Nimekamilisha taratibu zote za mirathi, lakini miezi 2 sasa mahakaman haijalipa fedha za mirathi

wakikosi

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,354
1,483
Waungwana naomba niwashirikishe jambo hili,kesi ya mirathi ilifunguliwa ikaisha,na nyaraka za kuhamisha fedha toka bank ambako marehemu aliweka fedha kwenda kwenye akaunti ya mahakama zilishapatikana na kuchukuliwa na muhasibu wa mahakama na ili kuandaa faili kwa malipo.

Lakini ni mezi 2 sasa hela hazijalipwa,ukienda mahakamani muhasibu anakwambia ukaguzi bado unafanyika, mara ukaguzi mara 3 wa faili.

Naona sarakasi na ucheleweshwaji ni mkubwa, sasa naomba ndugu zangu kama kuna utaritibu fulani au kuna sehemu naweza kwenda ili fedha hizo zilipwe mapema maana muda unaenda sana na muhasibu majibu yake hayanifurahishi.

Nifanyeje ili hela hizo zilipwe mapema na kwa wakati maana taratibu zote nimekamilisha tatizo ni mahakama tu inachelewa sana kulipa hela hizo
 
Pole mkuu. Naomba nikujibu nikiwa kama muelewa wa jambo hili coz nimepita huko mala kadhaa . Baada ya mahakama kupokea faili kutoka benk kinachofuatia ni hazina kuruhusu fedha na kutoa taarifa kwa mahakama kua Sasa mlengwa apewe.

Hapo mahakama hua haifanyi ufuatiliaji wowote hazina zaidi ya kusubili tu.

Kwa uzoefu mala nyingi msimamizi wa mirathi ndio hua anatakiwa kuipush hazina ili i approve malipo haraka. So jiongeze hata kwa visenti kidogo ili Mambo yaende
 
Mpaka nimeshaikatia tamaa hiyo. Alifariki bro. Ameacha mtoto mmoja. Nimefuatilia bima wakamaliza wakairudishia mahakama. Huko mahakamani wanapiga chenga tu mkoani. Mwaka wa 4. Mpaka nimekata tamaa. Mtoto wa marehemu anajua nilishapewa,japo niliandika akaunt yake.
 
Pole mkuu. Naomba nikujibu nikiwa kama muelewa wa jambo hili coz nimepita huko mala kadhaa . Baada ya mahakama kupokea faili kutoka benk kinachofuatia ni hazina kuruhusu fedha na kutoa taarifa kwa mahakama kua Sasa mlengwa apewe...
Maana mimi natakiwa kwenda hazina sasa kwa njia zangu ili nifanye michakato mambo yaende au sio mkuu?
 
Waungwana naomba niwashirikishe jambo hili,kesi ya mirathi ilifunguliwa ikaisha,na nyaraka za kuhamisha fedha toka bank ambako marehemu aliweka fedha kwenda kwenye akaunti ya mahakama zilishapatikana na kuchukuliwa na muhasibu wa mahakama na ili kuandaa faili kwa malipo.

Lakini ni mezi 2 sasa hela hazijalipwa,ukienda mahakamani muhasibu anakwambia ukaguzi bado unafanyika, mara ukaguzi mara 3 wa faili.

Naona sarakasi na ucheleweshwaji ni mkubwa, sasa naomba ndugu zangu kama kuna utaritibu fulani au kuna sehemu naweza kwenda ili fedha hizo zilipwe mapema maana muda unaenda sana na muhasibu majibu yake hayanifurahishi.

Nifanyeje ili hela hizo zilipwe mapema na kwa wakati maana taratibu zote nimekamilisha tatizo ni mahakama tu inachelewa sana kulipa hela hizo
...Penye Udhia penyeza Rupia...!
 
Back
Top Bottom