaya mbele za watu au kubisha
6. Mtie moyo na kuwa msaaada wakati wa jambo gumuJihadhari na jinsi unavyomuuliza maswali
7. Changamkia pale anapoonesha upendo
8. Fikiria mambo mazuri juu ya mumeo
9. Thamini vitu anavyovipenda na asivyovipenda Mith 12:4

KAWAIDA MWANAMKE

1. Usitegemee starehe nyingi kama zile ulizokuwa unapata kwa wazazi wako au ndugu zako
2. Utakuwa na juhudi katika kujenga nyumba ya mume wako uliye naye.
3. Hutakuwa mgomvi na mchokozi wala kumpiga mumeo kwa mwiko
4. Utampa mume wako haki yake
5. Thamani ya mumeo ni zaidi ya wanaume wote.
6. Umtii mumeo kwa Roho ya upole na unyenyekevu
7. Usimuruhusu mtu yeyote atambue kwamba unao wakati mgumu ( siri za ndani zisitoke nje)
8. Utahaakikisha macho yako yanamwangalia mumeo wakati amevaa kabla ya kutoka kwenda kazini au kutembea
9. Utajitoa na kumtii mumeo kwa moyo wote na kumruhusu kuwa kichwa cha nyumba
10. Utahakikisha mumeo ni bora kuliko watu wengine
11. Mwanaume ni dereva wa gari la ndoa na mwanamke anaweza akashauri na kupednekeza njia ya kupita na siyo kunyang'anya usukani

SIFA ZA MWANAUME
1. Mpole
2. Asiwe mwepesi wa hasira
3. Mcheshi
4. Anayeshaurika
5. Anayewajali watu wa nyumbani mwake (mahitaji)
6. Aliye na shukurani na kusifu (kwa lolote jema alilolitenda mkewe)
7. Anayeaga aondokapo kwenda matembezini au kazini au popote.

10. WAJIBU WA WA MUME KWA MKEWE

1. KUPENDA - matatizo mengi hutokea kwa sababu watu hawajui maana na jinsi ya kupenda kupenda ni matendo (action) siyo kujisikia au kuhisi ni kufanya vitu vizuri kama vile kutoa, kutabasamu, kusamehe

KIONGOZI (KICHWA) MTAWALA
- Mume ni kichwa cha mke

MLINZI WA MKEWE
- Mke hujiona salama awapo na mumewe. Hivyo mume mlinde mkeo na maadui wa ndani na nje kama vile baba na mama, mashemeji/mawifi na marafik

4. KUTUNZA FAMILIA.
Kuhakiki familia inapata chakula cha kutosha, malazi, mavazi na elimu kwa watoto

KUMPAMBA MKEWE - mume sharti ampambe mkewe apendeze ili aweze kuvutia (amununulie vipodozi, nguo nk)

KAWAIDA MWANAUME:
1. Utamheshimu mke wako kama mrithi
2. Mke wako ni mtu wa kwanza kwako siyo ndugu zako wala rafiki zako
4. Mara kwa mara utamwambia mke wako alivyo wa muhimu na thamani kwako
5. Utaendelea kumpenda kwa upendo ule wa kwanza wa wakati unampata.
6. Utakuwa kiongozi wa kusimamia nidhamu ya nyumba yako ukisaidiwa na mke wako.
7. Utakumbuka kutekeleza au kutimiza vile vitu vidogo ambavyo ulimwahidi mke wako kwamba utafanya
8. Macho yako yataelekea kwa mke wako tu na sivinginevyo.
9. Utafanya juhudi kusikiliza yale yaliyosemwa na mke wako.
10. Utambusu kila siku asubuhi kwa upendo.
11. Hutakuwa mchungu likija swala la fedha.

12. WAJIBU WA MKE KWA MUMEWE KUTII
- Kutii kunakosemwa hapa ni kuwa endapo wawili mume na mke mmeshindwa kufikia uamuzi wa pamoja, basi,basi mke atatii uamuzi wa mumewe kama vile wamekubaliana awali

KULEA WATOTO (FAMILIA)
(a) Kuhakikisha afya ya mumeo na watoto
(b) Kuhakikisha kuwa chakula kinaliwa kwa wakati na kizuri
(c) Kuhakikisha usafi wa malazi, mavazi na miili yao
(d) Kufundisha watoto maneno ya Mungu
(e) Kuchunguza nyendo na tabia za watoto na mumeo na kuchukua tahadhari mapema.

KUMSHAURI MUMEO
Mke mwenye busara ni mshauri mwema kwa mumewe. Hatatoa ushauri wa kuleta maangamizi. Ushauri unafaa lakini ushauri mwingine upimwe kabla ya kufanyia kazi.

13. ADUI WA NDOA NI:-
UTAJIRI - Tajiri hupendwa na wasichana na pia huwa na tamaa ya kutafuta fedha kiasi cha kukosa muda na mkewe

UMASKINI - kazi ya kutafuta lishe ni ya baba, hivyo hushughulika sana na kujikuta amekuwa baba zaidi kuliko kuwa mume

MADARAKA - madaraka ya ofisini huyaleta hadi nyumbanini chukuzo kwa mume/mke. Maafisa hawana muda na wake zao kwa sababu ya makongamano/semina/ziara mbalimbali.- Hivyo wake zao wengi hutumia madereva kukidhi haja zao za kimwili- Mke ambaye ni ofisa humwachia house girl kazi za kupika, kufagia chumbani, kupeleka maji bafuni na hata kutandika kitanda, hivyo kusababisha mke kupinduliwa na house girl.

MAMBO YANAYOWAKERA WAKE

1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
9. Mume kubagua watoto
10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani..
 
hapa naona mwanamke ni mtumwa tu hamna jengine ... umesahau kumfulia nguo zake za ndani hata kama anatoka nje ya ndoa ... kama huna racket ya viatu uiname uvunguni umtolee viatu vyake, umfulie socksi , usimuulize anatoka wapi akirudi usiku ... usimkunjiee uso, umbebe mgongoni, umbembeleze akikasirika hata ukimfumania uwe tayari kukubali makosa yake mwenyewe .. eeeee the list is endless..
Women have to be free siyo kutawaliwa kama kondoo wa Bwana ..........
Naona inabidi you let your patner decide kunyoa au kusuka unamwambia kabisa ukinioa tunagawana kazi ... not mwanamke to do kila kitu even when you are tired or sick unalazimika kumtimizia mume .... no no sikubali
 
Kwa ufupi ndoa ni ngumu sana hasa unapokuwa na mume asiyejali. ila majukumu yote haya kwa wanawake mh. hata mi inanikatisha tamaa
 
Jamani tatizo siku hizi hakuna Ndoa ni pesa tu, si wanawake si wanaume wanaangalia pesa. NDOA, DOA, OA, Aaaah kumbe mambo yenyewe ndio hivi? Maisha ya sasa hata mtu umpe mboni ya jicho lako hakuna cha maana.
 
Is it possible for a woman to do all that while the husband doesn’t care about the family? I mean how can those happen while he does not play his part? Are women created to suffer? Make sure unamfulia, unamnyooshea, unampikia, unatandikia kitanda, akirudi anatupa nguo zake popote uwe unaokota unaweka at the right place, Unalea mtoto, usiku mzima hata kama unaumwa hawezi hata kuchange mtoto napy na kumfeed. Kazini pia wewe unaenda siyo house wife, vilele anataka wewe uchangie budget ya nyumbani tena kwa kiasi kikubwa kuliko yeye, otherwise hata mtoto maziwa anakosa. Ukiumwa utajiju, how you go to hospital he doesn’t care, he doesn’t even ask how you feel, just a simple qn, forget hata matunda hawezi kukununulia ukiwa mgonjwa outing ndio kabisaa it doesn’t exist into his vocabulary. Habari ya nguo na mapambo don’t mention it’s a forbidden word. Sasa kwenye mazingira ya hivi hizi sifa za mwanamke zitapatikana, I mean hata kama alikuwa hivyo mwanzoni ataendelea hivyo kweli? Result ya haya ni chuki, ugonvi(yaani hivi vinadevelop naturally kutokana na situation) Misho unajiuliza whats the point of getting married in the first place. Its adding stress to yourself. Men please don’t do this to your wives. It’s a destruction to marriage.
 
yes, walipoondoa mafunzo ya jando kwa wanaume, basi tena, zile basics za kumtunza mke japo kizamani hazipo, wameishia tu akishaoa mke anaanza kutoa maksi wake za wenzie. Wake hamuoni tena.
 
