Elections 2010 Nimekatishwa tamaa sana na Kagera

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
1,045
Matokeo ya uchaguzi yaliyowapa ushindi Wabunge wa ccm mkoani Kagera na hasa kagasheki yamenihuzunisha sana ikizingatiwa huko ndo nyumbani. Wale wa kwetu, kuendelea na ccm bila wapinzani si ni sawa na kukataa maendeleo? Tujipangeje 2015?
 
hivi we omutwale.. unafikiria vizuri wewe.....usishabikie chama ukasahau mtu anayeweza kuleya maendeleo....kagasheki desserve it
 
Kazi ya MB si kutoa misaada atakapo kwa pesa zake au rasilimali zake bali ni kuwashirikisha wananchi wajiletee maendeleo, kuwawakilisha ktk utunzi na urekebishaji wa sheria na kuhakikisha kodi wanazotoa wananchi zinawarudia kwa huduma bora za jamii ikiwemo miundombinu.
 
Matokeo ya uchaguzi yaliyowapa ushindi Wabunge wa ccm mkoani Kagera na hasa kagasheki yamenihuzunisha sana ikizingatiwa huko ndo nyumbani. Wale wa kwetu, kuendelea na ccm bila wapinzani si ni sawa na kukataa maendeleo? Tujipangeje 2015?

mimi nimesikitika zaidi. Bado wamefumba macho. hata hivyo tutawafumbua macho by 2013
 
Kweli bana Bukoba ilikuwa tegemeo la wengi lakini ndo hivyo tena wametuangusha....
 
Nadhani wao ni nafuu, Taarifa ya Mkoa wa RUVUMA ni kuwa majimbo yote wameyakabidhi CCM. Hata sisi tumekuwa wajanja hapa kwetu LINDI mjini tumepeleka CUF
 
:smile-big::A S angry:bukoba ni strongpoint ya CUF na si Chadema,hivyo uongozi wa chadema inabidi uweke nguvu za ziada bukoba/kagera
 
Matokeo ya uchaguzi yaliyowapa ushindi Wabunge wa ccm mkoani Kagera na hasa kagasheki yamenihuzunisha sana ikizingatiwa huko ndo nyumbani. Wale wa kwetu, kuendelea na ccm bila wapinzani si ni sawa na kukataa maendeleo? Tujipangeje 2015?
:A S-cry::A S-frusty::frusty: Nitaku PM Omutwale nikuambie jambo!
 
Bukoba dini ndio tatizo. Huko ndiko tunakoelekea.......... Nawatakia safari njema...........
 
:A S-cry::A S-frusty::frusty: Nitaku PM Omutwale nikuambie jambo!

Sawa MF labda itanipunguzia stress maana hakuna picha wala uwiano kati ya Rais ucyemjua kumpa ushindi wa zaidi ya 50% na kumnyima uliyemlea, unayemtambua kwa mazuri ushindi ule ule!
 
Yah.., mkuu nami sikutegemea wana BK kuangusha mabadiliko kiasi hicho...
 
Matokeo ya uchaguzi yaliyowapa ushindi Wabunge wa ccm mkoani Kagera na hasa kagasheki yamenihuzunisha sana ikizingatiwa huko ndo nyumbani. Wale wa kwetu, kuendelea na ccm bila wapinzani si ni sawa na kukataa maendeleo? Tujipangeje 2015?

Bwana Mshanage!! Mimi pia kule ni kwetu tena jimbo la NKENGE, ni ukweli CCM inatawala ila wabunge wetu ni wa ukweli wanazidi wengi wa upinzani. KAGASHEKI namkubali, Mama Tibaijuka namkubali pia. Sasa ukiwa na hawa upinzani wa nini!!!!
 
Kagera ni wazuri. Mgombea wa CUF ndo katupunguza. alijua hawezi kupata lakini akampunguzia kura Rwakatare. Ata Ubungo, Mtatilo Kidogo amwaribie Mnyika. Ila Bukoba Mjini Dr. Slaa kaongoza. Umeelewa? Si udini tu bali CUF.
:israel::israel:
 
Bwana Mshanage!! Mimi pia kule ni kwetu tena jimbo la NKENGE, ni ukweli CCM inatawala ila wabunge wetu ni wa ukweli wanazidi wengi wa upinzani. KAGASHEKI namkubali, Mama Tibaijuka namkubali pia. Sasa ukiwa na hawa upinzani wa nini!!!!

Vipi Karagwe?
 
Ni kweli mtu wangu sikutegemea rafiki zangu akina Nshomile kfanya makosa makubwa hivyo.....anyway ndio demokrasia....... majuto mjukuu...... watajifunza 2015.
 
kwa ujumla ndg zangu,nina mengi ya kuwaambia kuhusu bukoba,wana bukoba wana njaa sana kutokana na umaskini wa tanzania; Nasema hivyo kwa kuwa wameweza kununuliwa kwa kanga,tisheti na vilemba vya ccm vilivyomwagwa kama njugu siku mbili kabla ya uchaguzi.Aidha matokeo ya hapa yalijulikana mapema miezi miwili nyuma au mitatu pale ambapo wana kagera walipouza shahada zao kwa bei ya kilo moja ya nyama(steki).
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom