NIMEKOMA kushobokea vi-offer mbuzi! (My Bad Friday Night) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NIMEKOMA kushobokea vi-offer mbuzi! (My Bad Friday Night)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by lara 1, Oct 21, 2012.

 1. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Peopleeeeeeeeeessss! (Wakubwa zangu shikamooni)

  Natumai wote wazima, na hakuna alieshikwa kwenye maandamano sababu wengi wenu wazee WAKUJIKAUSHA na kufatilia kwenye tv. (With the exception with fazaa, sijui kama umepona mpambanaji wa ukweli) Mie mzima nimetoka kwenye upambe nuksi wa uchaguzi wa Wanawake wa CCM huko (lazima nijikombe viti maalumu mchezo!!!) na mgombea wangu kashindwa, anyway sio mwisho wa dunia, tunajipanga upya. Life has to go on.

  Kubwa lilinonileta hapa ni tukaio lililonikuta ijumaa jioni, Daaaaaah! Acheni tu! Almanusura nipewe MITAICHI, TAIKONDO, JUDO, KARATE, SUMARAI, KUNGFU, SUMO NA KICK BOXING KWA MPIGO!!!! Chezeya wachina nyie.

  Ishu ilikuwa hivi, mchaga kasafiri kikazi sasa nikaona kuwahi kulala ijumaa kwa sie wanywaji ni zambi, so nitafute mishe mishe za japo kupunguza kiu kwa tuhenken tuwili ili nisiamke na hangover. Basi kuna sharo flani hivi aliniofferga dinner , nikawa sisomeki kwenye radar, sasa kila nikikutana nae inakuwa kama deni vilee, haishi kuniinvite over n over. Nikaona nimtafute tukapunguze mawazo kidogo. Basi nikamuuliza if the offer still stands akasema yah! Tukaonana tayari kwa dinner.

  Akaniuliza ungependa kwenda wapi? Nikamwambia chagua weye! (Maksudically sabab yeye ndo anajua ana bajeti gani, itatosha wapi, alaf hawa masharo wasumbufu sana, ukimpeleka uswazi anaweza kukushusha bure) Akangangania bana chagua mwenyewe(mie ndo nichague) Mimi nikachgua bana, twende kwenye kisehem flani cha wachina nasikia wanauza wine na liquor za China, Taiwan na Hongkong. Akakubali banaaa. Kufika ushamba mzigo, nikamuuliza mhdumu whats is the favourite ya wengi hapo, akanitajia nikamwambia tuletee. Inapimwa kwenye tuglass tudogo, sie tunatirishia tumboni tu. Ni tamu kusema kweli, magnificient! Glass moja yaanzisha ingine.

  Midamida tukaitisha bili basi, sharo kuona bili sura ikamsawajikaaa! mie kimyaa!,Mara akanigea nikaitazama, ni nomaaa! Kumbe the shit was damn expensive!!!! Ila nikanyuti sikusema chochote. Basi ndo kuniambia kwa upole, i cant cover this bill, nina shoti!!! Mtumeeeeeeeee! Na mie ndo sikubeba pesaa! Chupi ilinibanajeeee! Nikajikaza kibingwa nikamwambia toa basi uliyonayo, Ndo kunipa robo ya bili!!!!!!!!! Nikaona huyu anatka anichakachue, mwenyewe wa kitaa vile vile, nikamwambia Mimi natoa pesa ya nusu yangu tuuu, we hiyo robo iliyobaki utajiju! Nikaza kwenye kitita cha ofisi nikakwapua kadhaa, kumcheki huku mtu chozi linamlengalenga. Nikaona aibu za nini nikamuita muhudumu, nikamlipa bili yote. Sema ndo kanitia SHOTI KUBWAAA! HAIKUWA MPANGO!!!! Tukaondoka kimyakimya, njiani analeta story za ILL MAKE IT UP TO U!!!!( He will make it up to me My As*) I SO SORRY! Blah! Blah! Blah!

  Hapa najamba jamba kupata pesa ya kujazia kitita cha ofisi kesho ndo kesho!!!! Na uchaguzi ndo tumepoteza, najihisi malaria, sijui nimwambie nini mchaga anitumie hizo MBESA za watu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hahahahahahahah pole bibie ndo mana ukatoweka,ila uwe uko full unapotaka kutoka na sharo,mie nikitoka na sharo lazima nijipange yaan nahakikisha pochi iko sawa ila kama mtu mwenyewe yuko fiti nabeba naul2,pole lara 1 ndo challenges za masharo hao,hapo alinywea nadhani hata kama alitaka kuonja hakuwa na jeuri tena
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  bili ilikuwa kiasi gani?
  hoteli ipi?
   
 4. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Mwenzanguuuuuu! Sharo kaniingiza KINGI na usafiri wa MDINGI wake, mi nikajua ANAJIMUDU!!!!!!!!1 Kumbe ushuzi mptupuu! NIMEKOPWA LIVE LIVE!!!! Nimenuajeeee! Nasonya kimya kimya tu hapa. LOL!
   
 5. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Mpana we mwanaume kama MEZA ZA KAMARI!!!!! Bili wataka unisaidie? (Ningekutajia ila ni personal manake utaanza mjadala kama hiyo ni kubwa, ndogo au kawaida. La muhimu kwangu KUBWAAA!) Hoteli wataka na wewe uende? sio hoteli ni kisehemu cha Wachina kama PUB flani hivi, kapya, kapya huko mitaa ya wenyewe sidhani kama kinajina, mwenyewe nilielekezwa tu kwa directions. Haya info ambazo sijaziweka ujue ni private, na nimezi ommit kwa maana yangu. Upo hapo?
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  nitumie account yako nikutumie pesa..
   
 7. B

  Bi nyakomba JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 387
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  haahahahah post zako mie huwaga mbavu sina inanikumbusha enzi za kina Mwasity na Muft Darhotwire. Pole lol hahhaah
   
 8. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Shosti ogopa masharo, ushuzi mtupu kila kitu dady this,mumy that....vimezoea kulelewa viepuke kama ukoma usirudie tena!!
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Offer za migomigo ndo zilivyo lol
   
 10. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Ngoja ni ku PM Namba ya M- PESA!!!! Tahadhari kabla ya hatari, je huo msaada hauna VIGEZO NA MASHARTI YATAKAYOZINGATIWA BAADAE? Hahahaaaaaaaa!
   
 11. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Hahahaaaaa! Nimekomajeee? Itabidi the boss uniunganishe na offer za obay bana, nitahadhirika mwenzio!!!! Ukinipigia pande MI THE BOSSES wenzio sio haba atiii!
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mh! nahisi kizunguzungu, kwani hata kama ingekuwa ni Famous Grouse Gold Reserve 12 Year Old bado najiuliza ilkuwa ni chupa nzima au?
  Kwa huku bongo bei yake mpaka sasa imfikia 15,000 kwa tort moja na hapo nazungumzia 5 Star Hotel, sasa kama ni Chinese Pub, Sidhani inaweza kufikia bei hiyo...

  Hii mwanangu lara 1 kwangu mimi ni ngumu kumeza...
  [​IMG]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mkipewa ukimwi mnalalama
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ndio maana mimi nikimpa mtu offer namweleza bajeti yangu mapemaaa na hata drinks selection natoa angalizo...
  haya mambo ya kujifanya unamuachia mtu uhuru wa kuchagua aina ya vinywaji wakati pocket yako inapumulia ICU siyataki kabisa.
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi kuna sehemu ukimpa mtu offer
  hata ukiwa na laki haitoshi...

  kuna beer zinaitwa corona i guess ..
  ukipata mtu akazigida zaidi ya kumi kama ni five star hotel...umeumbuka lol..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Angalia usizoee sana,halafu hiyo ndo faida ya usaliti si ulitaka kumsaliti mchaga wa watu,haya yamekukuta.nilitaka nikutumie vijipesa kama mchango wangu lakini umeniudhi kumbe we mali ya mutu tena mutu menyewe Muchaghaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ndio maana mpaka leo unanizungusha ki date changu....
  Njoo bibie nitakukabidhi mshiko ujipangie mwenyeweeeee.....!
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hahahahahaha.... kama kawaida yako lara 1 hukosi vijimambo.
  Ilikuwaje ukashindwa kutumia ujuzi wako wa external factors kujua kama kiwanja unachomchagulia huyo baro anakimudu?

  btw, naomba nikuletee kadi ya chama chetu. Nakuona wewe ni kamanda mwenzetu, unaipatia sana hiyo salamu yetu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nayajua hayo, kuna baadhi ya wadada hupenda kujaribu kila kitu ukiwapa Ki date, kama huna uhakika na bajeti yako sema usikike kuliko kukaa kimya.
  Mimi huwa sirembi, namwambia kabisa, hapa ni mwendo wa sofri drinks tu bia tutakunywa uswaziii........
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  dawa ni kutowapeleka huko
  wewe nenda nao kwenye taarab...tu lol
  kiingilio 5000, beer 2000...
  shughuli imekwisha lol
   
Loading...