Nimekosea wapi

coco bella

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
305
315
Niliwahi kuandika uzi wangu wa kutafuta mwenza humu ndani, katika wengi waliokuja nikabahatika kupata kijana mmoja aliyeukuna moyo wangu,nikaona nijaribu mahusiano naye sikutaka kujiachia mazima tangu nimemkubali ni wiki tatu zimepita na bado hajaweka fedha zake kwenye pochi yangu (sex) amekuwa akinionesha upendo wa hali ya juu, .

Hana elimu kabisa ila ni mfanyabiashara aliyefanikiwa, imekuwa ni kawaida kunifuata kazini kila ambapo nikimwambia aje na kunipeleka nyumbani,neno langu limekuwa sheria kwake, sasa tatizo ni hili wiki iliyopita akaniomba anifundishe kuendesha gari ili nikiweza anipe moja nitumie kati ya machache anayomiliki.

Mwanafunzi mimi nimekuwa muoga kuingia barabarani kibaya zaidi niliparamia ukuta na gari ikabonyea akanifokea sana kiukweli iliniuma kufokewa naye kwani mpaka alinitolea tusi, ndani ya gari ukapigwa wimbo wa sisi tunakula bata wa Jay mo, nikamuomba autoe akataka kujua kwanini nikamwambia simpendi Jay mo tumegombana, akataka kujua sababu sikumwambia basi hapo ndipo tatizo likaanza amenuna hataki kuongea na mimi.

Sasa Wakuu sielewi nimekosea wapi kwenye kugonga gari au kukataa kumwambia ugomvi wangu na Jay moo ni nini!!! nakosa raha yaani mahusiano yangu mapya yavunjike ndani ya wiki tatu sina rahaa kabisa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi kuandika uzi wangu wa kutafuta mwenza humu ndani, katika wengi waliokuja nikabahatika kupata kijana mmoja aliyeukuna moyo wangu,nikaona nijaribu mahusiano naye sikutaka kujiachia mazima tangu nimemkubali ni wiki tatu zimepita na bado hajaweka fedha zake kwenye pochi yangu (sex) amekuwa akinionesha upendo wa hali ya juu, hana elimu kabisa ila ni mfanyabiashara aliyefanikiwa, imekuwa ni kawaida kunifuata kazini kila ambapo nikimwambia aje na kunipeleka nyumbani,neno langu limekuwa sheria kwake, sasa tatizo ni hili wiki iliyopita akaniomba anifundishe kuendesha gari ili nikiweza anipe moja nitumie kati ya machache anayomiliki. Mwanafunzi Mimi nimekuwa muoga kuingia barabarani kibaya zaidi niliparamia ukuta na gari ikabonyea akanifokea sana kiukweli iliniuma kufokewa naye kwani mpaka alinitolea tusi, ndani ya gari ukapigwa wimbo wa sisi tunakula bata wa Jay mo, nikamuomba autoe akataka kujua kwanini nikamwambia simpendi Jay mo tumegombana, akataka kujua sababu sikumwambia basi hapo ndipo tatizo likaanza ameninua hataki kuongea na mimi Sasa Wakuu sielewi nimekosea wapi kwenye kugonga gari au kukataa kumwambia ugomvi wangu na Jay moo ni nini!!! Nakosa raha yaani mahusiano yangu mapya yavunjike ndani ya wiki tatu sina rahaa kabisa


Sent using Jamii Forums mobile app
Tulizana ndg,ili upate kuolewa

Usijaribu kuyajaribu mapenzi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole
Screenshot_20190210-210316~2.jpeg


Be Humble is free of charge
 
Ulipokosea ni hapo pa JAY MOO,jamaa akafikiria inawezekana mlikua na ukaribu wa hali ya juu kiasi kwamba uchukie mpaka nyimbo zake,yani ishu imeonekana too personal,na atakua kakuona wewe ni mtu wa starehe sana mpaka unashinda na kina MO TEKNIK...na kama unavyojua watu wengi wanavyowachukulia hawa wasanii wetu kua wako active kwenye maswala ya kuchezea wanawake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom