Nimekodi shamba la mikorosho Masasi Mtwara, nina hofu na Corona kuharibu soko

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,051
Pamoja na kwamba zao la korosho hutegemewa Sana na Wana kusini, lakini kumekuwa na desturi ya wakulima Kukodisha mikorosho yao kwa mwaka mmoja, miwili hadi mitatu.

Binafsi nimechukua shamba la mkulima fulani kwa miaka miwili, hivi karibuni nitaanza kuipalilia na mwezi wa 6 nianze kuipiga dawa. Hofu yangu ni hizi lockdown za mataifa makubwa, kweli watanunua korosho msimu ukiwadia? Hazitatuozea majumbani kweli. Najaribu kuwaza tu, maana nimesoma Uzi mmoja humu Kuna makampuni yapo mbioni kulazimisha kuwapa wafanyakazi wake likizo kutokana na kukosa malighafi toka nje kutengenezea bidhaa zao, ina maana meli na ndege zimesimamisha huduma nchi nyingi.

Je, korosho zitabebwa na nini? Na nani? Tutazifanyia nini sisi hapa Bongoland?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usihofu bwana kwani unavuna muda huu, Si bado? Corona itaisha mambo yataendelea kama kawaida,

Wanaostruggle ni watu waliokuwa wanasafirisha bidhaa kwa ndege Hali ni mbaaya Sana kiukweli.. Avocado, mboga nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah korona ikiendelea kutafuna hawa weupe. Korosho itakosa soko kabisa na Bongo LAND wanakula wakishua tuu muda wa asubuhi kwa breakfast. Usikate tamaa lakini huku buza itabidi tuanze kuzila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kinaitwa Aftermath, kumbuka pia Dunia nchi karibia zote zimeingia kwenye Mdololo wa Uchumi hivyo madhara ya huu ugonjwa yatalast muda sana
Usihofu bwana kwani unavuna muda huu, Si bado? Corona itaisha mambo yataendelea kama kawaida,

Wanaostruggle ni watu waliokuwa wanasafirisha bidhaa kwa ndege Hali ni mbaaya Sana kiukweli.. Avocado, mboga nk

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom