Nimekata tamaa ya maisha nahitaji msaada

Mwenzako changamoto yake sio kuchafuka kwa tope wala kushindwa kusimamia au kuingia shambani, mtaji au pesa ya kuendeshea shughuli za shamba ndio tatizo.

Sasa wewe unaelezea usimamizi wa vibarua na mambo ya boot wapi na wapi? Lakini hongera kwa kuwa na shamba.

Kwa kweli hata mimi nilibaki tu nashangaa
 
Update

Wakuu nashukuru sana kwa nyote mlijiotokeza kunipambania mdogo wenu na kunifanya nirudi katika mstari, Mungu awabariki nyote nyote ikiweka brother Ushimen kwa kunipa changamoto ya kutafuta kazi na kunisaidia katika maswala ya uandishi nilikuwa mweupe sana, pia kuna wadau 2 wengine sijajua ID zao ila mmoja alikuja hadi shamba nakushukuru kaka sana kwa kunitia moyo na nitapambana ubarikiwe, wa wa tatu huyu anahitaji shamba nadhani nitafaulisha heka 3 ili nibaki na tano nizihudumie japo mbili ndio zitakuwa kipaumbele sana...

Huyu mdau wa Mwisho kaka kutoka Arusha aisee Mungu akubariki sana broh tena sana kama nilivyokuhaidi nitatenda hivyo hivyo kwa kadiri Mungu atakavyonibariki huyu brother anijui wala ajanifahamu lakini ameniamini na amenisaidia kwa kiwango cha kimataifa kabisa jamii forum ina watu wazuri mno iishi milele... kaka Thom heshima yako ikufukie nathamini sana uwepo wako na ulipotoa uzidishiwe mara 10, ahsante kwa kuniamini na nimedhaminika...

Nakaribisha wadau wengine pia tusaidiane kwa hali na mali nawashukury ninyi nyote wengine tuendelee kuwasiliana kwa kawaida nadhani nishatengeneza ndugu sasa mbarikiwe, nimechelewa kuleta update maana nilikuwa busy kidogo kukamilisha nilichokianzisha shukrani wadau, VIVA JAMII FORUM!

Aisee ushimen is a very great person

Hongera Kwa kupiga hatua
 
Aisee kwanza hongera na pole sana kwa mapito hayo.
Kwenye njia ya mafanikio kuna vikwazo vingi mno na vya kukatisha tamaa.
Kilimo ni fursa nzuri ila usiombe yatokee majanga, Mimi binafsi kilimo kiliacha nipatwe na ugonjwa wa moyo, niliacha kazi, niliitwa tapeli, nilipoteza ndugu na marafiki wote, niliacha masomo ya juu wakati nimelipa hela zote, niliuza kila asset yangu mpaka mashamba yenyewe na vifaa vyake na sikupata ahueni hata robo, yaani matatizo yalizidi mpaka nikawa nalala njiani. Watoto wangu wote waliacha shule hata nisijue naanzia wapi.
Ushauri wangu usijaribu kukopa tena au kutumia asset zako zote kwenye kilimo ambacho bado hujajua soko lake au ustawi wake utakuwaje huko shambani hasa kilimo kinachotegemea mvua.
Kama utapata kazi weka nusu ya hela kwenye hiyo ndoto yako huenda sera zetu za kilimo cha biashara zitakuwa nzuri baadae.
Mwisho kabisa usikate tamaa, omba Mungu sana, na yamekukuta ukiwa bado huna familia kubwa na umeweza kukwepa madeni mengi.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom