Nimekamatwa kwa kukutwa nachezesha Playstation.

dumbi

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
868
1,000
Katika hiyo biashara kukamatwa ni kama sehemu yake ya uendeshaji biashara ingawa siyo fair.

Niliwahi kukamatwa saa 7 usiku nilikua wazi mpaka mida hiyo.

Niliwahi kukamatwa asubuhi saa 5.

Niliwahi kukamatwa saa nne asubuhi.

Anyway katika ishu zote walitaka pesa. Mara zote nilizozungushana nao sijawahi toa pesa zaidi ya 20K. Hata hivyo mimi nija ID ya Mjasiriamali so walivyosema kuhusu kodi nikawaonyesha id.

Kwakua umesema umegoma kutoa pesa basi kitakachofuata ni kuzungushwa kwa muda mrefu na siku kesi ikienda mahakamani basi mashtaka hayatokua kuchezesha play station.

Niamini mimi.
Mashahidi wapo waliiona nimekamatwa kwa ajili ya PlayStation kesho naenda kucheza karata ya mwisho wakibug hawatoweza kunishtaki kwa kosa lingine.
 
Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
1,216
2,000
Mashahidi wapo waliiona nimekamatwa kwa ajili ya PlayStation kesho naenda kucheza karata ya mwisho wakibug hawatoweza kunishtaki kwa kosa lingine.
Hamna watu wana roho mbaya kama hao watu, we wape ela achana nao, africa hamnaga haki, ukijidia unasimamia haki, unaweza shangaa kesi inabadilika na utaambiwa umekutwa na misokoto ya bangi.

Waliofungwa jela sio wote wenye hatia.

Rushwa haiwezi kuisha daima.
 
Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,938
2,000
Mashahidi wapo waliiona nimekamatwa kwa ajili ya PlayStation kesho naenda kucheza karata ya mwisho wakibug hawatoweza kunishtaki kwa kosa lingine.
Stupid!Unasababisha watoto waache kuzingatia masomo.Peleka hiyo Play Station kwa watoto wako ucheze nao.Kujiliza JF hakutosaidia.Marabook!
 
dumbi

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
868
1,000
Ngoja uuone moto wa serikali ndiyo utamjua nani ni mshamba na nani bwege.Narudia:Kama una watoto ni vema hiyo PlayStation ucheze nao na mama yao awe anaandika mshindi.Maana hujui kama hujui.
Watoto wangu tayari wanayo PS4 na wanacheza kuna lingine?
 
marinetive

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
316
500
pole sana mkuu!! naamini watakuacha ukifata wnachokitaka..iBTW nilikua naomba ABC za kuanzisha biashara hii mana nina mpango huo siku kadhaa.. sasa sjui wapi naanzia.. yan vitu vya muhimu vinavohitajika.. kwa kuanzia..tafadhali.
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
22,678
2,000
Mashahidi wapo waliiona nimekamatwa kwa ajili ya PlayStation kesho naenda kucheza karata ya mwisho wakibug hawatoweza kunishtaki kwa kosa lingine.
Na wenyewe watakua na ushahidi wa mashtaka watakayokupa.

Kwani una miaka mingapi? Naona kama una illusion hivi
 
ngawia

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
450
500
Wazaz wanalalamika kwa mwenyekiti then mwenyekiti anamwambia polisi then unakamatwa. Kosa hawakosi kwanza Una lesen ya biashara
 
dumbi

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
868
1,000
pole sana mkuu!! naamini watakuacha ukifata wnachokitaka..iBTW nilikua naomba ABC za kuanzisha biashara hii mana nina mpango huo siku kadhaa.. sasa sjui wapi naanzia.. yan vitu vya muhimu vinavohitajika.. kwa kuanzia..tafadhali.
Usijali njoo pm kma upo dar itakuwa vizuri zaidi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom