Nimekata tamaa

yaani wewe toka mwezi wa saba wakati wenzako wanamiaka mitano 5 hadi viatu vimekwisha wamebakia kufunga tai balabarani lakini bado hawajakata tamaa..Ukikata tamaa ndiyo mwisho wa maisha?hakuna kukata tamaa haujui kesho yako hiko wapi.KEEP UP
 
Yaani wewe umetuma maombi sehemu 20 na umeshakata tamaa?

Don't abandon your to despair like that. Just keep sending them applications and you'll start getting calls.
 
bahaticaro hustahili kukata tamaa... Umesoma, una nyenzo ambazo ni Watanzania wachache wanazo, tayari umekuwa exposed kwa kiasi cha kutosha kuweza kujisimamia na kufanya Change. Najua ni ngumu ila inawezekana.

Miezi saba ya kutafuta kazi na umekata tamaa? Saizi nimapemaa sana na naomba nikukatishe tamaa zaidi kuwa utamailiza hata mwaka, pengine hata miwili na zaidi. Soko la ajira limekuwa gumu mno likisukumwa na sababu mbali mbali ikiwemo na ukiritimba humo humo. On top of that graduates wamekuwa ni wengi sana ukifananisha na miaka ya nyuma.. Hivo tambua hili tatizo linazidi kuwa sugu na wala halina matumaini ya ufafuu...

Hata hivo nakupa hope kwa kukusihi kuwa jaribu kuangalia namna na taratibu zingine za kujishughulisha nje ya kuajiriwa. Najua kuwa sio rahisi na mitaji inasumbua ila bado inawezekana kabisa kuanza from somewhere kwa mtaji mdogo sana ili mradi tu usiwe katika kundi la wale ambao huona aibu kufanya kazi ambazo siio za ofisini kwa vigezo vya kuwa wasomi.

Kuna hii thread hapa, sijui ila yaweza kukusaidia ukapata mwanga wa kitu gani namaanisha. Kila la kheri na Mungu akuwekee wepesi wa kupata suluhu ya tatizo lako. Pamoja saana.

Link - https://www.jamiiforums.com/ujasiri...a-mtaji-pesa-mkubwa-au-bila-mtaji-kabisa.html
 
Last edited by a moderator:
bahaticaro nakusihi uzingatie neno hili.

215978_412262798846926_1351128228_a.jpg
 
Last edited by a moderator:
Pole sana,umesoma nini na umefaulu kwa kiasi gani na uwezo wako ni upi?umefikiria kufanya kazi ingine zaidi ya ulichosomea?kama una imani umefanya maombi maalumu kupata kazi?unaweza kuendelea na degree ya plili kama una uwezo huku unaendelea kutafuta
 
Huo muda ni mfipi sana kukata tamaa.We kata tamaa tu ili upunguze competition!
 
nipo idle tangu mwez wa saba nimeshaaply kazi zaid ya sehemu 20 sijapata hata moja nimejichokea maisha magum dah! nimekuwa nayaona:wof:

My goodness, only 4 months and 20 applications!?!? you're mad! There was a time I was out of work for more than that and I had sent more than 250 applications in and out of the country! Ukizingatia kisomo changu ni cha juu. Mungu hawezi kusaidia ambao wanakata tamaa. Haya basi umekata tamaa... kaa nyumbani ulale... tuone kama kazi itakutafuta hapo kitandani! Nafikiri watoto tunaowalea siku hizi are too weak. Someone needs to talk some sense into them... talking about nimekata tamaa niko idle tangu mwezi wa saba nimeapply zaidi ya sehemu ishirini...mssscchheeewww! Get off your behind and apply to 50 more... TOUGH LOVE and Good luck!
 
pamoja na juhudi zako - kumbuka - THERE IS NOTHING IMPOSSIBLE WITH GOD - haijalishi situation ikoje - rushwa, kujuana etc. lakini MUNGU AKIINGILIA KATI KWENYE ISSUES ZAKO .............. YOU WILL MAKE IT.

so usikate TAMAA - pambana na mpambanaji bora hakati tamaa - Mwombe Mungu pia akupe direction - na afungue ufahamu wako - ili uwaze sawa sawa - ujipange - WAWEZA KUWA MWAJIRI BADALA YA MWAJIRIWA - FOCUS HIGH - :amen::amen:
 
asa ww umeanza juzi unakata tamaa, wenzio tuna mwaka wa pili sasa. usikate tamaa ndugu yangu asa hivi tafuata kazi yoyote itakayokupa kuishi wakati unasaka ajira, hata kama ni kupiga tofali kaka usichague kwa sasa. utapata kazi just b mvumilivu. wenzio walikaa miaka mitano ndo wakapata bt walikuwa wavumilivu na maisha yao yako poa sasa
 
nipo idle tangu mwez wa saba nimeshaaply kazi zaid ya sehemu 20 sijapata hata moja nimejichokea maisha magum dah! nimekuwa nayaona:wof:
kukata tamaaa ni dhambi, nikutomuamini MUNGU!
Ila nafasi ingalipo endelea kujibidisha katika kutafuta kazi na fursa zingine
 
nipo idle tangu mwez wa saba nimeshaaply kazi zaid ya sehemu 20 sijapata hata moja nimejichokea maisha magum dah! nimekuwa nayaona:wof:

Uko idle - maana yake hujishughulishi na jambo lolote......????, huwezi kupata kazi kwani hata huko kazini utakuwa IDLE na waajiri wanaliona hilo kutoka ndani yako. BADILI MTAZAMO......!!!!
 
Hili ndio tatizo la elimu ya kitanzania, inawaandaa wasomi kuwa wafanyakazi wa kuajiriwa badala ya kuwaandaa kuwa watu wanao weza kutengeneza fursa za ajira kwa kutumia rasilimali zilizopo.. Nakushauri ubadilike, achana kabisa na hiyo attitude ya kutafuta kazi ya kuajiriwa. Dhana ya kusoma & kufaulu vizuri ili upate kazi ya kuajiriwa ilikuwa valid mwaka 1985 kurudi nyuma, sasa hivi hali imebadilika sana. Dunia ya sasa hai wa accomodate watu wanao amini katika kuajiriwa, bali wanao weza kuthubutu kujiajiri wenyewe. Wewe kama mpaka leo hii bado una mawazo ya kutafuta kazi ya kuajiriwa, basi count urself as a person who can fit in the winners circle.



[h=1]“Do not pray for an easy life, pray for the strength to endure a difficult one” Bruce Lee.[/h]
 
Yaani wewe umetuma maombi sehemu 20 na umeshakata tamaa?

Don't abandon your to despair like that. Just keep sending them applications and you'll start getting calls.

na mi nimekata tamaa..... hakuna kazi za box huko??????
 
Duuu!miaka mitano,si hadi material yote alojifunza class yanayeyuka.
Mh!dunia kweli tambala bovu


asa ww umeanza juzi unakata tamaa, wenzio tuna mwaka wa pili sasa. usikate tamaa ndugu yangu asa hivi tafuata kazi yoyote itakayokupa kuishi wakati unasaka ajira, hata kama ni kupiga tofali kaka usichague kwa sasa. utapata kazi just b mvumilivu. wenzio walikaa miaka mitano ndo wakapata bt walikuwa wavumilivu na maisha yao yako poa sasa
 
nipo idle tangu mwez wa saba nimeshaaply kazi zaid ya sehemu 20 sijapata hata moja nimejichokea maisha magum dah! nimekuwa nayaona:wof:

yaani umeapply kazi 20 then unasema umekata tamaaa! acha kukufuru wewe, watu wameapply zaidi ya kazi ya mia na bado hawajapata. chezea Tanzania wewe jikaze ndugu bado muda upo utapata tuu kazi. na ni bora kidogo ulivyochelewa kupata ili ukipata uwe na nidhamu ya kazi,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom