Nimekamata vitabu vya NDOA YANGU, NINGEJUA - vilivyoibwa

kautipe

Member
May 6, 2011
64
6
Ndugu wana jamii, nimesukumwa kuwaandikia wenzangu katika forum yetu, kuwataarifu na hasa kumtaarifu Bw C. Misango ambaye ni mtunzi wa kitabu kiitwacho NDOA YANGU, NINGEJUA kwamba jana mchana mjini moshi, nimekuta nakala ya kitabu hicho kwa muuzaji mmoja akiviuza kwa bei ya shs 10,000/= kwa nakala. kwa kuwa huyu mtunzi aliwahi kutoa tangazo katika chombo kimoja cha habari akilalamika kuibiwa kwa vitabu vyake na kutuomba wale wote wenye mapenzi mema kumsaidia kufichua wezi hao, nimeona nimjulishe kwamba ndugu huyo ambaye alikuwa na nakala zaidi ya 250, nimemkamata na kama atasoma ujumbe huu awasiliane nami haraka kwa email yangu nimsaidia aweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwizi wake. Kitabu hicho najua kinauzwa shs 5,000 tu lakini kwa sababu ni adimu na kinatafutwa sana ndio maana baadhi ya watu wanakilangua
 
Kwani na yeye ni member wa JF?
 
Back
Top Bottom