Nimekataliwa kwenye maombi ya kazi kisa Ulemavu wangu

Mwenda bure si mkaa bure, huenda akaokota.

Pamoja na udhaifu/ulemavu wangu sijakata tamaa kurusha ndoano kila ninapopata/kukutana na fursa yenye harufu ya mkate wa kila siku kwani nina imani ndoano yangu inaweza kuinasa fursa. Mungu hamtupi mja wake.

Hadi sasa nishajaribu kutega ndoano zaidi ya saba katika madimbwi tofauti ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali.

Baadhi ya madimbwi hayajaonesha ishara yeyote ya kutambua kitu kigeni kwenye mazingira hayo jambo ambalo naweza kusema huenda ndoano niliyoitega haijaleta athari za kutambuliwa kuwa ni kitu kigeni ili kiweze kuchukuliwa hatua. Kwa upande mwingine pia inaweza kuwa ndoano yangu imetambuliwa ila imekwepwa kwa namna moja au nyingine.

Bali na tathmini hiyo niliendelea kuweka mitego ya ndoano yangu hadi nikabahatika kuona kidimbwi kisicho cha kiserikali, bila hiyana kama kawaida yangu nikarusha na kuitega ndoano. Baada ya ndoano kufika kunako penyewe athari zikaonekana. Mkazi mmoja wa kidimbwi akaamua kuanza kushughulikia ndoano yangu ili kuweka mazingira salama kidimbwini.

Alifanya utafiti ili kubaini ni aina gani hii ya ndoano iliyotegwa kama itakuwa na manufaa chanya au hasi kidimbwini. Mara ghafla notification ikaibuka ikisomeka "Kazi uliyoomba na usikivu hafifu sidhani".

Moyo ukanyong'onyea ila ulipigwa moyo konde, na kushukuru kwa kupewa ukweli bila kuzungushwa, nikajibu kwa upole huku nikiwa na masikitiko moyoni.

Kipindi cha mwishoni cha Awamu ya tano nilisema hivi Haikuwa uamuzi sahihi kusitisha ajira hata kwa Walemavu, hili kundi linataabika sana mtaani.

Ni matarajio yangu Awamu ya Sita hili jambo mtaliangalia kwa jicho pevu
Pole sana ndugu!

Haya mambo kuna wakati yanakuwa sensitive sana. Ni kweli kuna baadhi ya kazi inaweza kuwa ngumu kutimiza majukumu yake kama una udhaifu fulani, bahati mbaya waajiri huwa hawatoi kitu gani wanategemea kukipata toka kwa mwajiriwa tarajiwa na pia hawatoi feedback baada ya usaili. Wanaweza wakawa na sababu genuine kabisa ya kutotoa ajira fulani, lakini wakakosa kutoa feedback.

Ni waajiri wachache tu wanaweza kukutenga au kukunyima ajira kwa sababu ya udhaifu wa kiungo au viungo vya mwili.

Lakini pia kuwa dhaifu wa kiungo sio sifa ya kwanza ya kupata ajira, ila ni sifa ya kupata upendeleo wa kazi ukifanya usaili vizuri.
 
Hearing Aids nishawahi kutumia bila mafanikio yoyote, nimetumia hivyo vifaa vya aina tatu tofauti.

Hospital nishaenda mara nyingi sana, Muhimbili nimeenda mara 3, TMJ mara 1, Ekenywa mara 1, Hear Well mara 1(hii ni Clinic ya masikio ipo Upanga, Diamond Tower)

Kote huko walisema nitumie vifaa lakini hivyo vifaa havikusaidia chochote
Pole sana..., basi nadhani the only way ni kutafuta kazi ambayo usikivu hauathiri utendaji kila kazi ina skills set zake (au kama vipi ni kutafuta kitu cha kufanya mwenyewe ili mradi mkono uende kinywani)

Kuna jamaa alikuwa ni kipofu ila hilo halikumzuia kuwa Home Secretary wa UK.... Duniani hususan dunia ya sasa inabidi usingoje kupewa / kukubaliwa kama unaweza ni kuchukua..., (ila all in all ili mradi mkono uende kinywani). Mpaka pale tutakapokuwa na system ya Kila mtu kupata kulingana na skill set yake na sio tamaa yake wengine wengi wataendelea kuwa marginalized...

"David Blunkett, Baron Blunkett, PC (born 6 June 1947) is a British politician, now in the House of Lords, who was MP for the Sheffield Brightside and Hillsborough constituency for 28 years until the 2015 general election, when he stood down.[3] Blind since birth, and coming from a poor family in one of Sheffield's most deprived districts, he rose to become Education and Employment Secretary, Home Secretary and Work and Pensions Secretary in Tony Blair's Cabinet following Labour's victory in the 1997 general election."
 
Pole sana ndugu!

Haya mambo kuna wakati yanakuwa sensitive sana. Ni kweli kuna baadhi ya kazi inaweza kuwa ngumu kutimiza majukumu yake kama una udhaifu fulani, bahati mbaya waajiri huwa hawatoi kitu gani wanategemea kukipata toka kwa mwajiriwa tarajiwa na pia hawatoi feedback baada ya usaili. Wanaweza wakawa na sababu genuine kabisa ya kutotoa ajira fulani, lakini wakakosa kutoa feedback.

Ni waajiri wachache tu wanaweza kukutenga au kukunyima ajira kwa sababu ya udhaifu wa kiungo au viungo vya mwili.

Lakini pia kuwa dhaifu wa kiungo sio sifa ya kwanza ya kupata ajira, ila ni sifa ya kupata upendeleo wa kazi ukifanya usaili vizuri.
Sawa mkuu, Asante
 
Back
Top Bottom