Tukisema bunge ni dhaifu tunafokewa!Nukuu ya Prof Assad wakati akiwa CAG "Kama Bunge linashindwa kusimamia serikali huo ni udhaifu wa Bunge". CAG Assad aliitwa na Ndugai kibabe Bungeni ajieleze
Swali la Pascal Mayaalla"Je Bunge linatumika kama muhuri au rubber stamp kupitisha mambo ya serikali? "Pascal Mayalla aliitwa Bungeni kibabe na Ndugai ajieleze
Unaweza ukacheka na kukasirika kwa wakati mmoja lakini kinachowafanya waumini wa katoliki kila jumapili kabla ya sala na mahubiri kutubu kwa kutamka maneno haya:Nimekosa Mimi, Nimekosa sana ndio maana nakuomba...........
Kwa wasiofahamu hapa JF, Kila jumapili kwa Wakatoliki ni sherehe kubwa sana, Na sio dhihaka hata kidogo
Kila jumapili wakati wa Misa Wakatoliki wanaadhimisha nguzo kuu ya ukristo yaani sherehe ya Kufa na Kufufuka kwa kristo, Hivyo wanoamini kama Wakatoliki kuwa kuna ufufuo baada ya haya maisha wanatakiwa kuishi kwa toba au kutubu wakati wote yaani Nimekosa Mimi, Nimekosa sana........
Dhihaka iliyofanyika Leo mbele ya waandishi wa habari na yule mheshimiwa haikubaliki hata kidogo,
Unawezaje kutubu ukweli ambao kila mtu anaufahamu ni ukweli wa mambo kuhusu deni la Taifa?
Unawezaje kutubu na kukana kauli sahihi ambayo ulitamka mbele ya umati na maelfu ya watu?
Dhihaka kuu kabisa ni kuomba radhi wananchi kwa mambo ambayo hatujawahi kushiriki bungeni au kushirikishwa kuhusu nchi hii
Sio mara ya kwanza mheshimiwa Spika kufanya dhihaka mbele ya jamii
Aliwahi fanya dhihaka juu ya maslahi ya Tundu Lissu na hakuomba msamaha mpaka Leo hii
Aliwahi fanya dhihaka kwa CAG Prof Assad hajatubu mpaka leo
Aliwahi fanya dhihaka kwa tangazo kuwa atawashughulikia wanatoa maoni tofauti hajawahi tubu mpaka wakati huu
Wakatoliki wanapoomba toba hata siku moja hawatamki kauli kwa sauti kwa mambo walioyafanya na wala hawatangulizi risala ya kujisafisha kwanza ndio watubu makosa yao
Kitendo cha Ndugai kutanguliza hotuba na risala ndefu ili kukana kauli zake sahihi na kujisafisha haikuwa toba wala kuomba msamaha bali ilikuwa ni dhihaka kwa wana ccm na Mamlaka iliyojichimbia mzizi zaidi
Ni busara Ndugai akaachana na uspika wa Bunge au akajivua uwanachama wa ccm ili kujenga heshima yake uzeeni
Ndugai kutamka nimekosa sana, Nimekosa Mimi....... Alikuwa anatubu dhambi na kujuta kwa nani?
Ndugai kwa kutamka Nimekosa sana.... Alikuwa anahitaji nani amuombee na kumsamehe, Kuna binadamu anaweza toa msamaha na hata akitoa msamaha kwa kibali gani alichopewa wakfu wa kutoa msamaha?
Tuache dhihaka kwenye imani za watu daima tusimamie ukweli tunaouamini