Haika,
Nakubaliana kabisa kuwa ndoa ni ngumu kwa wote japo ina raha zake pia kwa wote. Ingekuwa hayo yaliyosemwa kwenye hiyo nukuu yako yanazingatiwa na wahusika, basi huenda ambaye hajaoa au kuolewa wangejikuta wanakosa mengi, lakini ndoa nyingi especially za siku hizi mapungufu ni mengi mno, kiasi kwamba kutokuoa au kuolewa ni salama zaidi.
 
TRUE Benoir,
Lakini ni kwa mtu ambaye hajui responsibility yake kama binaadam, kwa binadamu wenzake. yani anajifikiria yeye tu, maadamu keshazaliwa hataki kutoa mchango wake kwa humankind.
look at tha bigger picture. Ni vema kila mtu akajitafutia raha zake binafsi? inatosha kuridhika na nafsi yako tu? je utaridhika kweli?
Kwa kuwa tulivyoumbwa najua, furaha ya mtu inategemea sasa furaha ya watu wanaomzunguka.
 
Sijaelewa mnacholalama maana hamjakiainisha.

If you get married for the wrong reasons, huenda akakufanya zulia au doormat.
Compatibility is one of the key thing. Unaona kabisa maji yana kina kirefu unatumbukia; please, pick the right size.
Oooh "baba mama LOOK, ...nimepata mwenye Masters".

Wanawake ni wataalam wa kujua mume mwema/asiye mwema ni yupi. Sidhani wanaume wana intuition kubwa kuliko wanawake kwenye hili.

Things can be complicated at times though, a woman is easy to convince. Isipokuwa intuition yake iko palepale.

KIONGOZI (KICHWA) MTAWALA
- Mume ni kichwa cha mke

Hili limepigiwa kelele sana. Sasa kuna aliyekuja akaongezea......
Kama Mume ni kichwa, ....Mke ni shingo.

I'm out!

.
 
nimeiona hii kutoka kwenye blog moja nikaona tuijadili hapa..........

SIFA ZA MWANAMKE (SIFA NJEMA)
1. Awe mwema
2. Mwenye hekima
3. Mwenye adabu
4. Mwenye busara
5. Awe mkarimu
6. Msafi (mwili na nyumba)
7. Mpole
8. Mwenye huruma
9. Mdadisi
10. Mvumilivu
11. Mcheshi (kiasi)Yampasa mke aanze siku kwa kauli nzuri hata kama anaumwa:-- Amsalimie mume

- Amwage mumewe akimtakia kazi njema baada ya kumuandalia
(a) Maji ya kuoga
(b) Kifungua kinywa
(c) Nguo za kuvaa siku hiyo

Mume atokapo kazini:-
(a) Mkaribishe kwa tabasamu, mkaribishe kwa furaha.
(b) Mpigipige mgongoni
(c) Vaa nguo nzuri (mwanaume hupenda anachoona) macho huvutiwa kwa kuona
(d) Waeleze watoto wako unavyompenda baba yao ( watoto nao watawapenda wote)
(e) Kila mmoja wenu ajue kile anachopenda ua anachotaka

ILI KUMHESHIMU MUME
1. Muombee kila siku - Yeye alivyo hekima, busara, ulinzi, baraka, ujuzi, uelewa, kiroho, mafanikio, kushinda majaribu nk - angalia na tarajia majibu ya maombi - Mshukuru Mungu kwa kazi anayofanya kwa familia yako - Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mume wako- ombea mtazamo wako.
2. Kumbuka Mungu amemuweka mume wako kuwa kiongozi wa nyumba yako pamoja na wewe.
3. Angalia sifa za mumeo na uzikubali na ongeza mara kwa mara
4. Mwambie mumeo ni namna gani unamfurahia na kumpenda
5. Usitoe sifa zake mbaya mbele za watu au kubisha
6. Mtie moyo na kuwa msaaada wakati wa jambo gumuJihadhari na jinsi unavyomuuliza maswali
7. Changamkia pale anapoonesha upendo
8. Fikiria mambo mazuri juu ya mumeo
9. Thamini vitu anavyovipenda na asivyovipenda Mith 12:4

KAWAIDA MWANAMKE

1. Usitegemee starehe nyingi kama zile ulizokuwa unapata kwa wazazi wako au ndugu zako
2. Utakuwa na juhudi katika kujenga nyumba ya mume wako uliye naye.
3. Hutakuwa mgomvi na mchokozi wala kumpiga mumeo kwa mwiko
4. Utampa mume wako haki yake
5. Thamani ya mumeo ni zaidi ya wanaume wote.
6. Umtii mumeo kwa Roho ya upole na unyenyekevu
7. Usimuruhusu mtu yeyote atambue kwamba unao wakati mgumu ( siri za ndani zisitoke nje)
8. Utahaakikisha macho yako yanamwangalia mumeo wakati amevaa kabla ya kutoka kwenda kazini au kutembea
9. Utajitoa na kumtii mumeo kwa moyo wote na kumruhusu kuwa kichwa cha nyumba
10. Utahakikisha mumeo ni bora kuliko watu wengine
11. Mwanaume ni dereva wa gari la ndoa na mwanamke anaweza akashauri na kupednekeza njia ya kupita na siyo kunyang'anya usukani

SIFA ZA MWANAUME
1. Mpole
2. Asiwe mwepesi wa hasira
3. Mcheshi
4. Anayeshaurika
5. Anayewajali watu wa nyumbani mwake (mahitaji)
6. Aliye na shukurani na kusifu (kwa lolote jema alilolitenda mkewe)
7. Anayeaga aondokapo kwenda matembezini au kazini au popote.

10. WAJIBU WA WA MUME KWA MKEWE

1. KUPENDA - matatizo mengi hutokea kwa sababu watu hawajui maana na jinsi ya kupenda kupenda ni matendo (action) siyo kujisikia au kuhisi ni kufanya vitu vizuri kama vile kutoa, kutabasamu, kusamehe

KIONGOZI (KICHWA) MTAWALA
- Mume ni kichwa cha mke

MLINZI WA MKEWE
- Mke hujiona salama awapo na mumewe. Hivyo mume mlinde mkeo na maadui wa ndani na nje kama vile baba na mama, mashemeji/mawifi na marafik

4. KUTUNZA FAMILIA.
Kuhakiki familia inapata chakula cha kutosha, malazi, mavazi na elimu kwa watoto

KUMPAMBA MKEWE - mume sharti ampambe mkewe apendeze ili aweze kuvutia (amununulie vipodozi, nguo nk)

KAWAIDA MWANAUME:
1. Utamheshimu mke wako kama mrithi
2. Mke wako ni mtu wa kwanza kwako siyo ndugu zako wala rafiki zako
4. Mara kwa mara utamwambia mke wako alivyo wa muhimu na thamani kwako
5. Utaendelea kumpenda kwa upendo ule wa kwanza wa wakati unampata.
6. Utakuwa kiongozi wa kusimamia nidhamu ya nyumba yako ukisaidiwa na mke wako.
7. Utakumbuka kutekeleza au kutimiza vile vitu vidogo ambavyo ulimwahidi mke wako kwamba utafanya
8. Macho yako yataelekea kwa mke wako tu na sivinginevyo.
9. Utafanya juhudi kusikiliza yale yaliyosemwa na mke wako.
10. Utambusu kila siku asubuhi kwa upendo.
11. Hutakuwa mchungu likija swala la fedha.

12. WAJIBU WA MKE KWA MUMEWE KUTII
- Kutii kunakosemwa hapa ni kuwa endapo wawili mume na mke mmeshindwa kufikia uamuzi wa pamoja, basi,basi mke atatii uamuzi wa mumewe kama vile wamekubaliana awali

KULEA WATOTO (FAMILIA)
(a) Kuhakikisha afya ya mumeo na watoto
(b) Kuhakikisha kuwa chakula kinaliwa kwa wakati na kizuri
(c) Kuhakikisha usafi wa malazi, mavazi na miili yao
(d) Kufundisha watoto maneno ya Mungu
(e) Kuchunguza nyendo na tabia za watoto na mumeo na kuchukua tahadhari mapema.

KUMSHAURI MUMEO
Mke mwenye busara ni mshauri mwema kwa mumewe. Hatatoa ushauri wa kuleta maangamizi. Ushauri unafaa lakini ushauri mwingine upimwe kabla ya kufanyia kazi.

13. ADUI WA NDOA NI:-
UTAJIRI - Tajiri hupendwa na wasichana na pia huwa na tamaa ya kutafuta fedha kiasi cha kukosa muda na mkewe

UMASKINI - kazi ya kutafuta lishe ni ya baba, hivyo hushughulika sana na kujikuta amekuwa baba zaidi kuliko kuwa mume

MADARAKA - madaraka ya ofisini huyaleta hadi nyumbanini chukuzo kwa mume/mke. Maafisa hawana muda na wake zao kwa sababu ya makongamano/semina/ziara mbalimbali.- Hivyo wake zao wengi hutumia madereva kukidhi haja zao za kimwili- Mke ambaye ni ofisa humwachia house girl kazi za kupika, kufagia chumbani, kupeleka maji bafuni na hata kutandika kitanda, hivyo kusababisha mke kupinduliwa na house girl.

MAMBO YANAYOWAKERA WAKE

1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
9. Mume kubagua watoto
10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani..

Nikimpata mwanamke wa aina hii, nitampa talaka baada ya siku mbili au wiki.
Sitaki mwanamke mtumwa ambaye ananyenyekea mwanaume, nataka mwanamke mwenye msimamo na thabiti asiyeyumbishwa na mila za kikale zilizopitwa na wakati. Mwanamke ambaye tutasaidiana kulea watoto na si yule ambaye atawalea watoto pekee.....
Ebo!
 
Let me guess your type!
- Your compatible partner is the one who can challenge you appropriately.
- Mara moja moja atakusogezea chakula mezani kwa teke :)

To be happy with a man, you must understand him a lot and love him a little.
To be happy with a woman, you must love her a lot and not try to
understand her at all.
 
Hata kama kukiwa na kasoro za hapa na pale ukweli lazima ubaki kuwa "Ndoa ni mbaraka kwa wanandoa wanaoingia katika misingi na taratibu zinazotakiwa"

Mungu aliyenzisha ndoa alisema "Si vyema mtu huyu aishi peke yake" Leo watu tunataka kupindua kauli ya Mungu na kusema "Ni vyema kuishi peke yako"??????????

Hakuna mwanadamu aliye na upeo hata kufikia 1/100 ya upeo wa Mungu aliyetuuumba. Hivyo ukweli huu kuhusu ndoa utabaki palepale. Tatizo ni kuingia katika ndoa bila kufuata kanuni alizoziagiza Mungu.

Labda nikumbushie baadhi ya kanuni hizi:-
1. Mwanamume ndiye kiongozi wa familia na mwanamke anasimama kando yake kama msaidizi. (Tunaoamini Biblia tunaipata hii katika Mwanzo 2:18, Efeso 5:22-25)
2.Tendo la ndoa halitakiwi kufanywa nje ya ndoa. Hii inamaanisha kwa wasiooa na wasiooolewa na waliooa na kuolewa
3. Matatizo na changamoto katika mahusiano ni jambo la kawaida lakini anayeweza kupitisha katika hizo changamoto ni Mungu mwenyewe.

Cha ajabu sana......

Leo wanadamu tunataka kuingia katika ndoa kwa namna tunayotaka sisi wenyewe tena tunataka kuishi kwa namna tunayotaka wenyewe halafu tunategemea kuwe na maisha ya furaha. La! haiwezekani mpaka watu wamerudi katika kanuni alizoweka Mungu.

Tusitishe watu kwa kusema ndoa ni ngumu wakati ugumu tumeutaka wenyewe kwa kukiuka taratibu zinazotakiwa tukaingia kwa laana. Tuwatie moyo watu waoane maana ndoa ni njema tena ni takatifu tena ni mahali ambapo maadili ya jamii yanaanzia. Sasa tukisema ni ngumu kwa hiyo watu wasioe na kuolewa? Na watoto wazaliwe nje ya ndoa? Nani atawafundisha maadili?
Matokeo yake ni kuwa na watoto wengi mitaani, ama wengi wasiofundishika na kwa hiyo taifa na dunia nzima kukosa mwelekeo.

Jamani turudi katika misingi ya awali waliyotumia mababu zetu na wazazi wetu.
 
Re: Nimekubali Ndoa Ni Ngumu Kwa Wote, Japo Ni Raha Pia, Unasemaje?

...ugumu wa ndoa utausababisha wewe mwenyewe, labda tu kama hiyo ndoa ulilazimishwa na kweli hukuwa na hiari ya kuikataa.

ili ndoa idumu,inahitaji;

effective communication (masikilizano,maelewano); kupishana lugha ni jambo la kawaida ndani ya nyumba, si kila ulielewalo weye ndio mwenzako naye anastahiki alielewe hivyo, au akubaliane na kila ulisemalo. Kuna wakati inabidi kujishusha ili kukubaliana na matakwa ya mwenzako. Hata mapacha hawapatani kwa kila kitu.

empathy (kujali, kuhurumiana, kuelewana, etc); jiulize kila mara, "Ingelikuwa wewe ungejisikiaje"! hakuna jambo linalostawisha stawi wa nyumba kama kujipangia na kugawana majukumu. Hali hiyo inawezesha kuwepo na amani na haki sawa za maamuzi ndani ya nyumba yenu. Kasoro nyingi hujitokeza iwapo kutakuwa na uhuru unaopitiliza kupitiliza kiasi mpaka inaonekana ni uonevu na unyanyasaji.

Responsibility (uwajibikaji, juu ya kila jambo lihusianalo na ndoa yako). Kama mlivyoamua nyie wenyewe kuoana kwa hiari yenu mbele ya kadamnasi na kuapa mpaka kifo kitapowatengansha, ndio hivyo hivyo mnatakiwa kulirutubisha penzi lenu. Maisha ya ndoa ni kama nguo nzuri uloinunua na unaipenda kikweli kweli, bahati mbaya nguo hiyo hiyo 'inaweza chuja, kuchanika au kuja kukubana' usipokuwa mwangalifu. Jitihada gani utazochukua kuienzi nguo hiyo? ndio maisha ya ndoa hayo.

...kubwa kuliko yote, mheshimu, akuheshimu ili mheshimiane!
 
Ugumu wa ndoa unatokana na malezi yetu na ya wenzi wetu. Watu kujitoa hatutaki, tunatakaa kupata tu faida za ndoa, kuzitoa hatutaki.
 
Ni kweli ndoa ni ngumu lakini wengi huichukulia ndivyo sivyo. Wanaume wengi wao huchukulia kuwa kwa vile kaoa then mkewe anapaswa kumtumikia na ndio maana tunaona wanaolalamika kuwa nimeoa mke kiburi au mvivu hanifulii au hanichambi!! Wanasahau kuwa vyote hivyo vinafanyika kwa upendo. Mimi kukufulia underpant yako si kwa kuwa ni wajibu wangu na wala usije ukakaa hata siku moja ukanipazia sauti kwa nini sijaifua. Nafanya hivyo kwa sababu nakupenda na sipendi kukuona kila mara unastruggle kufikicha mikono yako wakati nipo. But ni kwa kuwa nakupenda na siku ukiniudhi dont expect nitaifua!!

Wanaume wengi hawaheshimu wake zao kisa wanaamini ni jukumu la mwanamke kumheshimu yeye. Mnanikera sana ninyi msojua maana ya ndoa ...... wa head ninyi!!

Wanawake pia wapo ambao wanakera kwa kutojua thamani waliyo nayo. Wewe umeolewa ukawe mke na sio mtumwa ama!! Jua thamani yako na haki zako za ubinadamu. Fanya yale unayoyaweza kwa kuwa unampenda mumeo na si kukulazimisha kufanya usiyoyapenda kisa amekuoa. Pia muache kuendekeza dhana ya kuwa mume ndie anayetakiwa kuhudumia familia kama una kipato nawe hudumia its your family too.... ukitegea ndo mwanaume anapopata mwanya wa kukunyanyasa kwa vile anajua wewe ni tegemezi. Sipendi

Naomba niwasilishe.
 
Ugumu wa ndoa unatokana na malezi yetu na ya wenzi wetu. Watu kujitoa hatutaki, tunatakaa kupata tu faida za ndoa, kuzitoa hatutaki.
Na kwa kuongezea ni kwamba.... wenye ndoa wenyewe ndio watakao determine mstakabali wa ndoa yao.... tokea mwanzo wanapaswa kujiwekea " rules of the game"... kuna zile basic minimum ambazo kila mmoja anapaswa kuzitekeleza kwa mwenzie.. halafu kuna mambo mengine ya ziada.Mara nyingi watu hawako wakweli..nimewahi kusikia baadhi ya wanawake wakijidai ati kuwa waume zao hawawezi kula chakula alichopika hausigeli... kwa msingi huo huanza na hiyo gia ya kupikia waume zao kila siku na kila mlo na baada ya kuzoeana na ile excitement kuisha wanaacha kupika na kuleta visingizio kuwa wamechoka. Sasa mwanaume aliyezoeshwa kupikiwa na mke kila siku toka amuoe ataelewa vipi?..jamani tuwe wakweli na tuache unafiki!Kwa wanaume nao, utakuta pale mwanzo penzi bado tamu... mwanaume atamfanyia mkewe mambo mazuri kama kumnunulia gifts, kumpeleka outing.. n.k. baadae anaanza kumwacha nyumbani kwa visingizio chungu nzima.. hapo mke atamwelewa vipi?..
Ninachotaka kusema ni kuwa gia unayoanza nayo basi uhakikishe utaendelea nayo na pengine uzidishe na si upunguze,Vinginevyo ndoa itayumba.

Hayo ya mume kuwa kichwa na mke shingo... yanaweza kujadilika zaidi..ila the bottomline ni kuwa katika nyumba kama ilivyo taasisi nyingine yeyote ile..lazima awepo kiongozi.. na kwa upande wangu sione shida kukubali kuwa mume ni kichwa na I think im happy with that.Kiongozi maana yake ni majukumu zaidi,, na si lelemama...kiongozi has to deliver.. na mume ambaye haonyeshi uongozi kwa maana halisi basi anastahili kuchekwa na si kushangiliwa.
 
Nakubaliana na wewe kabisa.

I am happy kwa nafasi yangu kama mama, Hata sina hamu ya kuwa na majukumu yake, kwanza namuonea huruma, maamuzi mengine magumu mno, yanataka ujasiri wa kiume. Mfano misiba, ndugu wakorofi, nk.
mimi niko tayari kumback wakati wote, 100% na kumpa ushauri kwa bidii zote, kumfahamisha mengine asiyoyajua,
unajua watu wanadhani kumpa mtu mmoja kuwa kiongozi ni kukubali kushindwa, na kuwa familia ni mashindano ya nani zaidi!
Hasa wanawake wasomi wanadhani usomi wao utaishia hewani, kama mume akiwa top! mimi sidhani kama ni kweli.
Unless hamuaminiani. (hili ni tatizo jingine)
 
Ndoa sio ngumu hivyooo kama watu wengi wanavyosema, it is all in your mind. Yaani kama kwenye nyumba mkiwa na positive attitude na mnakazamia mambo ambayo mazuri (Yaani mambo mazuri yanayofanywa na mke/mume) nyumba inakuwa na amani sanaa. Jaribu uone (Yaani Positive Attitude in the house na ku-complimate each other) kwa mambo yoote mazuri, na msi-concentrate kwenye mambo mabaya. Maana watu wengi wanapenda kukumbuka mabaya tuu na sio mazuri yanayofanywa na mwenzake
 
Ugumu wa ndoa unatokana na malezi yetu na ya wenzi wetu. Watu kujitoa hatutaki, tunatakaa kupata tu faida za ndoa, kuzitoa hatutaki.

Nakubaliana nawe kwa kiasi fulani. Hata hivyo, kumudu maisha ya ndoa elimu inahitajika kwani tofauti za malezi zipo na zitaendelea kuwepo. Hali kadhalika tofauti ya mahitaji baina ya wake na waume.

Na kwa kuongezea ni kwamba.... wenye ndoa wenyewe ndio watakao determine mstakabali wa ndoa yao.... tokea mwanzo wanapaswa kujiwekea " rules of the game"... kuna zile basic minimum ambazo kila mmoja anapaswa kuzitekeleza kwa mwenzie.. halafu kuna mambo mengine ya ziada.Mara nyingi watu hawako wakweli..nimewahi kusikia baadhi ya wanawake wakijidai ati kuwa waume zao hawawezi kula chakula alichopika hausigeli... kwa msingi huo huanza na hiyo gia ya kupikia waume zao kila siku na kila mlo na baada ya kuzoeana na ile excitement kuisha wanaacha kupika na kuleta visingizio kuwa wamechoka. Sasa mwanaume aliyezoeshwa kupikiwa na mke kila siku toka amuoe ataelewa vipi?..jamani tuwe wakweli na tuache unafiki!Kwa wanaume nao, utakuta pale mwanzo penzi bado tamu... mwanaume atamfanyia mkewe mambo mazuri kama kumnunulia gifts, kumpeleka outing.. n.k. baadae anaanza kumwacha nyumbani kwa visingizio chungu nzima.. hapo mke atamwelewa vipi?..
Ninachotaka kusema ni kuwa gia unayoanza nayo basi uhakikishe utaendelea nayo na pengine uzidishe
na si upunguze,Vinginevyo ndoa itayumba.

Mazingira ya sasa yanawaanda wasichana kuwa na matarajio makubwa kupitiliza, kama fairy tale vile. Mazingira hayamtayarishi mvulana kutimiza hizo fairy tale dreams za kina dada. Kumtegemea mwanaume aendelee na gia ile ile kipindi mnachumbiana ni makosa na wala sio realistic. Wanawake hawabadilishi gia?

MAMBO YANAYOWAKERA WAKE

1. Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
2. Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
3. Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
4. Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
5. Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
6. Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
7. Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
8. Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
9. Mume kubagua watoto
10. Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
11. Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
12. Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumbani..

This is very serious! Nani limemtokea mojawapo ya haya? (Please pick one)
Umewahi kusikia malalamiko yafananayo na haya?

Wanawake kwenye ndoa hapa nyumbani,
How do they handle/managing conflict? Upo msaada wowote kwa mwanamke nje ya familia?
Ofisi za ustawi wa jamii wanaweza kutoa msaada gani?

.
 
Nakubaliana nawe kwa kiasi fulani. Hata hivyo, kumudu maisha ya ndoa elimu inahitajika kwani tofauti za malezi zipo na zitaendelea kuwepo. Hali kadhalika tofauti ya mahitaji baina ya wake na waume.

Mazingira ya sasa yanawaanda wasichana kuwa na matarajio makubwa kupitiliza, kama fairy tale vile. Mazingira hayamtayarishi mvulana kutimiza hizo fairy tale dreams za kina dada. Kumtegemea mwanaume aendelee na gia ile ile kipindi mnachumbiana ni makosa na wala sio realistic. Wanawake hawabadilishi gia?

This is very serious! Nani limemtokea mojawapo ya haya? (Please pick one)
Umewahi kusikia malalamiko yafananayo na haya?

Wanawake kwenye ndoa hapa nyumbani,
How do they handle/managing conflict? Upo msaada wowote kwa mwanamke nje ya familia?
Ofisi za ustawi wa jamii wanaweza kutoa msaada gani?

.
A girl becomes a woman as soon as she realises that the there is no fairytale in life, that there is mister right, or prince coming her way.
A boy becomes a man when he understands that there is no damsel in distress , which will be forever be gratefull for what he once did.
Its all hard work, which will result to any happiness she/he gets.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom